Baadhi ya waumini wa Kiislam walifanya idada ya kusalia maiti ya Marehemu Mzee Said Fundi maarufu kwa jina la Mzee Kipara aliyefariki dunia jana Maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam.
Na Francis Dande
Maelfu ya wakazi wa jijini la Dar es Salaam na vitongoji vyake, leo wamejitokeza katika mazishi ya msaanii mkongwe wa sanaa ya maigizo, Fundi Said maaruku kama mzee Kipara.
Mazishi hayo yalimenyika jioni hii katika makaburi ya Kigogo jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na Waziri wa Afrika Mashariki, Mh. Samuel Sitta na viongozi wengine akiwemo mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Henry Clemens pamoja na wasanii mbalimbali.
Mzee Kipara alianza sanaa mwaka 1964 kwa kufanya kazi za mitaani kabla ya kujiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) sasa ikiitwa TBC Taifa na kukiendeleza kipaji chake alichokuwa amejaaliwa na Mungu ambapo aliweza kuonyesha umahiri katika uigizaji ambao ulimpatia umaarufu mkubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Akiwa RTD Mzee Kipara aliigiza katika michezo mingi na kipengele kilichompatia umaarufu zaidi ni ule uigizaji wake wa kujifanya mbabe na mkorofi na kujikuta akijizolea mashabiki lukuki hasa ukizingatia wakati huo Tanzania ilikuwa na kituo kimoja cha redio na mamilioni ya wanachi walikuwa wakiitegemea kwa ajili ya kupata habari mbalimbali na burudani ikiwemo michezo mbalimbali ya uigizaji iliyokuwa ikirushwa wakati huo.
Baadhi ya Wasafii na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kumzika Mzee Kipara wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Mzee Kipara wakati wa kuelekea Makaburi ya Kigogo Jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Sehemu ya Umati uliojitokeza kwa wingi kumzika Mzee Kipara ukielekea yalipo Makaburi ya Kigogo jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Mpiga Picha wa Globu ya Jamii,Francis Dande akiwa na Muigizaji wa Sanaa ya Maigizo wa siku nyingi,Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small walipokutana kwenye maziko ya Marehemu Mzee Kipara kwenye Makaburi ya Kigogo jijini Dar es Salaam leo.


MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMIN.KATIKA JENEZA LA MZEE KIPARA MANENO YASOMEKAYO ,LAAILAAHA ILLALLAH MUHAMMADUN RRASUULYLLAH.YAMEKAA CHINI JUU WAKATI MWINGINE KIONGOZI AWE MAKINI YASOMEKE SAWA HUO NI UJUMBE MAKINI.
ReplyDeleteS.KAWAWA UK.
Mpiga picha wa ''Globu'' ya jamii! hahahaha kwisha habari yako Michu.
ReplyDeleteMpiga picha wa ''Globu'' ya jamii! hahahaha kwisha habari yako Michu.
ReplyDeleteMbele yake nyuma yetu, leo watu wengi wamejitokeza kwenda kumzika, lakini alipokuwa mgonjwa anahitaji msaada wa watu ili atibiwe ni wachache tu walijitokeza. Tujifunze kupendana hata tukiwa hai sio kupendana tukiwa maiti! Innalillah Wainaillaihi Rajiun!
ReplyDeleteinnallillah wahinalillah lajiun
ReplyDeleteWingi huu ungejitokeza wakati anaumwa na hakika angepata matibabu stahiki
ReplyDeleteMwe Serikali haikuona hata umuhimu wa kumsafirisha kwenda kutibiwa India.Nasijui kama hata kiongozi mmoja wa serikaliwalimtembelea wakati yuko mmoja.Mtu akifa ndio watu wengi wanajitokeza na kutoa usifu wake."@%%%%¤ Huu unafiki uwishe mara moja.RIP Mzee Kipara.Nausikute ametumika sana kwenye propaganda za siasa-When they use you live big today, tomorrow you buried in a casket.
ReplyDeleteMtoto wa Kabwela
Sweden
Hongera Mdau Thu Jan 12, 07:05:00 PM 2012. Mimi naona nyota wewe unaweza kusoma ama kweli twazidiana hapa dunia.
ReplyDeleteRIP Mzee Kipara, ninalojifunza kutoka kwa wadau ni kuwa mtu mwenyewe pia ajiangalie akiwa mzima yaani aweke akiba kwa ajili ya fainali uzeeni. Ukiwa mzima una marafiki mwengi lakini ukiishiwa wanakukimbia. Kuna mtu aliwahi niambia kwa kiingereza kuwa " Together we stand alone you defend" Hivyo tujue kuwa kuna wakati wewe mwenyewe utatakiwa kijitetea peke yako
Naungana na wadau wa Thu Jan 12,09:09:00pm 2012 na anaemfuatia umati huu ungesaidia kipindi kile anaumwa angeishi maisha marefu leo tusingekuwa tunamzika, tukumbuke kusaidiana wakati wa dhiki na maradhi ili tupate thawabu kwa Mungu na sio kukaa kuchangia maharusi tu.
ReplyDeleteMdau Thu Jan 12, 09:01:00 PM 2012 umesema kweli tupu. Sina cha kuongeza.
ReplyDeleteNaungana na wadau kadhaa hapo juu. Hili ni tatizo kubwa sana miongoni mwetu Watanzania. Tunasikia kwenye vyombo vya habari kila siku kuwa mtu fulani aliyekuwa maarufu siku za nyuma (hasa wasanii na wanamichezo) yuko hoi kitandani na anahitaji msaada lakini hakuna anayejali. Lakini tukisikia amekufa tu, tunavaa vizuri sana na kujipulizia marashi na kwenda msibani au kwenye mazishi. Hili si jambo baya, lakini tukumbuke kusaidiana wakati bado tupo hai. Marehemu Mzee Kipara aliugua muda mrefu, lakini ni watu wachache waliokuwa wakimsaidia hadi alipofariki.
ReplyDeleteMzee kipara alikuwa mwalimu mkuu wa wasanii wengi wanaosifika katika tasnia ya filamu na sanaa ya maigizo hivi sasa. Familia yake itaniunga mkono kuwa ni watu wachache sana walikuwa wakimtembelea kipindi hiki kirefu alipokuwa anaumwa achilia mbali wale waliompa msaada wa hal;i na mali. Unafiki mbaya!!!!!!
ReplyDelete