Mwenyekiti wa TANZ UK Taifa Bwana John Lusingu akisisitiza jambo kufungua hafla.
Wengine katika picha ni wajumbe wa Kamati Kuu ya TANZ UK Taifa-kutoka kushoto ni Frida Kusamba (Leicester), Dessa Makoko (Coventry) na Nelly Nsemwa (Sekretarieti ya Jumuia ya Madola)
 Ukumbi ulifurika, wanachama, marafiki na wapenzi walikuwa makini kumsikiliza Mwenyekiti alipokuwa akifungua hafla kwa hotuba ya kusisimua.

 TANZ UK Leicester inatoa mwito kwa wadau kuchukua fomu za kujiunga. TANZ UK haibagui, watanzania, wasio watanzania wana nafasi sawa ya kujiunga uanachama
Wasiliana nasi kwa maelezo:
tanzukleicester@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. KABLA HATUJAJIUNGA,KWANZA BORESHENI MAANDALIZI YA UKUMBI WA MIKUTANO,UTADHANIA TUPO BONGO..NA HASWA HIZO CHUPA ZA MIRINDA HAPO KWENYE MEZA..LOL

    ReplyDelete
  2. UKUMBI ULIFURIKA .... HA HA HA ANKAL KUMBE WEWE MSANII

    ReplyDelete
  3. Jamani ee Nyumbani Raha yaani Bongo ni Raha tupu; hapo unaona tu watu walivyo kaa bila uhuru kama wakimbizi kwenye nchi za watu inatia huruma kwa mtu anayeweza kusoma picha hii utaweza soma nyuso za watu and what is going on into their mind.

    ReplyDelete
  4. Duu! mamtoni na vijuice vya AZAM! tetetetete!

    ReplyDelete
  5. Eeenhe majuu kuzuri kweli! Sitaki kusema mengi ila ukiangalia hii picha mengi yaweza kusomeka!

    ReplyDelete
  6. Haya wee buy one get one free, kwanza ni £0.50 mlishindwa kununua vinywaji vinavyoonyesha mko ulaya?

    ReplyDelete
  7. MIMI SIPENDI PENDI KUPAYUKA KUTOA MAONI, LAKINI LEO NIMESHINDWA KUJIZUIA.
    WACHA NISEME KIDOGO.
    NI UTUMWA KUKATAA NA KUCHUKIA KWENU, NA LABDA NDIO MAANA MACHO YA BAADHI YA WADAU YAMEUONA MKUTANO HUU UMETAWALIWA NA SIMANZI KIDOGO. MIMI NILIKUWEPO KIKAONI, M'KITI WA TANZ UK TAIFA ALIKUWA AKIWASILISHA TAARIFA YA ZIARA YAKE ALIYOIFANYA TZ HIVI KARIBUNI. KAMA WADAU MNGEKUWEPO NA NYINYI PIA MNGEONEKANA KAMA WAKIMBIZI, LABDA KULIKO HATA SISI.
    UNAJUA ULIMWENGU UMEHARIBIKA SASA, KILA ALIYE MBALI MAMBO HAYAKO SAWA.
    TUNA HAMU KUBWA KURUDI NYUMBANI, NI KWETU, LAKINI KILA TUKIELEZWA HALI ILIVYO, RUSHWA, UFISADI, CHOYO NA WIVU, UVIVU NA UZEMBE MAOFISINI, SISI WENYEWE TUNASHINDWA KUSHANGAA. NDIO MNATUONA HAPA TUMEISHIWA NGUVU, KWANI TULIYOSIKIA TOKA KWA M'KITI YANATISHA, NYUMBANI KUNAAMSHA ALARM YA KUKATA TAMAA.
    TWAPENDA TURUDI, TUJE KUWEKEZA, TUJE KUANZA UKURASA MPYA WA MAISHA, LAKINI IKIWA WEWE MTOA MAONI TU UNATOA MANENO YALIYOJAA WIVU NA HUSDA, ITAKUWAJE WENGINE?
    NA SIMAANISHI WOTE, LAKINI MIFANO IKO KIBAO, WADAU HAWAPENDI SOMEHOW KUONA WENZAO WAKIJIKWAMUA DHIDI YA SHUKA LA UMASKINI.
    MSIONE TUKO HUKU MKATUONEA WIVU, TUMEKUJA KUTOKANA NA SHINIKIZO LA MAISHA, KAMA NYIE WENGI MLIOKIMBIA VIJIJI VYENU MKAKIMBILIA MIJINI, MKAJIFANYA MA BORN TOWN KUMBE NI WA KUJA. SISI NASI TUMEPEPERUKIA HUKU.
    TUSICHEKANE, TUMEKUJA KUTAFUTA. TENA NYIE WENGINE MNAOJIDAI KUKIPAKA NDIO NYIE NYIE HAMWISHI KUAGIZA VIWARO NA MAGARI NA MAFRIJI NA MATV, ETI YA MCHINA NI KANYABOYA.
    HUSHANGAZWA SANA NA NAMNA SHEREHE ZA NYUMBANI ZILIVYOJAA KUPONDA PESA. UKURASA WA BLOGU YA JAMII HUJAA MAPICHA, WADAU WAMETINGA VIWARO VYA BEI MBAYA, MAPARTY YA GHARAMA KUBWA KUBWA, KUMBI ZA MAMILIONI, MAVYAKULA KEDEKEDE. MAPESA HAYO YANATOKA WAPI KAMA SI UFISADI?
    TZ IPI YENYE UTAJIRI HUO WA MATUMIZI YA OVYO?
    UKENDA HOSPITALI HALI INATISHA! USAFIRI KIAMA KITUPU, BARABARA HAZISHI KUUA. BADALA YA WADAU KUKODOA MACHO SISI HUKU TUNAISHI VIPI, BORA MJIULIZE, KAMA SISI TUFANYAVYO, NI LINI TZ YETU INAONDOKANA NA MAISHA DHALILI WALIONAYO RAIA WENGI. MSIJALI KUHUSU SISI, ALHAMDULILLAAH MAISHA SI HABA, KIMSINGI TUMETIMIZA MAHITAJI YOTE YA KAWAIDA KWA BINADAMU, KUANZIA USAFIRI, KULA, MAVAZI, ELIMU, AFYA, NK.
    HAPA UKEREWE HAKUNA CHOCHOTE KILICHO BIG DEAL. UNACHOTAKA UNAKULA. GARI UTAKAYO UNAENDESHA, LAKINI WATU HAWAHUSUDU MAISHA YA JUU. MENTALITY ZINAKUTUMA UJIKUNE UJIPATAPO, NDIO MAANA HATA UNAPOKETI KUTAZAMA FILAMU ZA KIBONGO UNAONA ALAMA ZA NDOTO ZA ALINACHA, MAJUMBA MAKUBWA, MAGARI YA BEI MBAYA, NGUO ZA THAMANI KUBWA, KUMBE VYOTE VYA KUAZIMA. HAPA FILAMU ZAO ZINAONESHA REAL LIFE SITUATIONS NA TRADITION YA WENYEJI. HAKUNA ULIMBUKENI, KILA KITU NI NORMAL.
    NDIO MAANA UKUMBI WA SHULE TU ULITUTOSHA KUANDAA HAFLA. UKO SIMPLE, LAKINI NI WA KISASA KABISA, KWA MAANA YA KUWA UNA HEALTH N SAFETY ZOTE. VIWANGO VYA JUU KABISA. SIMPLE.
    WADAU SIKUSUDII KUPONDA KWETU, NAJARIBU KUELIMISHA.
    KWETU NI KWETU, NAKUPENDA KULIKO KWENGINE KOKOTE, NATAMANI LEO NIRUDI NIANZE UPYA, NIELEWENI.
    Mdau ukerewe

    ReplyDelete
  8. Mdau wa Dec 14,02:04:00 AM 2011 Wewe ni Mtumwa tuu huna jipya la kujitetea. Hakuna cha husda wala wivu eti mtu anaishi majuu kwani shida za huko hazijulikani?!

    ReplyDelete
  9. NDUGU YANGU UTUMWA NI MPANA MNO, HUWEZI AMINI.
    MIMI NI MTUMWA SIKATAI, NA WALA SI JAMBO JIPYA KUWA MTUMWA.
    NAHISI KWA KIWANGO FULANI NIMELAZIMIKA.
    SIJUI WEWE UTUMWA KWAKO NI ISSUE KUBWA KIASI GANI, TUMEJIAMULIA UTUMWA, KAMA UUITAVYO, KWA SABABU NYINGI SANA. UNAPOKUWA NA INFERIORITY COMPLEX UNASHINDWA KUWAZA NA KUAMUA, UNADHANI KILA KITU KIKO NEGATIVE.
    MAJUU KUNA ANUAI YA WATZ WANAISHI, KWA SABABU ANUAI. SASA KAMA WEWE FIKRA ZAKO UNAAMINI KILA MTANZANIA NJE YA TZ NI MTUMWA, ENDELEA KUWAZA HIVYO. TUSEMEJE. NDOO ULE WIVU NA HUSDA, ILA NI SHARTI UJUE MIPAKA YAKO, MAANA TUKO WENGI HUKU MAJUU, TUMEKUJA KWA SABABU MBALI MBALI.
    SISI NI WATUMWA, WEWE UKO HURU, HILO HALITAKUBADILISHA WALA HALITATUBADILISHA, UNAJUA UNACHOWAZA NA KUTAMKA NI LUGHA ILIYOKOSA MWELEKEO, YA KITOTO NA NI AIBU KUITAMKA. ILA ELEWA KUWA HUKU MAJUU NDIKO KWA KIWANGO CHA ASILIMIA 99, TAKA USITAKE, KUNAKOCHANGIA MAENDELEO YA TZ UNAYOIONA LEO.
    ULIZA UTAELEZWA.
    ELIMU, AFYA, UCHUMI, MIUNDO MBINU, ORODHA NI NDEFU.
    GIGRII YA UKEREWE HAIFANANI NA YA MLIMANI.
    PAUNI SI SHILINGI.
    NA MENGI TU. TAFAKARI NDUGU YANGU.
    Mdau, ukerewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...