Mdau hebu nipe maneno ya hii taswira...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. ukisikia mkao wa kula ndio huu

    ReplyDelete
  2. Umaskini kitu kibaya sana. Umaskini wa maisha unasababisha umaskini wa akili vilevile kichwani.

    ReplyDelete
  3. ...Unatafuta ugomvi weye. Ngoja waje wanaosukutua kwa maji ya betri. Teh teh teh

    ReplyDelete
  4. Hapo jamaa wanawaza..."hawa wenyeji wetu wanaleta utani!! Yaani wameleta sinia moja tu??"

    ReplyDelete
  5. HAPA TUSUBIRI KWANZA WAMALIZE KUGAWA ILI TUONE SINIA MOJA WATU WANGAPI NDIO TUANZE KULA

    ReplyDelete
  6. HAPA WATU WANAOSEVU HUO UBWABWA NAONA WANALETA GIZA. WACHANGAMKE! MEKU

    ReplyDelete
  7. 1.Da sijui nianze?
    2.Ah hawa wanatusanif nini?
    3.La mbona sahani iko mbali?
    4 Sijui nihame?
    5.Yaani nyama moja tu?
    6.Ubaguzi huu yaani wazee tu?
    7.Niko karibu la!! leo nna ngekewa kweli.
    8.Njaaaaa!!
    Hapo maswali kibao bila majibu,

    ReplyDelete
  8. Unanikumbusha mbali! hapa ni kwamba hao wazee waliokaribu na hiyo sahani hawali pilau! sasa kwa bahati mbaya wali mweupe ambao hupikwa na wanawake umekuwa tayari mapema na umetangulia ukumbini!hao wengine wanasubiria pilau iletwe! na hao hawataanza kula mpaka wapewe ruhusa na aliyepewa dhamana na ukumbi!wakati huo vyakula vyote vimefika na watu wanaanza kula kwa pamoja!

    ReplyDelete
  9. du saani moja watu wote sie.??
    ikiwa tayari tu narukia nyama.
    hapa hata sisubiri kuosha mkono

    ReplyDelete
  10. Hiyo ni wali maji mzee, maalum kwa watu maalum, ambao wakila pilau inawakaba. Hii ndiyo 'socialisation' ya siye watu wa uswahilini. haihusiani moja kwa moja na umaskini. Mimi hata leo nikiwa bongo nikakuta shughuli lazima nishughulike.

    Mdau HK

    ReplyDelete
  11. Wakubwa kwanza, watoto baadae

    ReplyDelete
  12. Aaah wali mweupe kwa mashehe

    ReplyDelete
  13. shida yako tuseme kuna babu ana "BUSHA", wa tano walioegemea ukuta.

    ReplyDelete
  14. MIchuzi, tafadhali weka kitufe cha "like"

    ReplyDelete
  15. Acha kelele wewe anon wa pili. Hiyo ni shughuli na watu wanasubiri kupata pilau. Huo ni utamaduni wa watu wa pwani na waislamu wa Afrika Mashariki. Kwa taarifa yako na kama kumbukumbu siku za mbele hata Queen wenu wa UK akija atawekwa kama hao hapo. Wazee mwanzo hehehehe!!!

    ReplyDelete
  16. huo ndio ubeche ! hapo wanasubiri wali mweupe ! Kweli umasikini unaleta mambo ya aibu wkt mwingine lkn fahamu kuwa hao wanasubiri kwa hamu ubeche wa shuguli lkn vilevile wako ambao husubiri pia kwa hamu beer za sherehe !

    ReplyDelete
  17. Kwa tathmini ya haraka haraka. Hadi picha hii inapigwa ambapo imechukua sehemu tu ya idadi ya watu kama 30, ni sinia moja tu la shaba ndo limetua. Na kwa kuondoa lawama, jamaa kashusha mzigo walipokaa wazee, ma bwa'mdogo wamechanganyikiwa.

    Picha inaonyesha jinsi watu walivyo na shauku ya ubwabwa lakini nyuso zao zina dalili ya kukata tamaa maana kama tatizo sio idadi ndogo ya wahudumu au upungufu wa masinia, basi ubwabwa ulikuwa mdogo na watu walikuwa nyomi.

    Hii ni wazi kwamba hadi leo watu wanaponea kupata riziki kwenye shughuli kama hizi. Hali hii ni mbaya na inatokana na ugumu wa maisha. Inasikitisha sana.

    Raha ya shaba ni mkao wa duara, sinia moja watu 3 au 4, maji ya kunywa pembeni ikitokea umekabwa.

    Mdau wa Kigambonino

    ReplyDelete
  18. HII STYLE INAITWA PUNJA MKONO WAKO.... MWENYE MKONO MKUBWA NDIO ANAKULA KINGI

    ReplyDelete
  19. safu ya maustadh hiyo,, wanasubiri wali mweupe

    ReplyDelete
  20. UMASIKINI NI KITU KIBAYA SANA EMBU CHEKI HAPO INA MAANA WATU WOTE HAO WANASUBIRI KULA KWA MIKONO NA KUBADILISHANA MARADHI NA WOTE HAPO WANAONEKANA KANA KWAMBA NI WAGONJWA HAWANA AFYA KABISA . HIO TABIA LAZIME IBADILIKE KWA SABABU MLIPUKO WA KUAMBUKIZANA MARADHI NI MKUBWA SANA CHAKULA GANI HICHO HATA VITAMIN HAKINA HAKUNA SALAD, JUICE, MATUNDA BAADA YA HAPO WANAPEWA KUNYWA MAJI YA BOMBANI AMBAYO NA HAYO HAYANA USTADI WA AFYA KABISA, YOTE HIO NI UKOSEFU WA KUWA NA ELIMU ! UISLAM BAANA! WEE ACHA TU.
    MDAU MBAGALA ZAKIEM

    ReplyDelete
  21. Sinia ya kwanza imeanzia "meza kuu", nyingine zitafuata, na zinatokea upande wa kulia.Huu sio umasikini ni utamaduni wetu hasa tunapokua na shughuli maalum.

    ReplyDelete
  22. Halafu sinia lenyewe limekaa kwa wazee peke yake,hawakuangaliwa watoto wadogo....

    ReplyDelete
  23. hapa ninachokiona mimi au maoni yangu sahani imeanza kuwekwa kwa wazee.

    ReplyDelete
  24. Aghhh MIKONO INAKAUKA HAWA WAANDAZI WAPO SLOW SANA Aghhh

    ReplyDelete
  25. HAYA WATU SABA SABA.

    ReplyDelete
  26. Hii nchi ina kazi kweli kweli!..Hivi kuna watu mpaka leo wanamini kula pamoja na kwa mikono kuna sababisha kuambukizana maradhi?..sijui nani alifanya hii risech?..kama ni hivyo, Tza hii kungekua na watu tena kweli? wakati kila siku idadi wanaongezeka!

    Kumbe ndio maana watu wanajazana universities lakini nchi haiendi, wasomo wenyewe ndio hao wanajaji vitu kwa hisia? badala ya ukweli.

    ReplyDelete
  27. Hiyo sinia iliyowekwa hapo nadhani ni kwa ajili ya "Display" na itaondolewa kikija chakula halisi na hatakiwi mtu aweke mkono wake kwani mlo rasmi utafuatia baadae kidogo kwa hiyo si vibaya kwa watu kuangalia na kukodolea macho ila hutakiwi kuchangamkia kwenye sinia hiyo.

    ReplyDelete
  28. nyie wote hamjui taratibu za shughuli kama hizo, hapo kinachosubiriwa chakula chote kigawiwe then watu waombe duwa kisha waanze kula. Haiingiliani na umasikini kabisa na mkumbuke hiyo ni shughuli yaweza kuwa harusi,kisomo,arobaini au mwali kutoka mkoleni.

    ReplyDelete
  29. Hapa kwa mtaji wa sinia moja watu wote hawa ,,,kipenga pyee unakuta ndani ya dk 1 sinia jeupeeee!

    ReplyDelete
  30. Mtindo wa ulaji katika Ubwabwa huu hauna tofauti na Mpira wa kona unavyo gombaniwa unapopigwa Golini!

    ReplyDelete
  31. Hapa babake usione Vizee hivyo,,,lohh katika ubwabwa vinakuwa na nguvu kweli kweli,,,mpunga mchezo?

    Kupiga tonge hapo inabidi ujipange,uwe jasiri na uwe na uso wa Mbuzi kwelikweli!

    ReplyDelete
  32. Miundo mbinu hapo, tonge la kwanza unaanzia kwenye nyama kwanza, halafu tonge la pili chenga la tatu kiazi na kachumbari kachumbari, tonge la nne chenga lala salama,,,ubwabwa unakaribia kwisha au umekwisha!

    ReplyDelete
  33. Kwenye ubwabwa wa sherehe hakuna kuheshimiana kwa minajili ya umri!

    Hivi sinia moja watu wote hawa asalaleee babake unaweza ukaishia kunawa na usile kabisaa!.

    Hapo pyeee, unakunja bonge la gumi unapiga katikati ya sinia puuu!,,,wazee wanatoa mikono yao, unafunua kiganja cha mkono, unakomba fuba la ubwabwa mchanganyiko na nyama tonge moja KUBWA MOJA unakuwa umesha fikia lengo,mchezo umekwisha!

    KOSA LA WAANDAAJI WA SHUGHULI, KUWANAWISHA MIKONO WATU HALAFU KULETA UWANJANI WALI SINIA MOJA TU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...