Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea kwa masikitiko taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media Bw. Absalom Kibanda ya kujitoa kwenye Kamati ya Taifa ya kukamilisha mchakato wa kupata vazi la Taifa, Wizara haina pingamizi na uamuzi wake huo.

Wizara imesikitishwa na sehemu ya tamko lake kudai kuwa namnukuu,

“Nimelazimika kufikia uamuzi huu, baada ya kujiridhisha pasipo shaka kwamba mchakato mzima uliohusisha sakata langu kama Mhariri Mtendaji kuhojiwa na kufunguliwa mashitaka na Polisi na hatimaye kufikishwa kwangu Mahakamani usingeweza kufikiwa pasipo kuishirikisha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inayoongozwa na Waziri Nchimbi”, mwisho wa nukuu.

Kwa taarifa hii Wizara inapenda kuutarifu umma kuwa Habari hiyo ni uzushi usio na mashiko wenye nia ya kuharibu uhusiano mzuri uliopo kati ya Wizara na wadau wa Habari nchini.

Kwa mujibu wa majukumu ya Wizara, si sehemu ya kazi za wizara hii kushauri, kuchunguza au kuandaa tuhuma za makosa ya jinai. Ni vema iwe wazi kuwa Wizara hii, viongozi , watendaji, na watumishi wake hawajashiriki, hawajashirikishwa na hawajajishirikisha na hawajashauri wala kushauriwa juu ya tuhuma na mashitaka dhidi ya Bw. Kibanda.

Wizara inavisihi vyombo vya Habari kuendelea kuzingatia weledi, mila na desturi zetu katika kutekeleza majukumu yake.

Imetolewa na,
Msemaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. KUNA VIONGOZI WAMEFANYA KUTAFUTA VAZI LA TAIFA KAMA BIASHARA,HII INAWASHANGAZA WENGI....NYIE SUBIRINI MTASIKIA TU.

    ReplyDelete
  2. Nimefurahi kuwa kajitoa kwenye hiyo kamati ambayo haina tija kwa taifa letu. Vazi la taifa halikaliwi kikao ni kitu kinachopaswa kuja chenyewe kufuatia mila na desturi za wananchi. Sidhani kama kulikuwa na kikao cha Wamasai kuvaa lubega au kwa wahehe, wanayakyusa nakadhalika kuvaa migolole yao.

    ReplyDelete
  3. Karne ya 21 wenzetu wanapanga ni jinsi gani ya kuhamia kwenye sayari ya mars...nyie mnatafuta vazi la taifa....yaleyale ya babu wa loliondo!!!hovyooo..ndo maana kanchi haka hakaendelei...wasomi wengi wa bongo ni ma Zero!!

    ReplyDelete
  4. Mdau wa pili Anonymous wa Sat Dec 31, 03:43:00 PM 2011

    Nakuunga mkono kwa 1000% (kwa asilimia 1000) hawa Viongozi wanapoteza muda na kugharimu pesa ya kodi ya wananchi bure kwa vikao visio na tija!

    WALITAKIWA WAANZIE KATIKA LUBEGA, MGOLOLE NA KANIKI HADI KUFIKIA KUPATA VAZI LA TAIFA!

    ReplyDelete
  5. This is ujinga + hatuwezi pata vazi la taifa kamwe and that is impossible na kwa nini tunahitaji hilo vazi la taifa??? badala ya kushughulikia mambo muhimu na yenye tija na taifa kutoka kwenye wizara watu wanataka kuleta biashara ya vazi lataifa.

    ReplyDelete
  6. huyu nae anatafuta umaarufu tu wabongo du

    ReplyDelete
  7. Mimi huwa nashangaa sana kuona watu wanakaa kikao eti tubuni vazi la taifa! wapi mmesikia mambo haya? naungana na mtoa maoni hapo juu kuwa vazi la taifa ni sehemu ya tamaduni ya jamii husika hivyo huwepo yenyewe kutokana na watu wanavyoishi kamwe hawakai vikao na ndo maana haitawezekana kwa kuwa jamii haitapokea ni sawa na TUKI wanapolazimisha kuleta misamiati ya kutengeneza mezani. Ndege,magari, na majumba yaweza kukaliwa kikao cha namna ya kuunda lakini si utamaduni acheni kutuburuza. heri yako kibanda kujitoa ni uzushi mtupu

    ReplyDelete
  8. Spot on mdau wa pili hapo juu, wot a waste monies and time. Hizo sitting allowance wanazolipwa zinaweza kujenga 10 secondary schools. Nchimbi wake up, una digrii ya falsafa, I thought that would help you to analyse things and think strategically. Wots important kwa mtu mitaani, health, food, education. JK hawa mawaziri unatoa wapi. Come on Mwanyika and the Kabwe, wots your opionion on this!!!!!!Historically nguo zililtwa na wakolono, so tuvae ngozi na matawi ya miti - this will be interesting on wot crap you come up with which will be shoved into poor wanabongo.

    ReplyDelete
  9. MIAKA 50 YA UHURU LAKINI TAIFA BADO LIKO UCHI.

    ReplyDelete
  10. Mada hapa ni kibanda kujitoa na si vazi la taifa. Huyu kibanda ana mambo ya kitoto sana. Sasa anazira ili iweje. Alijiona untouchable! Pumbavu kabisa. Wewe unawahamasisha askari waasi halfu unsema sio uchochezi? Unakamatwa unalia?

    ReplyDelete
  11. vazi la taifa ni la kimasai au la kimangati tayari mavazi ya taifa yapo nyie hilo vazi mnalotafuta ni vazi lipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...