Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron wakati wa mkutano wao uliofanyika jana jioni mjini Davos,Uswisi.

Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron ametoa pongezi hizo kwa Rais Kikwete wakati wa mazungumzo yao jana jioni hapa Davos ambapo wote wawili wanahudhuria mkutano wa Kiuchumi Duniani wa kila mwaka, maarufu kama World Economic Forum (WEF), ambapo masuala ya uchumi, athari mbalimbali zinazokabili uchumi duniani kwa sasa na jitihada mbalimbali zinazofanywa kunusuru uchumi huo na njia za kuleta mabadiliko chanya ya kukuza uchumi barani Afrika yanajadiliwa.

“Afrika inapitia kipindi cha mabadiliko ambayo ni chanya, na Tanzania ni mfano bora wa kuigwa katika hili”. Bw. Cameron amemueleza Rais Kikwete.

Katika mazungumzo yao Rais Kikwete amemueleza Bw. Cameron kuwa kilimo ni sekta kubwa na inayotegemewa na Watanzania wengi na kwamba serikali inalenga katika kukuza kilimo kwa ajili ya kujitosheleza kwa chakula ndani na nje ya nchi.

Rais Kikwete na Bw. Cameron pia wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu siasa na usalama barani Afrika.

Mapema jana asubuhi, Rais Kikwete amejumuika na viongozi wengine kutoka Ethiopia, Guinea-Conackry, Kenya na Afrika Kusini kuzungumzia mabadiliko mbalimbali ya uchumi na maendeleo barani Afrika.

Katika mjadala huo uliongozwa na Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza Bw. Gordon Brown, Rais Kikwete amesema pamoja na mabadiliko hayo, bara la Afrika nalo ni sehemu ya Dunia Uchumi, hivyo nayo kupata athari mbalimbali zinazotokana na mabadiliko hayo ya Kiuchumi duniani.

Rais amesema pamoja na athari na mabadiliko ya Kiuchumi duniani, bado Afrika ina mahitaji zaidi katika kutekeleza sera zinazolenga katika uchumi imara na kuwekeza zaidi katika sekta za elimu, utafiti, kilimo, viwanda na miundombinu.

Rais Kikwete pia amefanya mazungumzo na viongozi na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo Bw. Bill Gates, pamoja na viongozi wa Ethiopia na Kenya ambapo wamezungumzia namna ambayo Bw. Gates atatoa mchango wake zaidi katika masuala ya kilimo na utafiti.

Rais Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Mama Sadako Ogata Rais wa Shirika la Misaada la Japan, maarufu kama Japan International Cooperation Agency (JICA) ambaye naye ameelezea kuwa JICA itaendelea kutoa misaada mbalimbali kwa Tanzania pamoja na kwamba yeye amefikia kipindi chakustaafu.

Rais Kikwete pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodafone, Bw. Vittorio Colao ambaye ameonesha nia ya kusaidia Tanzania katika kutoa na kusambaza elimu kwa kutumia simu za mkononi katika masuala mbalimbali ya afya, kilimo na elimu.

Mwisho.
Imetolewa na Premiere Kibanga,
Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais,
Davos-Switzerland.
27 Januari, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Misaada.....misaada..misaada everywhere...Miaka 50 ya uhuru.Inabidi tufanye kazi kweli Watanzania kama mchangiaji mmoja alivyowahi kusema humu kwenye blog hii

    David V

    ReplyDelete
  2. Serikali ya Tanzania inatakiwa kuwatumia watu waliokaa nje diaspora vizuri kwa kuwa ambia wandike michanganuo ya miradi ya kilimo na biashara ili weweze kupewa mitaji ya kurudi nyumbani na kufungua biashara au mashamba makubwa, masoko kwa africa yapo mengi kuna nchi nyingi zinaitaji chakula cha kununua.
    Au njia nyingine ni kuanzisha vitengo kwenye balozi na kuajili watanzania ambao wamesoma kwenye ile nchi na wamekaa sio chini ya miaka mitano kwa ajili ya kuishauri pamoja na kuandika miradi ya maendeleo kwa ajili ya Tanzania. Maana mtu ambaye amekaa zaidi ya miaka mitano ulaya amekwisha elewa jinsi mfumo mzima wa maendeleo ya nchi aliopo jinsi wanvyofanya huo ndio mfumo ambao Japan na South Korea waliutumia baada ya vita kuu ya pili ya dunia sio kuomba wawekezaji waje wjenge viwanda au mashamba wakitaka waje kama watu wanaotaka kuingia ubia na watanzania wawekezaji hapo ndio tutaona maendeleo.
    Mtu ambaye ni mwelevu na amekaa ndani ya ulaya zaidi ya miaka mitano na amekaa mtaani sio kwenye kampasi ya chuo anajua mfumo mzima wa maisha na jinsi gani mabepari wanatengeneza pesa. Tuache siasa za mambo ya chama tujadili jinsi ya kutengeneza pesa na mfumo mzuri wa kodi kwa serikali ili mapato yaongezekena kila Mtanzania afaidike.

    ReplyDelete
  3. Humu ndimo tunamotiwa mitegoni ili tupitishe sheria za ukamiruni. Chondechonde Mhs wetu.

    ReplyDelete
  4. kuwa muangalifu mheshimiwa huyo jamaa asije kukushawishi tujiunge kwenye ule mchezo wa kaumu ruti kuoana midevu kwa midevu maana wao wamezoea na sisi kwetu tunapenda kuwekeza watoto na sio kupandana majogoo kwa majogoo.

    ReplyDelete
  5. Huyo jamaa asikueleze kitu, asije akarudia Mashariti yake ya Misaada!

    Mweleze tulishakataa na HATUKUBALI!

    ReplyDelete
  6. Kiongozi wetu, tunaamini Msimamo wetu ni uleule,,,hakikisha huyo jamaa mnajadili masuala muhimu ya Faida kwetu tena yanayokubalika kwa sisi wa Tanzania, asije akabadili Mada kimtindo akaanza mipango yake ya UBASHA!

    ReplyDelete
  7. Shida tunayo hatukatai, lakini hatuwezi kujirahisi hivyo kwa Mashariti ya ajabu kwa kupata misaada!

    Wacha tuuze majoka yetu misituni, vyura wetu mabwawani , michanga ya madini na vinginevyo ili tuweze kujitegemea!

    Ni bora turudi nyuma na kugeuka jiwe ,turudi ktk ''SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA'' badala ya kuumbuliwa na Mwingereza!

    ReplyDelete
  8. JK tafadhali, kuwa makini nae huyo jamaa Mkameroni mwenendo wake sio mzuri!

    Unajua mtu akishakuwa MENDE anakuwa hakati tamaa, anaweza akaja kivingine, ni kama Fisi anayeambatana na mtu akivizia labda Mkono utadondoka!!!, ingawa tulikwisha kataa anaweza akaja na mbinu nyingine ili ajaribu bahati yake tena!

    ReplyDelete
  9. This guy anapenda picha jamani anyway, hata kamera inampenda pia maana anapendezaga kwelikweli ila problem ye ndo mshika uskania wa hii nchi something that over the past 6 yrs he still sucks....ni mawazo yangu tu!

    PS:i hope sijakosea hiyo spelling hapo mwaweza nirekebisha sina ufasaha na lugha kiviiiile na sijivunii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...