Makamo wa rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Eckernforde Tanga Univesity Bw Santus Tangatya akiwasomoea wanafunzi wenzake barua ambayo wanafunzi 11 waliokosa mikopo ya bodi ya mikopo wakitakiwa kundoka chuoni hapo licha ya wanafunzi wenzao kuwachangia sehemu ya mikopo hiyo ili waendelee kubaki lakini uongozi wa chuo uling'ang'ania kutaka kuondoka.
"Tumechanga shilingi 100,000 kila mtu ili wezetu waziondoke chuoni lakini uongozi wamegoma na wameona barua hii eti wenzetu 11 waondoke, sisi kama viongozi wenu mliotuchagua tunasema hatukubali na hatutaingia darasani hadi hatma ya wenzetu hawa ambao wamewalazimisha warudie mwaka kwasababu ya kukosa mikopo, hawakubali wametumia ubabe tu," Makamo wa rais wa serikali ya chuo kikuu cha Eckernforde tanga univesity Bw. Santus Tangatya akiwaeleza wanafunzi wenzake waliokusanyika kwenye bustani za chuo hicho.
Mshauri wa wanafunzi "Dean Of Students' Bw. Zawadiel mkilindi wa kwanza kushoto akitoa maelezo ni kwanini uongozi wa chuo cha Eckernforde Tanga Univesity umewapa barua za kuwataka kurudia mwaka wanafunzi 11 kati ya 64 wa mwaka wa pili wanaochukua shahada ya elimu kufuatia kukosa mikopo kutoka bodi ya mikopo nchini, lakini hata hivyo wanafunzi hao hawakukubaliana na maelezo yake.
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Eckernforde Tanga Univesity kilichopo Jijini Tanga, wakimzonga Mshauri wa wanafunzi wa chuo hicho 'Dean Of Students' Bw Zawadiel Mkilindi kufuatia mzozo mkubwa ulioibuka chuoni hapo kuhusu kusimamishwa masomo wanafunzi 11 ambao walikosa mkopo kutoka bodi ya mikopo hivyo uongozi wa chuo kuwapa barua ya kuwataka kuondoka chuoni hapo.Picha na Mashaka Mhando,Tanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. haya maswala ya umoja na ujamaa ndo yanatufanya tusiwe na akili wala tusiendelee.

    acheni kila mtu apigane kivyake.

    kama wanafunzi hawakufaulu kwa nini wapate mikopo?

    ReplyDelete
  2. Watanzania wote tungekuwa na mioyo kama hawa wanafunzi waliojitolea kusaidia wenzao kweli tungekuwa mbali.....

    ReplyDelete
  3. jamani sasa hivi vyuo vikuu vingine du haya tutafika tu tuendako inabidi wizara husika iangalie hadhi ya vyuo kwa kweli hii ni aibu kubwa tulikimbilie tu kuanzisha vyuo vikuu eti kwa kuwa tunavihitaji

    ReplyDelete
  4. Hiyo ofisi ya dean haikukalia kichuo kikuu seuze maamuzi ya uongozi wa chuo.

    ReplyDelete
  5. Serikali irudie utaratibu wa zamani kwamba ni Div 1 na II tu ndio wapate mikopo.

    Leo hii mtu ana division III ama IV eti naye yupo chuo kikuu na anadai mkopo.

    Ajira hakuna na vyuo vikuu vinazidi kuchipua kila siku nasikia eti serikali inataka kujenga chuo kikuu kingine cha kilimo Mara eti kumuenzi Nyerere wakati graduates wa SUA karibu wote wako mitaani hawana kazi.

    ReplyDelete
  6. Idadi kubwa ya mifugo sio kigezo cha Utajiri, Umuhimu tuwe na idadi ya vyuo kulingana na uwezo wetu kuvihudumia ili kutoa kiwango bora cha Elimu!.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...