Kutokana na mvua kubwa zinazonyesha maeneo mbali mbali ya reli ya kati, Uongozi wa TRL umeamua kuchukua uamuzi mgumu wa kufuta safari zote za treni za abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kuanzia leo Jumanne Desemba 27, 2011 hadi itakapotangazwa vinginevyo!

Kwa hivyo basi abiria wote waliokuwa wamepanga kusafiri leo na pia katika treni zijazo wanatakiwa kufika na tiketi zao katika ofisi za Mastesheni Masta husika ili warejeshewe fedha za nauli walizolipa!

Atakayesoma au kusikia taarifa hii awaarifu wenziwe!

Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbubufu wote utakaojitokeza!

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano : Kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji

(Signed):

Midladjy Maez
Meneja Uhusiano -TRL
Dar es Salaam.
Desemba 27, 2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Huwa nasikitishwa sana na jinsi huyu jamaa anavyojidhalilisha kwa kubadili jina lake ili lionekane lina mwelekeo wa kimagharibi!Niliambiwa na mtu mmoja anaemfahamu vizuri huyu mheshimiwa kuwa jina lake ni Miraji Mahezi lakini amelazimisha kulichakachua ili lionekane ktk muonekano huo.Waswahili walisema mkataa kwao mtumwa,na mwenye kujikataa mwenyewe jinsi alivyo nae ni mtumwa.Jivunie chako kwa kila hali!!!!!

    ReplyDelete
  2. Mbona hamjasema plan b? Maana kuna wengine wamefiwa, wanawagonjwa na wanakwenda shule. Vipi Tz tunafika au tuhamie nchi za jirani?

    ReplyDelete
  3. Duuh kama kweli basi hii ni kali!

    ReplyDelete
  4. Mbona tumesafiri na mvua muda mrefu tu. Angetuambia labda reli imeng`oka inatengenezwa tungemuelewa. Kwa tamko la huyu mtu angeng`oa na reli kabisa ili watu wa Kigoma tujue hatuko TZ.

    ReplyDelete
  5. Anawakwepa ndugu zake wakija kumtafuta kwa jina la Miraji wasimpate. Tabu kwelikweli. Jamaa nomaaa.

    ReplyDelete
  6. Wajamani mimi Mwakei Karumanzira ,uwiiii tereni imesimamishwa,,,,,maisha Dari Salama yamenishinda !,,,ada ya chumba inakwisha 31 Disemba,2011 na vile narikuwa nimekata tikiti ya li tereni narikuwa narudi nyumbani Kaliua-Tabora kukata mkaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...