![]() |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindunzi Dk Ali mohd Shein |
Na Zahira Bilal Said-Maelezo Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindunzi Dk Ali mohd Shein ameitaka mamlaka ya maji itoe elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa vianzio vya maji katika sehemu mbali mbali hapa Nchini.
Amesema hivi sasa ulimwengu unakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji hivyo nivema kwa jamii kuelewa umuhimu wa uhifadhi wa maji Nchini.
Dk shein ametoa wito huo wakati akiwa katika ziara ya kutembelea vianzio mbali mbali vya maji ambavyo alivitembelea leo hii katika ambavyo ni pamoja na Saateni ;Mtoni, Welezo, Dole na Mwanyanya .
Aidha Dk Shein ameutaka uongozi wa mamlaka ya maji Zawa uanzishe vipindi maalumu kwa kupitia radio na televisheni vitavyoweza kusaidia kutoa taaluma kuhusu maswala ya maji kwa watumiaji katika sehemu mbali mbali hapa Zanzibar
Pia ameitaka mamlaka ya maji kuimarisha ulinzi katika vianzio ili kuepusha uvaminzi katika vianzio vilivyo karibu na wananchi
Hata hivyo amesema ongezeko la watu pia linasababisha kuengezeka kwa tatizo la upungufu wa maji kwa watumiaji
Mapema Mkurungenzi wa Mamlaka ya Maji Mustafa Ali Ngaru amesema moja ya sababu ya upungufu wa maji ni ukosefu wa mvua ambayo hutokana na ukataji wa miti ovyo na mabadiliko ya hali ya hewa
Vile vile Mkurungenzi huyo wa mamlaka ya maji ameitaka serikali kuwapatia vifaa kwa ajili wa kutoa huduma nzuri kwa wananchi na kuweza kuwapatia maji kwa uhakika zaidi
Aidha mkurungenzi huyo ameseama katika kulipatia ufumbuzi tatizo la maji ni vyema kuendelea kuchimba visima kwa wingi maeneo mbali mbali ya mijini na vijijini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...