Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA), Ahmad Kilima (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo kuhusu Mgomo wa madereva wa malori ,unaokusudiwa kufanyika tarehe 16 januari 2012,ambapoBw.Kilima alieleza kuwa kama kuna Madereva wenye matatizo na waajiri wao wafike Sumatra kwa makubaliano,Pichan kushoto ni Meneja wa masuala yaUmma,Bw.David Mziray.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hawa SUMATRA nao hovyo tu kama wababaishaji wengine maarufu kwenye huduma za nchi hii mf. no.1 TANESCO. Hawa SUMATRA ni aina ya "Kampuni zinazoanzishwa na serikali" na kuwaongezea wananchi ukali wa maisha badala ya kuupunguza kama inavyotegemewa. Kwa Mfano mimi nimewapigia SUMATRA zaidi ya mara 4 tangu mwezi wa tisa mwaka jana na 10/01/2012 na kulazimika kuchelewesha safari ili niwasaidie katika kufuatilia ulanguzi wa ticket unaofanywa na mabasi ya kwenda Mtwara DSM, hawajakuwa na msaada wowote. Mara utawasikia kesho ni jumamosi itakuwa ngumu kufuatilia mara tutatuma vijana na matokeo hayaonekani, HOVYO KABISA. Miezi michache nitakapofikia kikomo cha uvumilivu katika maeneo fulani fulani ya huduma, hawa TANESCO na SUMATRA mimi ndiko nitakapojitafutia hasara. Heri lawama kuliko fedheha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...