Rais wa Bunge la Korea Mhe. Kim Jong Nam akupita kwenye gwaride la heshima kwenye Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es salaam wakati alipowasili nchini jana. Mhe. Kim Jong Nam ameambatana na ujumbe wa watu 17 akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea, kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Mhe. Kim Jong Nam, Rais wa Bunge la Korea wakiangalia vikundi vya Burudani mara baada ya kuwasili nchini. Mhe. Nam amepokelewa pia na Mhe. Selina Kombani, Waziri wa Katiba na Sheria (kulia).
Waziri Membe, akimtambulisha Rais wa Malawi Mhe. Bingu wa Mutharika, kwa viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili mjini Dar es salaam jana. Rais Mutharika amepokelewa pia na Mhe. Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Kilimo wa Tanzania. Rais Bingu wa Mutharika amefuatana na ujumbe wa watu 15 kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara hapo kesho tarehe 9.12.2011.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akimtambulisha Rais wa Msumbiji Mhe. Armando Guebuza kwa Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi Mhe. Mathayo David Mathayo mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mhe. Bernard Membe akimtambulisha Mhe. Hifikepunye Pohamba Rais wa Jamhuri ya Namibia kwa maofisa mbalimbali waliofika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kumpokea mara baada y akuwasili nchini. Rais Pohamba ameongoza na msafara wa watu 12 kushiriki kwenye sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...