25 WAITWA TWIGA STARS KUIKABILI NAMIBIA
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars), Charles Boniface Mkwasa leo (Desemba 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Namibia.

Mechi ya kwanza itachezwa jijini Windhoek, Namibia kati ya Januari 14 na 15 mwaka huu, na ile ya marudiano itachezwa Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu itaanza mazoezi Desemba 19 mwaka huu kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Wachezaji waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti ofisi za TFF siku hiyo saa 9 alasiri tayari kwa kuanza mazoezi.

Wachezaji walioitwa ni Sophia Mwasikili (Sayari Women), Fatuma Bushiri (Simba Queens), Fatuma Omari (Sayari Women), Mwajuma Abdallah (JKT), Asha Rashid (Mburahati Queens), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Ettoe Mlenzi (JKT), Zena Khamis (Mburahati Queens), Fatuma Khatib (Mburahati Queens), Maimuna Said (JKT), Fadhila Hamad (Uzuri Queens), Fatuma Mustapha (Sayari Women) na Evelyn Senkubo (Mburahati Queens).

Rukia Hamisi (Sayari Women), Mwapewa Mtumwa (Evergreen), Judith Hassan (TMK), Aziza Mwadini (Zanzibar), Sabai Yusuf (Zanzibar), Semeni Abeid (Tanzanite Queens), Zena Said (Uzuri Queens), Pulkaria Charaji (Sayari Women), Tatu Said (Makongo Sekondari), Mwanaidi Hamisi (Uzuri Queens), Hanifa Idd (Uzuri Queens) na Fatuma Gotagota (Mburahati Queens).

COCA COLA DREAM TEAM KWENDA AFRIKA KUSINI
Timu ya kombaini ya Coca Cola iliyotokana na michuano ya Copa Coca Cola inaondoka kesho alfajiri (Desemba 17 mwaka huu) kwenda Johannesburg, Afrika Kusini kwenye kambi maalumu ya mafunzo ya mpira wa miguu.

Wachezaji 14 wanaoondoka ni Peter Manyika, Abdul Mgaya, Pascal Matagi, Mohamed Hussein, Mbwana Ilyasa, Farid Musa, Suleiman Bofu, Salvatory Raphael, Paul James, Miraji Adam, Kapeta Mohamed na Basil Seif.

Mafunzo hayo yataanza Desemba 18 mwaka huu, na timu itapata fursa ya kucheza mechi kadhaa za kirafiki. Timu hiyo itarejea nchini Desemba 22 mwaka huu.

Desemba 21 mwaka huu timu hiyo ya Copa Coca Cola itashuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) kati ya Orlando Pirates na Golden Arrows itakayochezwa Johannesburg.

Viongozi watakaondamana na timu hiyo ni pamoja na kocha Kim Poulsen, daktari Joakim Mshanga na ofisa kutoka kampuni ya Coca Cola ambayo ndiyo imeandaa na kugharamia safari hiyo.

SEMINA YA KUVUMBUA VIPAJI (GRASSROOTS)
Semina ya mafunzo ya kuhamasisha watoto kucheza mpira wa miguu na kuvumbua vipaji (Grassroots) inamalizika kesho (Desemba 17 mwaka huu) kwa tamasha (festival) litakalofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tamasha hilo litakaloshirikisha watoto 1,200 wa Mkoa wa Dar es Salaam wenye umri kati ya miaka 6-12 litaanza saa 3 asubuhi na kumalizika saa 6 mchana kwa mkutano na waandishi wa habari.

Mzungumzaji mkuu katika mkutano huo atakuwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambapo mbali ya grassroots, pia atazungumzia masuala mengine ya mpira wa miguu ikiwemo kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...