Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimpongenza Balozi Liberata Mulamula kwa kazi nzuri aliyoifanya katika sekreterieti ya Maziwa Makuu kwa miaka mitano. Pembeni ni Dr Asha-Rose Migiro Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa walipokuwa katika hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongoji cha Munyonyo nje kidogo ya Kampala kunakofanyika mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) ambapo Balozi Mulamula ndio amemaliza rasmi muda wake wa kufanya kazi kama Katibu Mtendaji wa ICGLR na kumuachia kiti Prof Lumu Alphonse Ntumba Luaba (59) wa DRC.
Rais jakaya Kikwete (kulia,mbele) akiwa na viongozi wenzie wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) kwenye picha ya Pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...