Mratibu wa onyesho litakalounganisha bendi tatu za jijini Dar (Mashujaa Band,Mapacha Watatu na Extra Bongo),King Dodoo (katikati) akiongea leo wakati akiitambulisha siku ya shoo hiyo itakayofanyika siku ya Ijumaa kwenye Ukumbi wa Business Park,Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kiongozi Muwakilishi wa Bendi ya Extra Bongo,Rogert Hega na Kushoto ni Kiongozi wa Bendi ya Mapacha Watatu,Khalid Chokoraa.
Kiongozi wa Bendi ya Mapacha Watatu,Khalid Chokoraa akiizunguzia shoo yao hiyo ambapo alitangaza kuwa siku hiyo ndio watamsaka pacha wao wa nne ambaye alitoweka kundini kwa kipindi kirefu na iwapo atapatikana basi jina la bendi yao litabadirika siku hiyo.Kulia ni Mratibu wa Onyesho hilo,King Dodoo na kushoto ni Kiongozi wa Madansa wa Bendi ya Extra Bongo,Super Nyamwela.
Kiongozi Muwakilishi wa Bendi ya Extra Bongo,Rogert Hega (kulia) akisisitiza jambo juu ya shoo hiyo.





Haya ndo mambo tunapenda, mnapromote muziki wetu wa asili si huu wa kuiga (fleva) na kuupachika/kuubatiza kuwa wetu. Big up King Dodoo na wadau wote wazalendo kwa kupenda na kuringia vya nyumbani.
ReplyDeletehuu mziki wanaopiga wenye mahadhi ya kicongo unakuwaje mziki wetu?
ReplyDeletemmh utapeli mtupu ,kuna watu wameishiwa hapo washachoka maisha ,lazima waingie sana kwenye mambo ya Bendi ili angalau wapate hela za kujikwamua kwa mara ya tatu katika maisha ...wana bendi muwe makini katika suala la hela kuna watu hapo wanaijua hela kuliko BENKI.
ReplyDeletewana longo longo nyingi sana....BE VERY VERY CAREFUL,MTAKUJA KULIA,