Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel Maige (kulia) akipokea Ripoti ya Tume ya Ngorongoro iliyoundwa kufuatia tuhuma zilizotolewa katika Kikao cha Bunge cha Agosti 17 2011 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Thomas B. Mihayo. Mhe Maige aliwashukuru wajumbe wa Tume hiyo kwa kufanya kazi kwa wakati na kuahidi kuwa uongozi wa Wizara utaipitia na kuyafanyia kazi mapendekezo waliyoyatoa.
Wajumbe wa Tume ya Ngorongoro, kutoka kushoto ni Jaji Mstaafu Thomas B. Mihayo (Mwenyekiti); Emmanuel P.C. Kitindi Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali Watu, Wizara ya Maliasili na Utalii.; Steven Nkonokaya Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Alois Msigwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais Utumishi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...