Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haji Omar Kheir (pichani) amewataka Manahodha wa vyombo mbali mbali vya Ngalawa kujiandaa zaidi ili kuweza kupata ushindi kwa kipindi cha mwaka ujao .

Hayo ameyasema leo huko Shangani,Forodha Mchanga Wilaya ya Mjini, wakati akifunga mashindano ya Resi za Ngalawa ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za sherehe za kuadhimisha miaka 48 ya Mapinduzi Zanzibar .

Alisema kuwa mashindano yeyote yale yanahitaji uvumilivu na busara kubwa hivyo ambae hakubahatika kushinda kwa Mwaka huu ajitahidi kujiandaa kwa Mwaka ujao ili aweze kuwa mshindi.

Waziri huyo alisema kuwa lengo la kuandaliwa mashindano hayo ya Ngalawa ni moja wapo ya juhudi za kuzidisha mashirikiano ya pamoja kwa Manahodha wa sehemu mbali mbali za hapa Zanzibar na kuweza kuimarisha Udungu na mshikamano .

Mhe Kheir alisema kuwa panapo ushindani lazima mmoja ashindwe hivyo alieshindwa ni lazima akubali kushindwa kwani asiekubali kushindwa huwa si mshindani .

Alisema kuwa kwa upande wake Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatarajia kujiandaa vizuri zaidi kwa Mwaka 2013 ili kuweza kufanikisha zaidi mashindano hayo ambayo hivi sasa yanaonekana kama ni utamaduni wa Mzanzibari.

Zaidi ya Ngarawa 15 zilishiriki katika mashindano hayo ambayo nahodha Simai Shinde wa Bumbwini ndiye aliyekuwa mshindi wa kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hili si suala la michezo na utamaduni?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...