Mkurugenzi Wananchi Group,Bw. Richard Bell akizungumuza na waandishi (hawapo kwa picha) wakati wa uzinduzi wa Zuku TV jijini Dares Salaam hivi karibuni.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wananchi Group,Bw. Ali Mufuruki.
Mkurugenzi Wananchi Satellite Ltd,Bw. Mohammed Jeneby akizungumuza na wandishi (hawapo kwa picha) wakati wa uzinduzi ya Zuku TV jijini Dares Salaam.Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wananchi Group,Bw. Ali Mufuruki pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mwananchi Group,Bw. Richard Bell.
Kampuni ya Wananchi Group imezindua Zuku Pay TV itakayowezesha wateja wake kupata burudani ya televisioni. Taarifa hii ilizinduliwa wakati wa mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika hivi karibuni katika ofisi za Infotech Investment Group jijini Dar es Salaam.
Zuku TV, ni huduma ya satelaiti ya Wananchi Group ambayo inaunganisha intaneti, televisheni na VoIP.
Akizungumza na waandishi Bw. Richard Bell, Mkurugenzi Mtendaji wa Wananchi Group alisema, "Tunafurahi kuizindua Zuku TV kakika soko la Tanzania. Uzinduzi wetu wa Zuku TV unatupatia fursa kubwa kuchunguza na kukuuza sekta ya filamu za bongo duniani kwa njia ya mtandao wetu wa Zuku TV”.
Zuku TV inatoa uchaguzi mpana wa burudani kama habari, michezo, filamu, makala na muziki. Hizi ni pamoja na vipindi mbalimbali za ulaya kama vile BBC, MTV Base, Setanta Sports, MGM Movies na E na vinginezo. Hali kadhalika, Zuku imebuni vipindi mbalimbali kama vile Zuku Africa inayonyesha burudani za Afrika, makala ya Zuku Life, Zuku Sports na filamu mbali mbali. Huduma inapatikana kwa njia ya satelaiti katika Tanzania.
Zuku TV imetimiza wajibu wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo inahitaji huduma zote za matangazo ya Television kuhama kutoka analog na digital ifikapo mwaka 2012.
Hawa jamaa wanapatikana wapi?
ReplyDeleteHawa wawekezaji wanatudharau sana sisi watanzania, hii zuku tv inaanza kazi bila kuwa na website, wala namba ya simi ya customer care sasa hatujui wanaonesha channel zipi.
ReplyDelete