Familia ya Dkt. Fanuel Maro wa Upanga/Kariakoo jijini Dar es Salaam,inasikitika kutangaza Kifo cha Baba yao Mpendwa Dkt. Fanuel Maro (pichani) kilichotokea jana jioni (tarehe 7/1/2012) katika Hospitali ya Regency iliopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Utaratibu wa Kutoa Mwili wa Marehemu hospitali hapo na Kupelekwa Nyumbani kwa Marehemu Upanga Mtaa wa Longido zinafanywa hivi sasa.

Ibada ya Kuaga Mwili itafanyika katika Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam siku ya jumanne (tarehe 10/1/2012) na baada ya kufanyika kwa ibada hiyo Mwili ya Marehemu utasafirishwa kuelekea Old Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa Mazishi ambayo yatafanyika siku ya Jumatano (tahere 11/1/2012).

Mungu aiweke Roho ya Marehemu Dkt. Fanuel Maro mahala pema peponi

-Amein.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Poleni wafiwa. Huyu ni babayake mzazi Balozi wetu nchini zambia? Mhe. grace Mujuma?

    ReplyDelete
  2. RIP Dr. Maro, ninatoa pole kwa familia yote ya Dr. Maro. Mungu aifariji familia ya marehemu.
    Jirani Upanga.

    ReplyDelete
  3. RIP Dr Maro, Pole kwa wote mliofiwa Dada Grace na wote. Poleni na kazi kubwa mliyofanya kumtunza mgonjwa. Mama Maro I hope you find peace and acceptance....

    ReplyDelete
  4. Dr. Peter pole sana na kufiwa na mpendwa Baba yeti.
    Apumzike kwa Amani. Dr. Ngirwa

    ReplyDelete
  5. Poleni sana wapendwa wetu. Babu yetu umeondoka kwenda mbinguni kwa aliyetuumba. Tutakukumbuka sana kwa huduma zako bora, utumishi uliotukuka na utu uliokuwa nao. Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema. Amina.

    ReplyDelete
  6. Poleni sana familia ya Maros, Tarimos na ndugu na jamaa wote waliopo Old Moshi Tella na sehemu nyingine mbali mbali. Mungu awape faraja kwa wakati huu mgumu. Ameni

    ReplyDelete
  7. Pole Maureen and the entire Maro family.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...