Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA OYEEEE!!!

    MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!

    Hakuna atakayeweza Kuishusha Paradiso kuja hapa ardhini bila kuwa na mapungufu yeyote,,,sio kweli kusema hatuna maendeleo kabisa!!!.

    1.Yapo mafanikio tuache unafiki kwa vile pana vitu huwezi tathmini kwa macho ila VIPO ni hatua kubwa!.

    2.Cha msingi hii tofauti iwe ndio kipimo cha kujituma ili tuende na wakati kufikia mafanikio halisi tunayotarajia!

    3.Sio tuache mzigo na lawama kwa viongozi tu, inabidi na sisi wananchi kujituma, ili kama viongozi wasipotekeleza tuweze kuwawajibisha vile watakuwa na la kujibu, Raisi wa zamani wa Marekani Bw. Kennedy aliwahi kuwauliza Waamerika kuwa msiulize serikali itawafanyia nini ila mseme ni nini mtafanya kushirikiana na serikali kufikia maendeleo!

    Na tuache kubeza licha ya mapungufu angalau hata hatua ndogo tuliopiga kimaendeleo!

    ReplyDelete
  2. Naona miaka 50 ya uhuru sasa tumeChinika rasmi, safi sana! Mambabu zetu na asili zenu mlie tu, mmekuwa sio vipaumbele tena, mtajiju!

    ReplyDelete
  3. Wewe mtoa maoni wa kwanza sina uhakika kama kweli unaweza kupambanua mambo! Umri wa miaka 50 ni mkubwa sana. Binadamu mwenye miaka hamsini anaitwa mzee. Sasa inakuwaje taifa zee liitwe taifa changa, huu ni upotoshaji.

    Nchi inaongozwa na viongozi wabinafsi, haiwezi kuendelee kwa jinsi hii, hata miaka 100 ijayo. Labda kije kizazi cha kujali maslahi ya umma, badala ya kizazi hiki kinachojali maslahi binafsi.

    ReplyDelete
  4. Anonymous wa Fri Dec 09,0957:00 PM 2011

    Wewe unaemkosoa mtoa maoni wa kwanza, unafikiri Dira ya Maendeleo (Develompent Vision) inapangwa na kuona matokeo ndani ya miaka 50 tu?

    Watu wanachukua makarne kwa makarne mfano nchi zilizo endelea hawakupata wala kukipanga jana au juzi hiki walicho nacho leo imewachukua muda!.

    ''WEWE NDIO UNAONYESHA HAKUNA UHAKIKA KUWA UNAO UWEZO WA KUPAMBANUA MAMBO''

    Unafikiri maendeleo yanakuja kwa pupa kama zako ambazo ni za wanasiasa wenye jazba...kalaga baho hawa wengi wankuwa na malengo binafsi!!! wakipata uongozi imekula kwetu.

    Inachotakiwa kama malengo yapo kama alivyotoa maoni ya kwanza halafu hayakufikiwa kama unavyodai ktk kipindi hiki cha miaka 50, hivyo ndio nafasi ya kupima upungufu uliopo na kuweka target ya kuyafikia.

    Uelewe maendeleo hayaji kama mvua au kwa kubadili utawala ,sio kigezo, kwa taarifa yako zinaweza kuja tawala mpya tukajuta kuzaliwa!

    Historia inatuonyesha mfano Zambia, walifanya mabadiliko ya utawala kwa kishindo wakitarajia MIUJIZA YA MAENDELEO, watawala wapya wakafikia kufanya biashara za madawa na Ufisadi matokeo yake wanamageuzi wakawa majambazi zaidi na kuifilisi nchi.

    Na kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2011 na kushinda Michael Satta Zambia imerudi kwenye muelekeo wa waliyemkataa kabla mwasisi wake Kenneth Kaunda!

    ReplyDelete
  5. nyote mmechangia vizuri lakini kumbuka miaka 50 ya uhuru wa tanzania bara una mapungufu mengi kuliko mafanikio.mfano wizara ya afya imetoa offer ya watanzania kupewa matibabu bure kwa wiki mbili pale viwanja vya mwl nyelele lakini ukifika utaona wingi wa watanzania wanavyo gombania kumuona dakitari huku msululu mkubwa usioisha ukiwa kwenye banda la kuchukulia dawa(MSD)Cha kujiuliza wale waliopo vijijini wamepata huduma wapi? si ndio wanakufa?. lakini pesa nyingi imetumika kugharamia sherehe hizo kwanini tusiwaseidie watanzania wanaoitaji tiba?.pia jiulize ndani ya miaka 50 ya uhuru ni watumiwa wangapi wamefungwa au kupewa adhabu kali na mahakama ya tanzania kwa kosa la rushwa/ufisadi?.lakini wengi waliofungwa ni kwa wizi wa vitu vidogovidogo.Hivi ni kweli Tanzania nimasikini? au tunatiwa umasikini na baadhi ya watanzania ambao baadhi yao wanajisafisha na gamba lisilovulika?

    saa imefika ya kuwauliza viongozi wetu mmefanya nini kwa ajiri ya watanzania?

    ReplyDelete
  6. Uhuru wa mawazo ni haki ya mtu lakini hoja za msingi ndiyo jibu sahihi na la mwisho.
    Kwa kusema kuwa tumeendelea sawa lakini je kwa kiasi kipi?Unapo kuta kuwa kuna mgawo wa umeme,shule hazifaulishi na kila kukicha afadhalia ya jana utasemaje eti tume endelea. Tunako enda ni kubaya kuliko tuliko toka na hatuna mwelekeo.
    Ndiyo maana mtu yuko form one hajui kusoma wala kuandika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...