JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
ASKARI WA WANYAMAPORI AMEUWAWA NA MAJANGILI KATIKA PORI LA AKIBA LA MASWA
Wizara ya Maliasili na Utalii inasikitika kutoa taarifa kwa umma kuwa tarehe 03/01/2012 mnamo saa 6.20 usiku, askari wa Wanyamapori aitwaye Dorcas K. Rumbagi alipigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili katika Pori la Akiba la Maswa. Marehemu alifariki njiani alipokuwa akipelekwa hospitali.
Mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda Kibara - Bunda mkoani Mara ambako alizikwa tarehe 6/01/2012.
Taarifa kuhusu kitendo hicho cha mauaji ya askari wa wanyamapori ilitolewa katika Kituo cha Polisi cha Meatu na hadi sasa watuhumiwa kumi wameshakamatwa na wanaisaidia polisi.
Wizara inachukua fursa hii kuwaomba wananchi wanaoishi karibu na Pori la Akiba la Maswa, na sehemu zingine, kutoa ushirikiano ili waliohusika wote na mauaji hayo waweze kukamatwa.
Wakati huohuo Wizara imeongeza askari katika Pori la Akiba la Maswa ili kuimarisha ulinzi.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Hivi mafisadi mkisoma habari kama hii mnajisikiaje?
ReplyDeleteWanyama pori wana thamani klubwa sana nafikiri ni zaidi ya fedha katika Benki!.
ReplyDeleteAskari wa Wanyama pori pia kazi yao ni humimu sana na uhakika wa maisha yao pia ni muhimu sana!.
Kaa uzito wa hayo hapo juu siona sababu kwa nini Ulinzi usiimarishwe kwa Teknolojia ya kisasa zaidi kwa vifaa vya kisasa vya udhibiti zaidi ya kutumia bunduki za kawaida na magobore tu!
Inasikitisha sana kuona mtu anafariki kwa kulitumikia taifa katika kulinda mali zetu wakati huo huo baadhi ya viongozi wanatumia nafasi tulizowapa kututumika kuziiba mali hizo hizo. Ukifuatilia hao majangili walohusika si ajabu ukakuta wana ukaribu wa kikazi na baadhi ya watu wakubwa katika nchi.
ReplyDeleteNaipa pole familia ya askari wetu shupavu,Mungu awajalie nguvu.