Mbunge wa Wawi kwa tiketi ya CUF, Hamadi Rashid Mohamed (mwenye kaundasuti) na wenzake wakitoka Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, jana, kuwasilisha kiapo cha mahakama kwa kulalamikia viongozi wa Cuf walikataa oda ya mahakama hiyo iliyozuia kufanyika kwa mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho Januari 4. Kushoto ni Shoka Khamis Juma, mmoja kati ya wanachama wanne wa Cuf walivuliwa uwanachama akiwemo na Hamadi.

MBUNGE wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake 10 sasa wameiomba Mahakama Kuu Dar es Salaam iiamuru Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi(CUF) wajieleze ni kwa nini wasitiwe hatiani kwa kukiuka amri ya mahakama hiyo.

Ukiacha wadhamini hao, Hamad Rashid na wenzake, waliomba mahakama iamuru pia wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad wajieleze kwanini wasitiwe hatiani kwa kukiuka amri hiyo.

Pia wanaiomba mahakama hiyo ibatilishe uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho wa kuwavua uanachama hapo Januari 4, 2012, kwa madai kwamba walikiuka katiba ya CUF.

Kabla ya uamuzi huo wa kuwavua uanachama, Januari 3, 2012, Hamad Rashid na wenzake waliwasilisha ombi Mahakama Kuu Dar es Salaama chini ya hati ya dharura wakiomba mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho uliokuwa ukitarajiwa kufanyika Zanziba, uzuiwe kuwajadili.

Kupitia kwa mawakili wao, kampuni ya uwakili ya GF Law Chambers Advocates walidai baraza hilo lina nia ya ama kuwasimamisha au kuwavua uanachama na kwamba uamuzi huo ungeathiri haki zao za kikatiba.

Waliendelea kudai kwamba, kuna kesi ya msingi ya madai namba 1 ya mwaka 2012 waliyoifungua mahakamani hapo wakihoji muundo wa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho na uteuzi wa wajumbe wa kamati hiyo.

Tayari Jaji Augustine Shangwa katika uamuzi wake wa Januari 4, 2012, aliamuru CUF kusitisha uamuzi wa ama kuwasimamisa au kuwavua uanachama walalamikaji hao.

Hamad Rashid jana alirejea amri hiyo ya mahakama kuu chini ya Jaji na kueleza kwamba CUF waliikaidi na badala yake kuendelea na kutekeleza azma yake ya kuwavua uanachama.

Katika hati ya kiapo cha Hamad iliyowasilishwa mahakamani hapo, alidai kwamba baada ya mahakama kutoa uamuzi huo, wakili wake akisaidina na mtumishi wa mahakama aliyemtaja kwa jina la Khatibu, waliwasilisha taarifa ya amri hiyo ya mahakama katika ofisi za chama hicho Buguruni saa 6:20 mchana.

Hata hivyo alidai kuwa Ofisa wa chama hicho aliyejulikana kwa jina la Mikidadi Nyandula alikataa kuipokea.
Alidai kwamba, baadaye saa 6:50 wakili wake alimtumia uamuzi wa mahakama hiyo kwa njia ya baruapepe na kwamba yeye Hamad Rashid aliiwasilisha nakala ya uamuzi huo wa mahakama kwa Afisa Mkuu wa mlalamikiwa saa 8.15 mchama ili aiwasilishe kwa Katibu Mkuu.

Hamad Rashid alizidi kudai katika hati hiyo kwamba, baada ya kuwasilisha uamuzi huo alitakiwa kufika mbele ya Baraza Kuu saa 8:25 na kutakiwa kujitetea na kwamba, ombi lake la muda wa kuandaa utetezi lilikataliwa.
Alisema pia aliwaarifu wajumbe wa baraza hilo kwamba mahakama kuu ilikuwa imetoa uamuzi na amri ya kulizuia kuendelea na azma yake.

“Niliwaonesha wajumbe wa baraza hilo waliokuwepo katika mkutano huo nakala ya uamuzi huo,” alisisitiza Hamad Rashid katika kiapo chake hicho.

Alifafanua kwamba hata hivyo, baraza hilo lilipuuza amri hiyo ya mahakama na kusisitiza kuwa ni lazima achague ama kujitetea mwenyewe au kutoka nje ya mkutano.

“Niliamua kutoka nje ya mkutano ili nisihusike katika kuidharau mahakama,”alifafanua Hamad Rashid.
Aliendelea kudai kwamba walalamikaji wengine nao waliitwa mbele ya baraza hilo na kila mmoja aliliambia baraza hilo kuwa hawezi kuendelea kwa kuwa kuna amri ya mahakama, ambayo inazuia kuendele na mkutano huo.

“Hivyo, kila mlalamikaji aliwaonesha wajumbe wa baraza hilo nakala ya uamuzi wa mahakama na lakini wajumbe wa baraza hilo walipuuza na kusisitiza kuwa ni lazima wajitete na walalamikaji waliamua kutoka nje ya mkutano,” alidai Rashid.

Alidai kwamba siku hiyo hiyo kabla ya uamuzi wa kuwafukuza, wakili wake aliyemtaja kwa jina moja la Panya mnamo saa 9:05 mchana, aliwasilisha nakala ya uamuzi huo wa mahakama ofisi ya makao makuu ya chama hicho Zanzibar.

Aliongeza kuwa licha ya kuwasilisha taarifa hizo kwa wakati katika ofisi za chama hicho na kwa Katibu Mkuu na katika mkutano huo wa baraza kuu, baraza hilo liliendelea na azma yake ambayo hatima yake ilikuwa ni kuwafukuza uanachama wa chama hicho.

“Hatua ya wa walalamikiwa kuendelea na mkakati wao wa kuwafukuza uanachama walalamikaji ulifanyika saa 9:55 jioni, wakati tayari kulikuwa na amri ya mahakama iliyokuwa imeshawasilishwa kwa walalamikiwa,” alizidi kudai.

Katika hati ya dharura iliyoambatanishwa kwenye maombi yao hayo, walalamikaji hao wanadai kuwa kwa kuzingatia uamuzi huo usio halali, walalamikaji wamewasilisha barua kumfukuza uanachama Rashid kwa Spika wa Bunge kwa ajili ya utekelezaji.

Wanadai kuwa ikiwa Bunge litatekeleza jukumu lake wapiga kura wa jimbo la Wawi, ambao mbunge wao ni mlalamikaji wa kwanza wanaelekea kunyimwa haki yao ya uwakilishi bungeni.

Mbali na Hamad Rashid wengine waliofukuzwa uanachama CUF ni Doyo Hassan Doyo, Shoka Khamis Juma na Juma Saanane, wote wakiwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho. (CHANZO CHA HABARI HII KUTOKA GAZETI LA MWANANCHI)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Kwani lazima uongozi?

    Heee hatari hii, umekosa uongozi wa upinzani ukajaribu wa kundi dogo ndani ya bunge umepigwa na chini.

    Sasa unatafuta kwa nguvu, pole sana Mzee lakini hata ukifanikiwa mahakamani hutakuwa na amani hata kidogo.

    ReplyDelete
  2. Komredi Rashid zimekunukia kilichobaki ukanunue mashua urudi Wawi ukavue. Hakiii!!

    ReplyDelete
  3. Ni aibu na fedheha kubwa kwa kuwa wananchi wanateseka na wanasiasa wanaleta mchezo wa kutaniana huku fedha za wananchi zikiteketea kila siku,mara mhakama,mara maandamano nk.its nonsense wananchi hawatatuliwi matatizo yao ya kimsingi.

    ReplyDelete
  4. BALAHAAUUUUUUUUU HUNA UANACHAMAA WACHEZEA MUNGU NCHANAAA,WE UNATAKA KUJARIBU BAHATI YAKO NA MAALIM? MUULIZE KOMANDOO NA MH.KARUME WOTE WALIKAA CHINI,SHAURI YAKO JIANDAE KUDHARAULIKA MAANA NAWAJUA WAZANZIBARI WATAKAVOKUFANYIA KAMA YALIYOWAKUTA SALUM MSAHABHA MAGIMBI MAPALALA NA MAREHEM DADI,

    ReplyDelete
  5. Hao ndio wanaotaka tuwape nchi, tutafika kweli? Watanzania tufunguke akili na macho hawa watakuja kutuua na jazba zao.

    ReplyDelete
  6. MLIANZA NA CHADEMA, DHAMBI YA UBAGUZI INAWATAFUNA

    ReplyDelete
  7. CUF ni chama cha Wapemba na wao hawaitambui mahakama kuu ya Tanzania.

    ReplyDelete
  8. Hawa Waarabu wachache madhalimu ndani ya CUF wakumbuke tarehe kama ya leo 12 January 1964 yaani miaka 48 iliyopita

    SWALI:kilimtokea nini Babu yao Sultani aliyewatangulia?

    JIBU:alipinduliwa!

    HAIWEZEKANI KATIBU MKUU WA CHAMA CHA SIASA AKAWA NA MADARAKA YOTE NDANI YA CHAMA,UONGOZI KTK SERIKALI YA KITAIFA YEYE,ANAPIGA KONA YEYE HALAFU ANAWAHI GOLINI KUFUNGA BAO!,KILA KAZI YEYE HADI KAZI YA UHASIBU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...