HABARI ZA KUAMINIKA NA KUSIKITISHA ZILIZOIFIKIA GLOBU YA JAMII ASUBUHI HII,INAELEZA KUWA MUIGIZAJI WA SIKU NYINGI WA SANAA YA MAIGIZO,MZEE FUNDI SAID MAARUFU KWA JINA LA MZEE KIPARA (PICHANI),AMEFARIKI DUNIA MAPEMA LEO ASUBUHI.
MZEE KIPARA AMBAYE ALIKUWA AKISUMBULIWA NA MARADHI KWA KIPINDI KIREFU AMEFIKWA NA MAUTI HAYO LEO MAENEO YA KIGOGO ALIKOKUWA AKIISHI.
GLOBU YA JAMII IMEPOKEA TAARIFA HIYO KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA NA INATOA POLE KWA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI WA KARIBU NA WAPENZI WOTE WA SANAA YA MAIGIZO NCHINI.
TUNAMUOMBEA KWA MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.
AMEIN.



Mzee Kipara Mungu akuweke pema peponi - Amin.
ReplyDeleteKwa kweli katika uhai wako umetufurahisha wengi katika maigizo yenu yaliyokuwa na busara sana na bila matusi wala aibu. Ilikuwa ni michezo kweli kweli na tukifurahia tangu enzi ya Radio mpaka televisheni.
Unakokwenda wasalimie akina Mzee Jongo, Bi Haambiliki, Pwagu na Pwaguzi na wengine wengi waliokwisha tangulia mbele ya haki.
Inna Lillahi wa Inna Ilahi Rajiun
ReplyDeleteRIP Mzee Kipara...Tulikumisi na tutaendela kukumisi!
ReplyDeleteM/mungu ailaze roho ya mzee wetu,mahali pema peponi na awape subira wanafamilia ktk kipindi hiki kigumu,poleni sana wafiwa.
ReplyDeleteInasikitisha sana wazee kama hawa wanaondoka duniani wakati kizazi kilichoko na kinachofanya mambo ya maigizo hakijaweza kufanya hata moja la mafunzo kwa jamii kupitia sanaa hiyo kama wazee hawa! Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya mzee Kipara mahala pema peponi.
ReplyDeleteWacha ajipumzikie mzee wa watu
ReplyDeletemichuzi wewe ni mwandishi mzuri sana wa habari sio kama globalpublisher asubuhi wametoa picha ya kipara amekufa ukiwa wazi kabisa bila ya kufunikwa baada ya kupata malalamiko ya watu wametoa huyo sio uhandishi wa habari sio vizuri kutoa picha ya mtu amekufa thanks uncle michuzi
ReplyDeleteinna lillah waina illaih ajiun kwake tumetoka na kwake tutarejea
ReplyDeletem.mungu akupe malazi mema peponi ameen
mchango wako katika kuchangamsha jamii tutaukumbuka.
Inna-Lillah_Waina -Ilaihi -Rajiun Mwenyezi Mingu amsamehe makosa yake
ReplyDeleteHawa kweli ndio walikuwa wakiijua sanaa, na sijui ni vipi tunawaenzi watu muhimu kama hawa?
ReplyDeleteWenzetu ulaya watu kama hawa huenziwa daima, jamani tufanye hivyo pia.
MUNGU ALIWEKE ROHO YAKE PEMA PEPONI, AMEN.