Ankali salaam aleykum,

Naomba uniwekee malalamiko yangu, watendaji wa tanesco watusaidie, ni hivi nina siku ya 4 nyumbani kwangu hakuna umeme mbaya zaidi umeme juu ya nyumba ambao unatoka katika wire wa umeme kuingia ndani unatoa cheche si mchezo mpaka amani imetoweka nyumbani, 

Nimetoa report tanesco tangia Jumanne ya tar 20.12.2011 cha kushangaza kila nikipiga namba 0784768584 napokelewa na mara nyingi amekuwa akinipokea Richard, lakini anaomba upya namba yangu ya simu na jina langu na hatoi reference number, Jana ambayo ni siku ya 3 tanesco hawajatokea na wakati huo nimeshapiga simu kama mara 14 kwa time tofauti, niliamua kwenda Tanesco mikocheni na nilionana na watu wa emergency, 

Nikawafahamisha tatizo langu na kuwa nimeshaongea na Richard mara nyingi sana na sina reference number, wakachukua details zangu na bado hawakunipatia reference number kw madai ya kuwa system zao zina shida lakin wakanihakikishia kuwa mafundi ndio wanaenda site na wamewapatia ramani ya nyumbani kwangu hivo niongozanenao, niliongoza nyumbani kw mategemeo ya kuwa mafundi watanipigia time yoyote lakni still hawakutokea, 

Leo hii Ijumaa nimepiga tena tanesco nimeongea na Rashid akaniambia hakuna taarifa yako yoyote hivo akachukua upya details zangu na akanipatia na reference namba, hivo sijui kama leo watatokea au laaah, Wakurugenzi na wasimamizi wa vituo tunaomba inapotokea shida mtusaidie na sio watendaji wenu wanaturusha danadana, Simu zenu za emergency kupatikana ni shida sana hivo tunaomba tunapozipata muwe mnatatua na matatizo yetu. 

Hii hali ya cheche inaweza kusababisha maafa makubwa wakati mna uwezo wa kuziwia maafa hayo mnapopata taarifa mapema, Lawama zote ziwaendee watu wa emergency wanaopokea simu maana wanapokea simu kama za nyumbani na hawaweki kumbukumbu popote na hawapeleki taarifa kw mafundi

Mdau Makumbusho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Lakini wewe nakushangaa sana kwani unakaa Nchi gani au umeingia TZ juzi. unaelewa wazi hao jamaa bila kitu kidogo hawaji. Utakesha na kiza na hata Xmaass kwako giza.

    ReplyDelete
  2. wanataka hela tu hao .....mikocheni emergency ni kiboko kwa rushwa....nafikiri wanaongoza kuliko watendaji wote wa tanesco tanzania......sema tukupe namba za wala rushwa chap chap watafika.....na kingine siku nyingine unakwenda moja kwa moja kwa meneja wao na kundi la waandishi wa habari......!

    ReplyDelete
  3. Watu wa TANESCO wanamaudhi sana. Yaliwahi kunikuta hayo kama mwezi hivi umepita. Hiyo reference number nilikuja kupewa baada ya kama wiki hivi baada ya kupiga simu sana na kila ukipiga unaulizwa wewe uko wapi na baada hata ya kupewa reference number nikaulizwa maswali yale yale. Nikawauliza nini maana ya reference number? nilipowauliza hivyo wakasema system zao ziko DOWN. Sisi watanzania customer care ni ZERO kabisa. Mtu unaweza ukaenda dukani na hela mtu akakataa kukuuzia kitu eti hana chenji. Nenda kwa wahindi uone kama utakuta huo upumbavu. Ni ujinga tunafanya, halafu tunalalamika kwanini hatuendelei.

    ReplyDelete
  4. Majibu kutoka kwenye Mamlaka baada ya Taarifa kutolewa imekuwa ni tatizo SUGU sana kwa watendaji wengi Duniani!.

    Na huu ni udhaifu hasa inapotokea taarifa kuwa ni za matukio yanayohusu maafa ambapo uharakishaji ni muhimu sana!.

    Isiwe kigezo kwa kuwa nchi husika kama ni nchi iliyoendelea au ni dunia ya tatu au la,hii inatakiwa kwa Mamlaka zote za Dunia kuanzia huko kwa wenyewe hadi huku kwetu!

    MIFANO:

    1.NORWAY,
    Mwezi wa Julai mwaka huu 2011 yalitokea mauaji ktk Kisiwa kimoja ambapo muuaji alilipua halafu akatumia bunduki kufanya mauaji ambayo ndani ya masaa mawili 2 tokea Taarifa zitolewe kwenye Mamlaka mjini Oslo mhalifu alikuwa hajakamatwa na kufikia kuua watu kiasi kama 80 hivi!

    2.MAREKANI,
    Kilitokea kimbunga cha bahari kitu kama Katrina au kile kilichotangulia miaka ya 2005, au 2006 hivi ambapo ''EMERGENCE RESPONSE'' (Yaani majibu ya dharura kusimamia maafa) kutoka Mamlaka yalichelewa kuwafikia waathirika!

    Sasa hebu angalia nchi zilizokuwa mbele kimaendeleo kama hizi zinakuwa pia na matatizo haya!, ila tusichukulie hii kuwa kama pasipoti ya uzembe ,kama nilivyotoa maoni hapo juu inatakiwa kwa Mamlaka ya nchi yeyote ile Duniani kuwa na uharaka wa kutoa majibu kunapotokea maafa au shida!

    ReplyDelete
  5. The godfatherDecember 23, 2011

    Mashirika ya uma,huduma mbovu ndio utamaduni wao.Yani hata hawajali wateja zaidi ya kudai mishahara yao kuongezwa

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli hili shirika linabidi libadilike. Mie nilitoa malalamiko yangu kwa njia ya mtandao wao. Hivi ninavyondika toka tarehe 5/12/2011 saa mbili na dk arobaini na nne asubuhi hakuna chochote kilichojibiwa. Kuna ref no unapewa kwa ajili ya kufuatilia na unapoingiza hiyo ref nbr pale penye sehemu iliyoandikwa Tanesco response hadi sasa ni "No records Found"

    Nikatuma maelezo niliyoingiza kwenye mtandao wao kwa manager wa Kinondoni South, sijajibiwa hadi leo. Inamaana hajapata au kaamua kunipotezea, Kwa kweli inauma sana!

    Bwana Misupu we mtu wetu wa habari hebu fuatilia hii imekaaje ?

    ReplyDelete
  7. Tanesco hakuna mahali wanapopapenda kama Emergency,yaani ni hela tu.mimi naona hii taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nao wanakula rushwa au hawajui nini maana ya rushwa.wamekaa kupokea mishahara tu,kazi hawajui wanangojea labda kikwete awape semina elekezi.

    ReplyDelete
  8. meneja wa mkoa wa ilala kabla ya huyu aliyepo, alilalamikiwa sana kuhusu tatizo la low power eneo la ukonga mwembe madafu kuvuka reli transforma ya mama sakina, hatimae akaelewa akaomba fungu la kutatua tatizo, akapigania akapata, akaleta nguzo kubadili zilizooza na kutengeneza mahali pa kufunga transforma ya nyongeza, akiwa katika matayarisho ya kazi hiyo akapewa uhamisho kwenda arusha, kazi haikufanyika! meneja aliyembadili ukimuuliza anakushangaa kama vile anakuuliza "nyie wa wapi? mbona hakuna kitu kama hicho?" nae anajiita engineer! sijui ni engineer gani huyu umeme unamu-engineer badala ya yeye kuu-engineer umeme!! aahh. anashindwa kumalizia kitu kidogo alichoacha mwenzake!

    ReplyDelete
  9. Tumieni namba hii ya TANESCO 022 2194400 mwaweza saidiwa. Ila pole pole tutafika.

    ReplyDelete
  10. Mie pale Tabata Kimanga kuna nguzo ya umeme kwa kulipuka hiyo, hadi nikimuelekeza mtu kwangu namwambia uliza kwenye nguzo ya umeme inayolipuka-lipuka. Hii hali ni zaidi ya miaka 10 na siku moto ukiwaka moja kwa moja basi zile nyumba za CCM, TRA na kontena la Gewe na vilivyomo ndani vitabakia historia na kutembelewa na wakuu wa nchi.

    ReplyDelete
  11. NDIO MAANA TAASISI ZOTE ZA SERIKALI ZILIFANYA MAONYESHO YA MIAKA 50 YA UHURU LAKINI TANESCO KWA KUWA WAZEMBE WALIOGOPA KUFANYA MAONYESHO

    ReplyDelete
  12. wewe hapo juu unayefananisha mifano ya sijui Norway na marekani ...Big difference ndugu yangu...Tanzaia kwishneni imedekezwa..

    Hiyo mifano ni tone la soda kwenye ndoo ya maji..Huku huduma bora saaaana..msisome tu kwenye news mkajipa moyo hata kwa wenzetu ni hivi hivyo hatuna sababu ya kulalamika...No

    Tanzania mmewazoesha wenyewe kwa kuwapa rushwa...Unaona hao hapo juu wanataka kukupa number za wala rushwa so who enable them?

    Ingekua hamna anayetoa rushwa huduma zingukua sambambamba...Lakini kwa vile bongo kila mtu anataka me first ...because I have money I can't wait na hao wala rushwa are having funny.

    Tabia ya tamaa kukata lines ndio inatupoza...Tunapenda me me me first sasa utakuta kuwa watu ambao waliharibikiwa nyuma ya huyu just becasue of them can't wait wamelipa wamefanyiwa speed service...

    Think about others when you bribe someone..Ujue rushwa unayotoa ni kuwa unapoteza nafasi ya mtu mwingine kutendewa haki....Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wahalifu

    ReplyDelete
  13. Wewe Mdau wa 12 chini Usifikiri kwa kuwa nchi ni MAREKANI au NORWAY na kwa vile wao wameendelea ndio kila kitu kinafanyika kwa muda sahihi au mambo yao yamekamilika hawana mapungufu hata kidogo!,jaribu kusoma vizuri maoni kwanza.

    MADA NI UCHELEWAJI WA HUDUMA KUFIKA KTK MAAFA NA SIO KIGEZO CHA MAENDELEO YA NCHI HUSIKA AU KUTOPATA HUDUMA KWA MUDA SAHIHI KWA VILE KUTOKUTOA RUSHWA!

    Ndio ninyi mnaofikiri kuwa kila aliyepo Marekani au Ulaya ana maisha mazuri na kuwa hakuna masikini huko!, sio hivyo kule wapo watu hata mlo mmoja kwa siku hawamudu tena wapo watu wana kaa na kulala mitaani kama huku!

    MAONI YANESEMA DUNIA NZIMA PANA UCHELEWESHWAJI WA KUTOA MAJIBU KWA SHIDA KUSHUGHULIKIWA, PINDI TAARIFA ZINAPOFIKA HUKO KWENYE MAMLAKA AU SEHEMU ZA KUTOA HUDUMA, NA HII NI HATA KAMA UMETOA RUSHWA AU HUJATOA!

    MFANO NYUMBA INAUNGUA, UMEPIGA SIMU KAMPUNI BINAFSI YA DHARURA UMEHAKIKISHA UTAWALIPA ,AU UMESHAWALIPA MNA MKATABA NAO LABDA KAMPUNI KAMA KNIGHT SUPPORT AU ULTIMATE SECURITY AMBAO WANA MAGARI ZA ZIMAMOTO, PANACHUKUA MUDA KUFIKA AU HAWATAFIKA KATIKA MUDA KAMA ILIVYOKUSUDIWA KULINGANA NA GHARAMA UNAYOTOA NA TAHADHARI ILIYOPO HIO NDIO MADA!

    ReplyDelete
  14. Tanesco Oyeeeeee

    ReplyDelete
  15. Wewe mtoa Maoni wa 12 sio kusikia tu Norway au Marekani ndio wao Huduma za Serikali zinawafikia Wananchi kwa haraka na nchi kama sisi ni hakuna au ni mpaka kwa rushwa!

    Mtoa maoni aleyeonyesha mifano ya NORWAY na MAREKANI amekupa matukio ambayo ni halisi,

    Kama unavyoona tukio la mauaji Kisiwani Norway pamoja na wao kuwa nacho kila kitu lakini imechukua masaa hadi 2 mhalifu hajakamatwa!

    Sasa je Muuaji huko Norway alitoa rushwa akafanikisha kazi yake kufikia muda huo na asikamatwe? huku nchi ikiwa na kila kitu?

    (Sasa je mbona baadae alikamatwa? na pia kwa nini asikamatwe ndani ya dakika 5 tu tokea mlipuko na tokea aanze kufyatua risasi?)

    Je kule Marekani waathirika wa Mafuriko ya Tufani la Bahari, hawakutoa rushwa mpaka huduma zikachelewa kuwafikia?
    -----------------------------------
    Kumbuka kiwango cha maendeleo ya jamii husika sio kigezo cha ufanisi ktk uwajibikaji wa mamlaka kwa umma.
    -----------------------------------

    Hapa watoa maoni walicho ongelea ni uharaka wa huduma kuwafikia wahitaji , bila kujali kiwango cha ufanisi wa jumuia au jamii kulingana na maendeleo yao au mtu ametoa rushwa au la.
    -----------------------------------

    ReplyDelete
  16. ningekuwa kiongozi nafukuza wote wapuuzi hawa wamechoka kazi..waafriak wana iq ndogo sana.saint ivuga mdu wa JF

    ReplyDelete
  17. Zaidi ya RUSHWA kuombwa kwa Mamlaka kama TANESCO ya Tanzania ili kupata huduma, kama Wadau wanavyotoa maoni kumekuwa na UCHELEWESHWAJI WA HUDUMA KUWAFIKIA WAHITAJI NA HII NI KWA DUNIA NZIMA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...