Mafundi wa ukarabati wa Barabara wakiwajibika mchana wa leo wakati wakiziba mashimo yaliyokuwa yameshamiri katika barabara ya Old Bagamoyo rodi,maeneo ya Mikocheni Chama,usoni kabisa mwa Hospitali ya TMJ.
 Sehemu ya Mashimo hayo ambayo yameanza kupigwa Virakazz leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. barabara ya zamani ya bagamoyo au ita old bagamoyo road na siyo barabara ya old bagamoyo RODI unawachanganya watu hili kosa tumelizoea wengi ndo maana utasikia BARABARA ya morogoro ROAD!

    ReplyDelete
  2. Duh, ina maana haya mashimo yamekuwepo tu kipindi chote hiki??? Yaani niliyaacha mwaka na nusu sasa ndio yanazibwa leo??? Ama kweli kiongozi wa kitanzania hastahili heshima hata kidogo.

    ReplyDelete
  3. Inaitwa "MITEGO YA PESA" na wala si mashimo kama mnavyoyaona maana yakijitokeza na nyie mkapiga kelele basi tenda nje nje,tunasiliba kiasi miezi mingine michache ikipita mwatuita tena.......... ili muradi maisha yanasonga mbele.

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza hapo hizo ni lugha za kawaida katika blog yetu ya jamii kwa hiyo usishangae kukutana na sentensi za hivyo kama "Barabara ya mandela road", "Hepi besdei ya kuzaliwa" n.k. Ni namna tu ya kufanya blog iwe ya burudani zaidi na ndo sababu mara nyingine badala ya "blog ya jamii" huwa tunasena "globu ya jamii" na haina maana kama kwamba aliyeandika amekose lahasha, ni "vijimambo tu" vya humu!

    By the way barabara zetu za mwanza zipo SHIMOZZ za kumwaga kila kona na bahati mbaya mkandarasi akitengeneza ni kwa kiwango duni na siku mbili tu(nasisitiza siku 2) shimozz zinarudi paleplale.

    Hu ni udhaifu mkubwa ukizingatia huyu ni mkandarasi mkubwa ambaye amepewa hata tenda ya kuboresha uwanja wa ndege Mwanza. Sasa najiuliza hivi hawayaoni haya kila siku mvua kidogo ndege haziwezi kutua? Na katika hali hizi kweli tutaweza kushindana na wakandarasi wa nje huku matokeo ya kazi zetu ni mabovu na huku tukiilalamikia serikali itujali kupata kazi za ujenzi kwa upendeleo. This is absurd. Waacheni tu wachina wapewe kazi mpaka siku mtakapokuwa na ustaarabu wa kujali kazi za watu. shame.............

    ReplyDelete
  5. if the anti corrupt r corrupt then there is no hope

    ReplyDelete
  6. madu wa nne tupo pamoja hiyo ilikuwa pia kuinogesha blogu yetu. mwendelezo wa misemo yetu kama vile "mdau akiwa na my wife wake" michuzi tupe vitu tupe vitu. ila msijisahau maana kuna watu hata mtaani huko kwenye mazungumzo makini pia hurudia maneno hayo hayo hususani kuhusu barabara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...