Wakuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili (MUHAS) wakiingia kwa maandamano kwenye Mahafali ya Tano ya Chuo hicho kabla ya kuzuka kwa vurugu.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili (MUHAS) wakimsikiliza mwenzao kabla ya kusambalatishwa na kikosi kazi cha Jeshi la Polisi (FFU).
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS),Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mh. Ali Hassan Mwinyi (katikati) akiongozana na baadhi ya wakuu wa Chuo hicho mara baada ya kuzuka kwa vurugu za wanafunzi wa chuo hicho waliokiwa wakitaka kurudishwa kwa Serikali ya Wanafunzi ambayo ilivunjwa hapo awali.
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo hicho akiwa ametiwa mbaroni na kina Ras Makunja.


Na Francis Dande

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Kishiriki, Muhimbili (MUHAS), leo wamesababisha shughuli za Mahafali ya Tano ya Chuo hicho kusimama kwa muda baada ya kuzuka kwa fujo kubwa zilizopelekea Askari wa Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya kishindo ili kuwatawanya.

Wanafunzi hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana huku wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kurudisha serikali ya wanafunzi (MUHASSO).

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Deogratias Ntukumazina alitoa ahadi kwa wanafunzi hao ya kuirudisha Serikali ya Wanafunzi pindi watakapofuta kesi waliyofungua Mahakama Kuu kauli ambayo ilipingwa vikali na wanafunzi hao na kutishia kuvuruga shughuli za mahafali zilizokuwa zimesimama kwa muda kutokana na wanafunzi hao kufanya mkutano wao uongozi wa Chuo mbele ya Jukwaa ambalo sherehe za kuwatunuku wahitimu zingefanyika kutokana na kugoma kuondoka mahali hapo hata baada ya uongozi wa Chuo kuwataka kufanya hivyo jambo ambalo lilisababisha Jeshi la Polisi kuongeza nguvu ili kuwatawanya.

Hali ilivyokuwa mbaya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alitoa amri kwa Polisi waliokuwa wakilinda Usalama kutumia nguvu jambo ambalo lilisababisha baadhi ya wazazi waliofika katika mahafali hayo kukimbia ovyo na kuanguka na watoto na kusababisha baadhi yao kuumia kutokana na mawe yaliyokuwa yakirushwa na wanafunzi na baadhi ya viti kuvunjwa na wanafunzi hao, katika kurupushani hiyo baadhi ya wanafunzi walikamatwa na Polisi.

Katika Mahafali hayo ambayo baadaye yalifanyika chini ya ulinzi mkali baada ya polisi kuwatawanya wanafunzi hao baada ya njia ya majadiliano kushindikana kutokana na jazba za wanafunzi hao waliokuwa walikuwa wakidai serikali ya wanafunzi ilirudishwe leo.

Hata hivyo Kwa mujibu wa mmoja wa wanafunzi hao aliyetambulika kwa jina la Njechele Boniface alisema kuwa walianza kukusanyika chuoni hapo majira ya saa mbili asubuhi ili kufanya mkutano wao na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Deogratias Ntukumazina ili kuepuka kuingiliana na shughuli za mahafali hayo lakini Mwenyekiti wa Baraza la Chuo alifika chuoni hapo majira ya saa sita mchana na kusababisha kuingiliana kwa mkutano huo na shughuli za mahafali hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Nafikiri ni kosa kumwita mfanyakazi wa chombo cha dola "Ras Makunja"!!

    ReplyDelete
  2. Pongezi jeshi la polisi kwa kuheshimu haki ya wanafunzi kugoma bila kuwafanyia mizengwe. Jeshi letu linaanza kukomaa. Sasa wanaonyesha uwezo wa kudhibiti watu bila kutumia nguvu!

    ReplyDelete
  3. Hizo ni dalili za watanzania kukosa uvumilivu

    ReplyDelete
  4. Nadhani huyo mwenyekiti wa baraza aliyewaweka hao wanafunzi tangu saa mbili mpaka saa sita inabidi awadibishwe kama hakutoa taarifa ya kuchelewa kwake mapema.

    ReplyDelete
  5. miaka mitano baada ya kutoka hapo chuoni unagundua kuwa ulichokuwa unapigania hakikuwa na maaana. Serikali ya chuo ndio nini?

    ReplyDelete
  6. jamaa anaomba msamaha kwa unyoge, hajui kama jamaa hawa hawana mioyo.

    ReplyDelete
  7. Kwa wale wazalendo watoto wa kitanzania halisi walio soma chuo hicho huwezi kuwapinga vijana hao. Sema tu siku waliyo amua kuonyesha hisia zao ni siku iliyo kuwa na tukio muhimu kwa wenzao walio maliza masomo, wangelitafuta siku nyingine.

    ReplyDelete
  8. serikali ya chuo ndiyo chombo kinachowaunganisha wanafunzi wa Chuo na Utawala na ndiyo chombo kinachowatetea wanafunzi kwa karibu zaidi hasa pale madai yao ya msingi kv mikopo yanapohitajika. Tatizo ninaloliona kwa wanafunzi hao ni approach wanayotumia kudai haki hiyo hasa kwa kuzingatia mazingira hayakuwa mazuri (hata kama mwenyekiti amechelewa kuwaona). walitakiwa watafute siku nyingine wademontrate namna ambavyo mwenyekiti aliwapuuza nk. lakini kwa hivi walivyofanya inaonekana wao ndo wakorofi maana kwa vyovyote vile wasingeepuka kuleta vurugu. walikosa uvumilivu, jambo ambalo si zuri kwa watu wanaojiandaa kuwa proffessionals wa baadaye

    ReplyDelete
  9. Ilikuwa ni IMTU sasa ni zamu yetu..viongozi wa vyuo kulikoni?something is wrong somewhere.

    ReplyDelete
  10. Siasa za Jazba za kuingizana mkenge zinaponza sana,,,jamani Ka Ankal ketu hapo picha ya chini(Manafunzi wa Udaktari Muhimbili) kana jaribu kuomba msamaha lakini inaonekana wapi!

    Ahhh wapi ndio kwanza kapo chini ya Ulinzi!

    Mjomba soma kwanza Udaktari, siasa za ki Mtulinga na Manyau nyau zitakuponza itokee ukatimuliwa bure usimalize kozi!

    ReplyDelete
  11. Kweli dogo yamemkuta ,inaonekana tokea azaliwe ndio mara ya kwanza anakumbana na Polisi, picha ya chini ahhh ma siasa siasa bwana ,sometimes yana lostisha!

    ReplyDelete
  12. Mjomba wetu picha ya chini kabisa,,,familia yetu inakutuma ukasomee Udaktari Muhimbili unafika Chuoni unakubali kutumiwa na Wanasiasa bila kujua kuwa unaweza hatarisha mustakabali wako kielimu na kimaisha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...