Bi Valerie Chilipweli Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) (Kushoto) akimkabidhi kadi ya Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya pamoja na zawadi mbalimbali kutoka TCAA kwa Bi Rahma Jumba Kishumba wa Kituo cha kulelea watoto cha UMRA kilichopo Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam.
Valerie Chilipweli Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) (Katikati)akiwa na Bi Joanna Werner, raia wa Ujerumani (kushoto) mmoja wa walezi wanaojitolea katika kituo cha UMRA na Bi Rahma Kishumba (Kulia) pamoja baadhi ya watoto katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha UMRA.TCAA iliwapatia zawadi mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya krismasi na Mwaka mpya.

Na Ally Changwila

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa zawadi mbalimbali zenye thamani shilingi Milioni 2 kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwenye Kituo cha UMRA kilichopo Magomeni Mikumi Jijini Dar es salaam.

Kutolewa kwa zawadi hizo ni sehemu ya utamaduni wa TCAA kurejesha sehemu ya faida inayoipata kwa kuinufaisha jamii pamoja na kufurahika kwa pamoja na watoto wa UMRA katika kipindi hiki cha Sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya.

Akikabidhi zawadi hizo mbalimbali kwa niaba ya TCAA Afisa Utumishi Mwandamizi Bi Valerie Chilipweli alisema japo kinachotolewa sio kitu kikubwa sana ila TCAA imeona ni vyema kuwapatia zawadi kidogo watoto hao ili walau waweze kufarijika katika kipindi cha sikukuu.

Zawadi zilizotolewa ni pamoja na magunia ya mchele, sukari , mafuta ya kupikia pamoja na Biscuit, akipokea zawadi hizo kwa niaba ya watoto hao , mwanzilishi wa Kituo cha UMRA Bi Rahma Juma Kishumba aliishukuru sana TCAA kwa kujitoa kwao na kuwakumbuka watoto wa kituo hicho.

Bi Kishumba alisema Kituo cha UMRA kina jumla ya watoto 65 kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini, ambapo kati yao wavulana ni 33 na wasichana ni 32.Ambapo pia watoto hao wapo kuanzia ngazi ya chekechea mpaka kidato cha sita.

Alisema watoto wote wanasoma shule kila mmoja katika hatua yake na pia ametoa wito kwa watanzania wengine kujitoa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...