Mwanasoka nyota wa zamani wa timu ya Taifa, Kitwana Manara, amefiwa na mama yake mzazi, Bi. Mishi Mikessy (pichani) jana usiku jijini Dar es Salaam.

Kitwana amesema mjini Dar es Salaam leo kuwa, mama yake huyo, anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 95, alifariki dunia baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.

Kwa mujibu wa Kitwana, mazishi ya Bi Mishi yanatarajiwa kufanyika kesho katika makaburi ya Waanglikana yaliyopo Buguruni-Malapa, jijini Dar es Salaam.

Marehemu Bi. Mishi ameacha watoto watano na wajukuu kadhaa.
Kitwana ni kaka wa wanasoka wengine nyota wa zamani nchini, Sunday Manara na Kassim Manara.

Mkongwe huyo wa soka nchini, aliyezichezea klabu za Yanga, Pan African na Taifa Stars, anaomba taarifa hizi ziwafikie ndugu na jamaa popote walipo duniani.

Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mahala pema Peponi.

-Amin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Inalilah waina ilaihi. Pole sana ndugu Qasim Manala wa Ubelgiji Mnyezi Mungu akupe subira kipindi hiki kigumu! I still remember when u show us the video of u're mom!is too bad that u were unable to see her.Qweman.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...