
Marehemu alifariki tarehe 7/10/2011 kwenye Hospitali ya KCMC Moshi, baada ya kuugua kwa muda mfupi na kuzikwa tarehe 11/10/2011, Usseri, Rombo. Misaada yenu na jinsi mlivyoguswa na kuomboleza msiba huo, lilitupa nguvu ya kupokea kifo cha mpendwa wetu.
Ni vigumu kumshukuru kila mtu, tunaomba kwa moyo mkunjufu kila mmoja apokee shukrani zetu za dhati kwa misaada yenu mlioitoa wakati wa kumuuguza marehemu wakati alipokuwa amelazwa KCMC na kipindi chote cha msiba.
Tungependa kutoa shukrani za pekee kwa madaktari na wauguzi wa KCMC; Jumuiya ya Mtakatifu Martha (Parokia ya Reha); Muungano wa Jumuiya nne ya Mtakatifu Christogone (Parokia ya Reha); Wafanyakazi wa NMB, Moshi; Wafanyakazi wa Kiliwater Company Limited, Mkuu, Rombo; G32-KNCI JVE Limited; Tarakea Rural Cooperative Society Limited; Kikundi Wazee Wastaafu, Tarakea; Wafanyakazi wa Kilimanjaro Cooperative Bank; Wafanyakazi wa WIOMSA, Zanzibar; Wafanyakazi wa TCMP, Bagamoyo; Wafanyakazi wa Departments of Zoology and Wildlife Conservation na Aquatic Sciences and Fisheries, University of Dar es Salaam; na Wanachama wa Kikundi cha MIBS.
Pia tunawashukuru kwa huduma za kiroho za Mapadre wa Makanisa ya KCMC Hospital na Parokia ya Reha (Rombo) na Wachungaji wa Kanisa la KKKT, Usharika wa Karanga, Moshi Mjini.
Tunawaomba nyote muungane nasi katika kumuombea marehemu apate punziko la milele
MUNGU AMETOA, MUNGU AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...