Wazalendo wenzangu,

Naomba nichukue fursa hii kuwapa pole wote kwa namna moja au nyingine kutokana na maafa yaliyosababishwa na mvua hizi zinazoendelea katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi yetu.

Ni dhahiri kuwa waliothirika ni wengi na hivyo basi watakuwa na mahitaji muhimu ya dharura . Hivyo basi ni wakati wa kusaidiana na kufarijiana , pale unapoweza basi msaidie mwenzako aliyeathirika.

Naomba nichukue fursa hii kuwaomba wote wenye nia ya kuchangia waliothirika na maafa haya basi wawasiliane na TPN Staff Miss. Anna Machanga machangaanna@yahoo.com0652 945422 ; na Mr. ASED KIPEPE: sdkipepe@gmail.com0716 898685 . Michango inayopokelewa ni fedha taslimu au hundi, vifaa vya nyumbani, vyakula, vinywaji, nguo mpya na zilizotumika n.k.

Kama unataka kuchangia kwa M-Pesa , Tigo Pesa, Airtel Money etc wasiliana na Mr. Gervas Lufingo +255 (0784/0767/0658) 48 25 97  : nasemaasante@yahoo.com

Wafanyakazi  hao wa TPN watakufuata ulipo na kupokea mchango wako na kukabidhi risiti.

Michango yote itakayopatikana itawekwa hadhani na  itawasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa DSM, Mhe. Mecky Sadik kwa ajili ya kufikishwa kwa waathirika.

Kutoa ni Moyo na wala si utajiri.

Nachukua fursa hii kuwatakia wote siku kuu njema ya Krismas kwa wale wanaosherehekea, mapumziko mema ya mwisho wa mwaka na pia nawatakia wote mwaka mpya mwema na wenye mafanikio tele.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Mungu awabariki wote.

Phares Magesa
Rais- TPN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwenu TPN, nimeperuzi ktk tovuti yenu www.tpntz.org isipokuwa nimekuta e-mail:president@tpntz.org na namba ya simu 0784-618320 kitu ambacho anuani za barua pepe mlizotoa ktk blogu na namba za simu ktk tovuti hazifanani!,,,,,sasa hapo vipi?

    Masuala haya ya hisani na uwajibikaji kwa jamii yanataka zaidi uwazi zaidi ya nia na kujituma!

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza hapo juu hata na mimi naungana na wewe,

    Unajua hata kama pana mabadiliko ya namba za simu ilibidi taarifa ya ktk Blogu ifafanue hayo na siyo kubandika tu namba mpya za simu na anuani mpya za barua pepe.

    Licha ya kuwa ktk Blogu mwenye kutoa taarifa pale chini ni Raisi (President) wa TPN ndugu Phares Magesa na inawezekana ndie mwenye e-mail:president@tpntz.org ,Tatizo panapatikana maswali mengi kuliko majibu mojawapo:

    1.Kwa nini asitumie mawasiliano halisi kama kwenye tovuti?

    2.Kama hakuna maelezo ya mabadiliko ya mawasialiano watu wataelewa vipi kama mtoa taarifa ndio wahusika halisi wenyewe au mhusika halisi mwenyewe?

    3.Kama hawakutumia mawasialiano ya Kiofisi kama namba halisi ya simu na kupitia anuani ya barua pepe ya tovuti www.tpntz.org wakatumia yahoo na gmail watu watakuwa na uhakika gani juu ya uwazi wa suala zima?

    WAJAMENI HAYO NI MAONI BINAFSI NA SIO UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...