Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Eugen Mikongoti (katikati) akionyesha Tuzo ya Utoaji wa Huduma Bora za kijamii baada ya kuibuka na ushindi wa jumla katika mashindano ya Mashirika ya Hifadhi za Jamii kwa nchi za Ukanda wa Afrika,baada ya kukabidhiwa na Rais wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank Stoove (kushoto) kwenye hafla fupi iliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha usiku wa kuamkia leo.Kulia ni Muweka Hazina wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA),Philippe Conus.
Rais wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank Stoove (kushoto) akikabidhi tuzo mbili za Utoaji wa Huduma Bora za Kijamii kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) William Erio (katikati) katika hafla fupi ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Mount Meru,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi Serikali (GEPF), Daudi Msangi akipokea tuzo ya Utendaji Bora Afrika kutoka kwa Rais wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank Stoove (kushoto) baada kushinda katika mashindano yaliyozishirikisha nchi 19 katika Ukanda wa Afrika. Kulia ni Mweka Hazina wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA),Philippe Conus.
Rais wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA) ,Bw. Errol Frank Stoove (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Eugen Mikongoti (pili kulia) ambaye Mfuko wake ndio Ulioshinda Tuzo ya jumla Utoaji wa Huduma Bora za Kijamii kwa Mashirika ya Hifadhi za Jamii kwa nchi za Ukanda wa Afrika,akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA),Bw. Hans-Horst Konkolewsky Pamoja na Mweka Hazina wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Kimataifa (ISSA),Philippe Conus.

kwa picha zaidi 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. GEPF ni mfuko mdogo lakini kwasasa ndo unaongoza kwa ubora Tanzania hongera ndugu Msangi

    ReplyDelete
  2. Hongera NHIF kuipa sifa Tanzania kwa kuwa washindi wa jumla barani Afrika wakati tukielekea Miaka 50. Hongera GEPF na Hongera PPF. Hongera NSSF kwa kuandaa mkutano huo mkubwa. Kazeni buti.

    ReplyDelete
  3. Mafanikio haya ni mazuri na nadhani yanampa Mdhibiti na Msimamizi wa Sekta ya hIFADHI YA jAMII picha ya nini kifanyike katika utoaji wa huduma za pensheni na bima ya afya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...