Kwa niaba ya kamati kuu ya TANZ UK na kwa niaba ya Watanzania waishio Uingereza tuna penda kutuma rambirambi zetu za dhati kwa watanzania wenetu waliopoteza Ndugu, Rafiki au Jamaa zao kwa vifo vilivyo sababishwa na janga la mvua kubwa iliosababisha mafuriko. Dua zetu ziuwendee marehemu wote katika jiji la Dar es Salam na pengine popote Tanzania.
Pia tonamwomba Mwenyezimungu awaape nafuu na haraka wale waliojeruhiwa na awape uvumulivi wale waliopoteza mali zao na kupata hasara kubwa ikiwa ni pamoja na kupoze nyumba zao.
Pia tonapenda kuipongeza serekali na vyombo vyake vote kama jeshi la polisi, Watumish wa wizara ya Afya Vikosi wa zimamoto Jeshi la Wananchi Watanzania na bila ya kuwasahau Wananchi wa kawaida waliojitokeza katika kusaidia juhudi za uokoaji kwa kuwania maisha ya Watanzania wenzao.
Janga hili niletu sote Watanzania, tuungane katika kuomboleza na katika kuasadia walio fikwa na maafa.
Tujiweke tayari kujenga na kukarabati Miundombinu iliyoharibiwa. Tuwe pamoja chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais na Serekali yetu tukiweka mbali tofaouti zetu za kisiasa na nyinginezo. Kama tunavoona janga hili halikuchagua Mfuasi wa Chama cha Siasa au wa Dini fulani.
Mwisho tunatoa pole kwa mheshimiwa rais na kumwomba ajipange vema na viongozi Wafuasi toka pande zote ili kupambana na Janga hili na sisi wananchi tutakua nao bega kwa bega katika juhuda za ukarabati baada ya maafa.
Kwa Wenyeviti na Makatibu wa Mtawi TANZ UK zindueni mifuko ya Pole kuwachangia Wananchi wenzetu walioathiriwa na Janga hili.(Asanteni)
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Tubariki Watanzania.
Dessa M Makoko.
Kaimu Katibu Mkuu TANZ UK.


Sasa tusemeje, huyu jamaa kukaa sana uingereza amesahau kiswahili au muandishi alie andika hii ndio anamatatizo ya kuzingatia anacho kiandika!!?,humu wanasoma wengi,kabla ya kutoa kitu ni vema kukipitia kwanza kuona kama kipo sahihi ndipo kitoke kwa wasomaji,au ndio tatizo la shule za leo?waandishi wa Tanzania jipangeni,enzi za mwalimu kwa uandishi kama huu kesho kazi hauna.
ReplyDeleteHao Uk maneno hata pounds tano imewashinda.
ReplyDelete