Na MERY AYO,arusha

Serikali imeadhimia kuboresha na kuanzisha mfumo wa usimamizi wa fedha za umma na kutekeleza mipango iliyojiwekea kikamilifu ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho makubwa kupitia mfumo wa fedha (IMFS) ili kupunguza changamoto zilizojitokeza kwa miaka kumi ya utekelezaji wa mfumo wa epicor kwenye baadhi Halmashauri zake.

Akiongea katika ufunguzi wa mafunzo ya Epicor 9.O5 kwa wakuu wa idara na wasimamizi wa miradi wa halmashauri katibu tawala mkoa wa arusha Eveline Itanisa alisema kuwa mafunzo hayo ya mfumo wa fedha yataweza kuboresha hali ya utendaji katika halmashauri hasa kwenye upande wa usimamizi wa fedha za umma.

Alieleza kuwa mfumo huo ulioboreshwa wa Epicor 9.05 unaunganisha halmashauri zote nchini katika kompyuta kuu ambapo utazingatia na kwenda sambamba na maamuzi ya serikali ya kupunguza idadi ya akaunti za Halmashauri na kufikia akaunti sita (6) tu.

Aidha aliongeza kuwa mfumo huo mpya utaweza kuthibiti matumizi ya fedha na kufuatilia kinachoendelea kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na kupata taarifa muhimu kuhusu maeneo yao toka kwenye mfumo huo muda wowote.

Naye mwezeshaji wa kitaifa kutoka ofisi ya waziri mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI) bw,Jeeremia Ezekiel Mtawa amesema kuwa lengo hasa la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakuu wa idara na wasimamizi wa miradi kusimamia fedha zao katika mfumo huo mpya.

Mtawa alisema kuwa mfumo uliokuwa ukitumika awali ulikuwa hautoi taarifa kwa wakati na wakati mwingine taarifa hizo zilikuwa sahihi lakini hazifanani.

Aidha aliwataka wahusika wakuu wa ambao ni wakuu wa idara kuwa makini katika mfumo kwa kuhakikisha kuwa wanasimamia fedha z a umma kwa kuzingatia kanuni na taratibu za mfumo huu ili serikali iweze kutimiza lengo lake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MIKAUSHO MIKALIJanuary 11, 2012

    Huu ni ulaji tu.Epicor ni system nzuri kabisa watu wakifunzwa vizuri na support iko hapa Tanzania.Wanachotaka ni kuleta kampuni nyingine ili waanze kuinstall nchi nzima,ku train nchi nzima watendaji na ma system administrators.Hivi ni Shs ngapi zitatumika ???watu hawana uchungu kabisa na nchi yao.TUKATAE TUSIKATAE NCHI HII INA HITAJI RAIS DIKTETA VINGINEVYO HATUTAFIKA POPOTE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...