Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua gwaride maalum wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo Uwanja wa Aman mjini Zanzibar .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Aman mjini humo.
 Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akipunga mkono kwa waandamanaji waliokuwa wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo Uwanja wa Aman mjini Zanzibar .
 Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Msafara wa Rais wa Zanzibar ukiingia Uwanjani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa jukwaani wakati ukipigwa wimbo maalum wa Taifa wa Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Safi sana mkuu! Mungu ibariki Z'bar, Mungu ibariki Tza!!!

    ReplyDelete
  2. Michuzi unatia AIBU, yaani badala ya kuandika BLOG ya jamii unaandika GLOBU ya jamii! Kiswahili gani hicho? Halafu eti umepewa tuzo, si uboya huo?

    ReplyDelete
  3. Zanzibar wana wimbo wao wa taifa?? makubwa haya!

    ReplyDelete
  4. Duh Eti Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la wawakilishi hehehe.

    ReplyDelete
  5. zanzibar kama nchi kamili ni haki yake kuwa na wimbo wa taifa, kama ni makubwa hayo mbona tz kuwa nao husemi?

    ambacho hutaki ni nini zanzibar kuwa nchi au kuwa na wimbo na bendera?

    ReplyDelete
  6. Kuwa na wimbo wa Taifa au Bendera si hoja cha msingi ni utekelezaji wa makubaliano ya muungano.

    Mimi kilichonitia hofu jana ni nidhamu ya majeshi yetu. Nilikuwa nafuatilia maadhimisho haya kwenye luninga na mara kadhaa mpiga picha alielekeza kamera yake kwenye kikosi kimoja cha akina dada na nilishuhudia karibu wote walikuwa wanatafuna BIG G kama sio mirungi!!. Wengine walikuwa wanaongea na kugeukageuka. Hili mimi lilinitia shaka kwani wakati huo walikuwa mguu sawa. Je huu ni utovu wa nidhamu ama ndio utandawazi?

    ReplyDelete
  7. MAPINDUZI DAIMA:!!!!!!!!!!!!

    Siku kama ya jana 12 Januari 1964 Mwarabu hataisahau milele,

    Katika dunia mambo 3 makubwa yanafedhehesha sana:

    1-Kufiwa na mtu wa karibu
    2-Kufilisika Mali
    3-Kushuka kwa Heshima mbele za watu au KUANGUKA MADARAKA!

    HILO LA 3 HAPO JUU NDILO MWARABU KTK ZANZIBAR ALIKUWA JUU AKICHAPA WATU MIJEREDI HAWEZI KUSAHAU KWA VILE ALIKUWA JUU GHAFLA AKABWAGWA CHINI!

    ReplyDelete
  8. NDUGU ZANGU SIPENDI HATA KIDOGO TABIA YA MICHUZI KUMWITA RAIS WA ZANZIBAR...RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI. LEO KANITIBUA SANA NILIPOANGALIA PICHA ZA MATUKIO YA SHREHE ZA MAPINDUZI. YAANI RAIS WA JAMHURI AKISALIMIANA NA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR????!!!!!!!! SIAMINI KAMA MICHUZI ANAKOSEA SIJUI KWANINI RAIS WA ZANZIBAR ANAMWITA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR LAKINI RAIS WA TANZANIA ANAMWITA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

    KAMA KUNA MAHALI ANANUKUU BASI AEKEWAZI, MBONA WENZAKE HAWAMWITI RAIS WETU WA ZANZIBAR HIVYO?

    KWANGU JAMBO HILI KWA MUDA MREFU NILANIUMA MNO NA KILA NIKISOMA BLOG HII NA KUONA ANARUDIARUDIA ANANINYIMA USINGIZI.
    AAAAAA!! AU HAPA KUNA MUENDELEZO WA DHARAU TOKA TANGANYIKA? HAYA. TUTAFIKA TU!!!!!

    WAKATABAHU,


    _______________________________________________
    Zanzinet mailing list
    Zanzinet@zanzinet.net
    http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net

    ReplyDelete
  9. wewe unaeshangaa kuwa zanzibar tuna wimbo wetu wa taifa umezaliwa lini? au tuseme ndi kwanza umeweza kuwa na chombo cha mawasiliano kinachokujuvya yanayotokea nje ya mtaa wako unaoishi?

    Wimbo wa taifa wa zanzibar umekuwepo miaka yote 48, na unatumika katika hafla zote za kiserikali za zanzibar, ikiwa pamoja na kila mwaka tunaposherehekea mapindzi ya januari 12,
    Sasa tatizo liko wapi? makubwa ni kuwa kuna watu tanzania kama wewe ambao hawajui lolote kuhusu Tanzania na muungano lakini wako mbele kutaka kuchambua kila jambo.

    ReplyDelete
  10. Mdau unaepinga Michuzi kumwita rais wa zanzibar kwa jina la rais wa serikali ya mapinduzi zanzibar naomba unielimishe. Ni lini serikali ya mapinduzi zanzibar imebadilishwa jina na kuitwa serikali ya zanzibar?

    Nipo nje toka kabla ya serikali ya mseto kuundwa, lakini nina barua tele rasmi kutoka serikalini na zina nembo inayosema serikali ya mapinduzi zanzibar, na ndivyo hivyo tumekuwa tukiita serikali yetu, jee ndugu yangu marekebisho hayo unayosema yameanza lini na jee ni official? Na vipi lile baraza la mapinduzi halipo tena kwa sasa?

    ReplyDelete
  11. brother Michuzi tafadhali sana usiitupe hii kwenye kapu kwani ni muhimu sana, na nafikiri ni vizuri hata kama ukiweka kama topic pekee ili watu wajadili.

    Inasikitisha sana kuwa ni juzi tu kuna mtu kachangia na kusema eti ni makosa kuita Tanzania visiwani kwa jina la zanzibar, na hata alifika kusema kuwa ni kosa kisheria kabisa.

    Leo kuna mtu hapa anashangaa kuwa serikali ya Mapinduzi zanzibar ina wimbo wake wa Taifa.

    Na mwengine anapiga kelele kuwa rais wa zanzibar asiitwe rais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar. Jambo ambalo linashangaza hasa ukizingatia kuwa serikali ya zanzibar inajulikana kama serikali ya mapinduzi ya zanzibar, sasa kwa nini rais asiitwe hivyo sijui ni kwa sababu gani.

    La muhimu brother michuzi ni kuwa kama kuna watanzania kama hawa waliojitokeza ambao wanaonyesha dhahiri hawajui mfumo wa mzima wa serikali ya Tanzania si hatari kuwa tunatakiwa kujadili katiba?

    ReplyDelete
  12. annon wa fri jan 13, 10:02:00 am 2012

    Nimeshindwa kukuelewa lawama zako. Official Tanzania inajulikana kama United repulic of Tanzania na zanzibar inajulikana kama Revolutionary Government of Zanzibar, sasa sijui kwa kiswahili utatafsiri vipi.

    Almuhimu kumbuka tu kuwa rais wa zanzibar anaendesha serikali hii inayoitwa Revolutionary Government of Zanzibar, na pia kuna baraza la Mapinduzi katika serikali hii.

    Sasa kama rais wa zanzibar si rais wa serikali ya mapinduzi kwa nini kuna baraza la mapinduzi ndani ya serikali yake? au baraza hili linafanya kazi nje ya serikali ya zanzibar?

    ReplyDelete
  13. Zanzibar si yaeleweka kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Tanzania hata FIFA wanajua hilo ndio maana hawana uanachama sasa Zanzibar iwe ni serikali ya mapinduzi au utakavyoita wewe unayekosa raha lakini iliasisiwa kutokana na Mapinduzi ya 12 Jan 1964 kasma hujui historia ya darasa la nne tu kwa hiyo kuwa na wimbo wa Taifa si hoja sana hata Mkoa wa Mwanza wanaweza kutunga wimbo wao wa kuwatambulisha kuwa wao ni wasukuma haina tatizo ila hoja ya msingi ni kuwa huyo ni Rais wa serikali ya mapinduzi na si wa Jamhuri ya Tanzania, lini Zanzibar ilikuwa Jamhuri?

    ReplyDelete
  14. Wewe Zanzinet@zanzinet.net

    Mimi ni Mdau najitahidi kujibu kama ninavyoelewa ingawa mimi sio Ankali Michuzi unayemlaumu.
    ---------------------------------
    JARIBU KUWA NA AKILI TIMAMU KABLA HUJAANDIKA MAONI::::JITAHIDI KUSOMA ELIMU YA URAIA ILI UELEWE
    ---------------------------------

    RAISI WA SERIKALI YA MAPINDUZI NA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA:

    HEBU ANGALIA MAMBO HAYA:
    1.MUUNGANO
    2.ITIFAKI

    1.MUUNGANO:
    ZANZIBAR IMEUNGANA NA TANGANYIKA IKAZALIWA TANZANIA HIVYO HAKUNA NYOKA MMOJA AKAWA NA VICHWA VIWILI LABDA AWE JINI:::HIVYO KAMA NCHI NI MOJA NA RAISI NI MMOJA( AU MAWANAMKE MMOJA HAWEZI KUWA MKE WA WAUME WAWILI KWA WAKATI MMOJA),Mmoja atakuwa labda ni mzazi mwezie au Mtalaka.

    2.ITIFAKI:
    UNGEANGALIA ITIFAKI KATIKA SHUGHULI HIYO YA SHEREHE ZA MAPINDUZI UNGEELEWA VIZURI.
    WANAPOKUWA ZANZIBAR BOSI ANAKUWA RAISI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR DR. SHEIN NDIE ALIKUWA WA MWISHO KUINGIA NA AKAWA WA KWANZA KUONDOKA, WANAPOKUWA BARA BOSI ANAKUWA JAKAYA KIWETE RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

    MAPINDUZI DAIMAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  15. Mdau wa Zanzibar Anonymous wa Fri Jan 13, 10:02:00 AM 2012

    Unayekerwa na na jina ''Raisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar'' na ''Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania''.

    La ziada ukumbuke kuwa kabla ya Muungano kujiri Mwarabu alipigwa mweleka na ndio watu walipojikomboa wakapata jina hilo halafu wakapiga pini kwa Muungano.

    Pia uelewe kuwa CCM ina alama mbili kubwa JEMBE na NYUNDO,

    Sasa Mwinyi (Mwarabu/ Dhalimu)yupo Zanzibar kila kukicha Nyundo inatokea Bara anapigwa Nyundo kichwani mwinyi huko Zanzibar!

    HIYO NDIO TASWIRA YA MAPINDUZI DAIMA UKUBALI USIKUBALI!

    ReplyDelete
  16. Zanzinet UTAKE USITAKE MAPINDUZI DAIMAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  17. MAPINDUZI yamezaa MUUNGANO Utake Usitake, pia MUUNGANO wa wazazi wawili ZANZIBAR(MAMA-jike) NA TANGANYIKA(BABA-dume) umezaa mtoto mzuri sana CCM.

    Na pia ni Lazima uelewe kuwa CCM ina Jembe na Nyundo, hivyo nyundo ya CHUMA ikishuka baada ya kuachiwa na jitu lenye musuli ya mkono (JITU LA BARA LILILOSHIBA UGALI WA DONA NA MAHARAGE) nafikiri unajua hakuna kitakacho baki, kama mtu akiweka vidole vitakuwa chapati!!!.

    wewe Zanzinet mailing list UTAKE USITAKE MAPINDUZI DAIMAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...