Bonanza la tatu la mazoezi ya viungo (Zanzibar Keep Fit Bonanza 2012)
Mazoezi yakishika kasi
Wanamichezo wakipita mbele ya mgeni rasmi
Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad akielekea katika Bonanza la tatu la mazoezi ya viungo (Bonanza 2012) lililofanyika katika Uwanja wa Amani mjini Unguja tarehe 01/12/2012.
Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad alikuwa ni mgeni rasmi katika Bonanza la tatu la mazoezi ya viungo (Bonanza 2012) lililofanyika katika Uwanja wa Amani mjini Unguja tarehe 01/12/2012.
Bonanza hilo lililofanyika kwa mafanikio makubwa ni la tatu kuandaliwa na Chama cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 1, januari Bonanza hili lilifuatiwa na wiki ya Bonanza ambapo michezo mbali mbali ilifanyika miongoni mwao ni pamoja na michezo ya Ki asili kama vile nage, na kuvuta kamba, pia kulifanyika michezo ya ki leo kama vile mpira wa miguu na mpira wa net ball.
Bonanza la 3 lilivishirikisha vilabu 30 vya mazoezi ya viungo vya hapa Zanzibar na pia lilishirikisha vilabu viwili(2) kutoka Tanzania Bara ambavyo ni Dar Jogging and Sports club naTaifa Jogging.
Lengo kuu la bonanza hili lilikuwa ni kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kujenga afya zao. Aidha bonanza hili lilitoa fursa ya kuvikutanisha vilabu vyote vya Zanzibar vinavyofanya mazoezi ili kuonana, kubalishana mawazo, kuelimishana na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimairisha afya zao kwa ujumla pamoja na kujenga uhusiano mwema na Serikali na taasisi nyengine za kijamii.
Maalim Seif alishiriki matembezi yaliyoanzia Uwanja wa Muembe kisonge, Michenzani kuptia Kwa Biziredi, Muembeladu, Mikunguni na kuishia Uwanja wa Amani pia alipokea maandamano ya vilabu hivyo na kuwahutubia wana mazoezi na wananchi kwa jumla, hatimae kukabidhi vyeti vya ushiriki kwa vilabu.
Washiriki Bonanza hilo walikuwa ni wana vilabu mbali mbali vya mazoezi wakiwemo wanawake, wanaume, vijana na watoto, Makocha wa vilabu na viongozi wao, Wabunge, wawalikishi, Mawaziri wa SMZ; Maafisa mbali mbali wa serikali, viongozi wa mikoa na wilaya, Waandishi wa habari, Wasomi na Wananchi kwa ujumla. Pia bendi ya Magereza iliongoza matembezi na kufanikisha shehehe hizo.
Mbali na kuonesha mazoezi hayo Wanamazoezi walipata fursa ya kuchangia damu ambapo Wananchi wapato 25 walichangia damu kupitia Benki ya Damu salama.
Katika hotuba yake Maalim Seif aliitaka jamii ya Wazanzibar na Wa Tanzania kwa ujumla kufanya mazoezi ilikudumisha afya zao na kuahidi kuwa serekali iko pamoja na itatoa ushirikiano kutatuwa changamoto zinazowakabili, aidha alitoa wito kwa Zabesa kuhakikisha kuwa na klabu ya mazoezi katika kila shehia, Unguja na Pemba.
Naam jiweke fit baba, maana wanataka kutingisha kiberiti hawa naona hawakujui eenhe!
ReplyDeleteMakamo ndio nini ni Makamu mwisho mtaanza kusema kaimo badala ya kaimu. Makamo ni umri na Makamu ni msaidizi ambaye pia hunaibu na kukaimu pia Duh! Kiswahili mnakiharibu nachukia kweli !!!!!!
ReplyDeleteHongereni sana, sherehe ilifana sana na ujumbe ilifika. Waandaaji tunawapa big up sana pamoja na changamoto mulizokabiliana nazo. Inshaala Mwakani liwe bora zaidi.
ReplyDeletewananchi tujiunge kufanya mazoezi ya viungo kwa faida zetu
Mdau wa mazoezi.
Mdau wa pili naungana na wewe kwa asilimia mia moja. Watanzania ni hodari sana wa kokusoa mtu akikosea kiingereza ama kuandika au kutamka maneno, lakini hamna mtu anamsaidia mtu kurekebisha kosa inapotokea mtu anavurunda maneno ya kiswahili na siku hizi mpaka kwenye magazeti makini utakuta makosa hayohayo tena ukurasa wa mbele. hovyo kabisa.
ReplyDeleteWatu wengine ni mafundi sana wa kukosoa kazi za wengine lakini wakiambiwa wao wafanye ni utumbo mtupu,Mdau wa pili amekuwa fundi sana kukosoa kiswahili, makamo/makamula kini hapo hapo anakuja na neno "HUNAIBU" nini maana yake? Jifundisheni kiswahili kwanza ndipo mukosowe.
ReplyDelete