Blog mpya habari za kitaifa,kimataifa,michezo na burudani ikiwa imesheheni picha na matukio mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania na duniani kwa Ujumbe. Kuwa mmoja wa watembeleaji wa Blog hii mpya inayomilikiwa na mtangazaji mahiri wa habari Marygoreth Richard.Ingia humu kufahamu mengi na mazuri zaidi..

LINK:http://marygorethrichard.blogspot.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Namtakia dada Marygoreth mafanikio katika kuendesha blog yake. Napenda kumtahadharisha kuwa kuendesha blog si kazi rahisi kwa hiyo ajizatiti. Watu kama akina Michuzi na Mjengwa wamefanikiwa kutokana na kuwa 'consistent' tangu walipoanzisha blog zao. Pamoja na kuwa mwanzo ni mgumu, hawa jamaa walikomaa na sasa wanakula matunda ya jasho lao. Kuna blog nyingi tu za Kibongo zilizoanzishwa kwa mbwembwe lakini zimekufa kifo cha mende. Nyingine zinasuasua vibaya sana na ni kama zimekufa. Mfano mzuri ni blog ya Kitime (wanamuzikiwatanzania). Mimi nilikuwa ni shabiki mkubwa wa blog hii lakini nimekatishwa tamaa na mwenendo wake katika miezi ya karibuni. Yaani sasa imekuwa ni bango la matangazo ya vifo vya wanamuziki na wasanii wengine. Ukiona post mpya (hii ni wastani wa post moja kila baada ya miezi miweili) basi ujue itakuwa inatangaza kifo cha mwanamuziki. Mtu unapoanzisha blog, basi uendeshaji wa blog hiyo unapaswa kuwa ni sehemu ya maisha yako ya kila siku. Ukijifanya uko ‘bize’ na mambo mengine basi wewe huwezi kuendesha blog. Watu kama Michuzi na Mjengwa inafaa waandae semina kwa ma-blogger chipukizi ili wasirudie makosa yaliyofanywa na wengine.

    ReplyDelete
  2. wewe fanya lako acha kiherehere cha kufundisha wenzako, sio kila kitu mtu anachoanzisha kinafanikiwa kama unaona hufanikiwi kwenye blogging you try else where. mdomo mdomo tuuu na kutaja majina ya watu hovyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...