Vijana wa Skauti wa Mkoa wa Morogoro, wakiwa ndani ya lori la kubebea Takataka na wengine wakijiandaa kupanda ili kuelekea kwenye kituo cha mradi unaopitia mbio za Mwenge wa Uhuru 2011 katika Manispaa ya Morogoro, zilizofanyika hivi karibuni, hata hivyo baadhi ya vijana hao walitoa malalamiko kuwa gari maalumu la kusomba uchafu , halikusafishwa na hivyo kutoa harufu kali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Ndio maana ya Skauti, wanalalamika nini sasa? walitaka wapewe VX kama wabunge wa CCM??? kweli Tanzania imepotea kila mmoja anataka aanzie maisha juu yaani kwa haraka, kazi tunayo kwa mawazo hayo potofu.

    ReplyDelete
  2. Kweli Hii Ni Dharau Dhidi ya Ubinadamu!! Lakini ndio Hivyo!! Walitakiwa Watumie Utashi wao wa Kuzaliwa

    ReplyDelete
  3. Haya ndiyo maisha na utawala bora wa Tanzania.Hivi kweli mkoa pamoja na kukakta pesa za walimu kama mchango wa mwnege wa uhuru bado watowato wetu wanaambukizwa magonjwa na kesho wakienda hapo hospital watukanwe na je hiki Kipindupindu na kuhara vitaisha?
    Hapana aliyehusika na kutoka gari hiyo achunguzwe na achukuliwe hatua kali ikiwezekana afukuzwe kazi.
    Je jeshi hawana magari?manispaa hawana magari?CCM mkoa hawana Magari?Jamani HUU NI UHUNI SI UTAWALA TENA

    ReplyDelete
  4. Mbona mlipanda kama lilikuwa chafu? Kwanza sijui kama mna akili ninyi. Hili kweli ni gari la kupanda abiria? Kuweni na msimamo, siyo kuswagwa kama ng'ombe.

    ReplyDelete
  5. Hilo gari lina kila aina ya bacteria.
    Hao vijana inatakiwa wakapimwe afya zao as soon as possible.

    Miaka 50 ya uhuru Oyee..!!

    ReplyDelete
  6. hao ni scout ou mgamba waache kudeka tena washukuru wamepata hata hilo gari ilitakiwa watembee kwa miguu mpaka huko hiyo ndio scout waache kuringa.
    wanavunja miiko ya scout

    ReplyDelete
  7. Shame on those responsible in sending this kind of transport to those kids -

    ReplyDelete
  8. diskas lol tangagiza ya wadanyanyika inatia huruma wakati mafisadi wanatumia magari ya mabilioni gari la baba gari la mama na gari la watoto kuwapeleka shule

    ewe mola muumba watie imani na upendo viongozi wetu wawe wenye kutuhurumia walala hoi zaidi ya maombi kwako hatuna njia nyingine hatupendezewi na uwamuzi wa kuingia mitaani kupambana vita kama wenzetu

    tunakuomba utupe amani milele ameen.

    ReplyDelete
  9. MZEE WA BUNJUDecember 01, 2011

    wanalalamika nini mbona ndugu zao huko kijijini wanapanda punda? ndo uzalendo huo walitaka wapande VX?

    ReplyDelete
  10. Chombo cha usafiri, kwa kawaida, huweza kutumika kwa shughuli iliyokusudiwa.Nchini Tanzania tunatumia aina mbali mbali za vyombo vya usafiri. Hapa ninasisitiza, vyombo vya usafiri na lori likiwa ni mojawapo ya chombo cha usafiri. Shida yangu hapa ni uchafu unaosemekana kwamba lori lilikuwa chafu. Hii ni tabia ya dreva anayeendesha gari hili kwamba ni mchafu. Lori likitunzwa vizuri, hakuna sababu ya kutotumika kwani linatakiwa kuwa safi hata baada ya kubeba uchafu toka eneo fulani hadi mahali pengine. Uchafu wa dreva anayeliendesha ndio ulalamikiwe kwa kutoliweka lori safi. Aelimishwe anavyopaswa kuliweka safi hilo lori kwa ajili ya matumizi ya usafirishaji. Uzuri wa chombo cha usafirishaji ni kuwekwa safi muda wote baada ya kufanyishwa kazi. Lori lioshwe baada ya kusafirisha bidhaa ambazo ndio shughuli za kila siku za hilo lori. Usafi na utunzaji mahiri ndio sifa ya kukabidhiwa hilo lori na mmiliki wake. Angekuwa dreva wangu, angeshafundishwa umuhimu wa kuliweka safi hilo lori. Shughuli njema ndugu Ma-skauti wenzangu.

    ReplyDelete
  11. Ankal acha uchonganishi...mbona wanaonekana wako poa tuu!

    ReplyDelete
  12. mngembeba humo mwanangu mngenitambua. wazazi, mnawezaje kukubaliana na ushenzi wa namna hii kwa watoto wenu?

    ReplyDelete
  13. Dharau namna hii ni kawaida miaka mingi kwenye mbio za Mwenge hata wasanii hubebwa hivi na kisha kuacha hukohuko wajitegemee kurudi. Ukikataa kesi kubwa sana huko wilayani.POLENI SANA kuonekana kwa picha rasmi kutasaidia sana kubadili akili ya wajinga

    ReplyDelete
  14. mtoto wangu hawezi kuwa skauti wa bongo hata kidogo bora nimpeleke uganda !wajameni

    ReplyDelete
  15. Wametaka wenyewe kwanza akili zao hazifanyi kazi kama waliliona chafu kwanini walipanda!??

    ReplyDelete
  16. Suala la Ujasiri na Uaskari upande mmoja ,,,na suala la kupanda lori la uchafu upande wa pili.

    Kupanda lori ktk uaskari wa Skauti sio hoja ndio Uaskari wenyewe huo, hoja ni usafi na usalama wa kiafya wa chombo hicho!

    ReplyDelete
  17. Hii haikukaa sawa wadau. Kama hili roli lilikuwa chafu na linanuka halikupaswa kutumika kuwasafilisha watoto wetu wa skauti. Kwa maelezo mafupi uskauti ni kujifunza: Usafi, nidhamu, ujasili, upendo na mbinu mbali mbali za kutatua matatizo ktk maisha ya kila siku. Pia kusaidia watu wenye shida. Uskauti sio uvumilivu katika uchafu unaoonekana bayana kuwa unaweza kusababisha maradhi. Uskauti ni kugundua kuwa hapa ni pachafu na kutafuta ufumbuzi. Hebu tujaribu kufikiri hili roli la uchafu hubeba uchafu wa aina zote, ikiwa ni pamoja na vyombo vilivyo na majimaji ya mwilini (body fluid): kondom, damu, mate, kamasi, kinyesi cha binadamu, ndege na wanyama. Mizoga inayaweza kuwa imekufa kwa wadudu ambao ni hatari kwa afya ya binadamu pia.
    Kwa ajili ya tukio hili la uzembe watoto hawa wanaweza siku moja kujikuta wanamaradhi kama: kifua kikuu, HepB au C, Ukimwi, kipindupindu, Safura, Nk
    Kilicho kibaya zaidi ni pale viongozi wanaposhindwa kukumbuka kuwa hawa watoto waliopandishwa roli lenye uvundo kesho watakuwa watumishi wa serikari, na kama hiyvo ndivyo ilivyo basi na wao pia wataendelea kutoa usafiri kama waliopewa, Maana tukionyeshwa upendo nasi tutatowa matunda ya upendo, lakini tukionyeshwa ukatili basi nasi tutatoa matunda ya ukatili. Kwa maneno mengine tunatoa tulicho nacho.
    Hawa watoto hawakutandewa haki.
    Mdau
    M. Mwisho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...