Mshambuliaji wa Twiga Stars, Asha Rashid ‘Mwalala’ akimtoka beki wa Namibia, Lovisa Mulunga.
Mashabiki ...
Mshambuliaji wa Twiga Stars, Mwanahamisi Omari akiruka daruga la beki wa Namibia, Esther Amukwaya.
Wachezaji wa Twiga Stars kutoka kushoto ni, Mwanahamisi Omari, Etoe Mlenzi na Pulkaria Charaji wakishangilia ushindi wa timu yao.
Kikosi cha timu ya taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na timu ya Namibia wa kufuzu Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake (AWC) uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Twiga Stars imeshinda 5-2.
Picha zote Francis Dande wa Globu ya Jamii
Aisee ni macho yangu au vp?nahisi km timu yetu inawanaume au ndio mambo yakina Semenya?
ReplyDeleteCongratulations Twiga Stars!! Mbona uwanja mtupu lakini, kwani viingilio kiasi gani?
ReplyDeleteHongera sana Twiga Stars!Taifa Stars ya wanaume ingevunjwa na tungewekeza kwenye mpira wa wanawake zaidi.Wangepewa kipaumbele zaidi au mechi za Taifa Stars wanaume tungewasilishwa na Twiga stars wanawake;)
ReplyDeleteMtoto wa Kabwela,Sweden.
Go Twiga
ReplyDeleteHongereni Sana Twiga Stars!
ReplyDeleteHONGERA TIGWA STARS:
ReplyDeleteNi muhimu tuache hulka mbaya ya upendeleo wa Kijinsia!
Inaweza tokea katika Familia mtu akawa anawajali zaidi watoto wa Kiume kwa huduma za masomo, malezi na kadhalika na akapuuzia wa Kike, Ilihali ikatokea wa Kike akawa na Faida zaidi kuliko wa Kiume!
Hakuna sababu ya kupoteza muda na Rasilimali UDHAMINI WA SOKA WA MAMILIONI YA KUTOKA MA BENKI,KAMPUNI ZA MITANDAO NA KAMPUNI ZA POMBE NI BORA YAFUTWE ''TAIFA STARS'' NA BADALA YAKE YAELEKEZWE ''TWIGA STAR''!
hebu siku wachezeshwe twiga na yanga tuone kitakachotokea
ReplyDeleteHONGERA SANA TWIGA STARS, HONGERA MWALIMU WA TWIGA STARS, WAHAMASISHAJI, NA WATANZANIA KWA UJUMLA. MAZOEZI MUHIMU "KEEP IT UP TWIGA STARS".
ReplyDeleteThis proves, Wacheza Mpira Wanawake ni Bora Kuliko Wanaume (TZ) .
ReplyDeletejamani wenzangu wa-tanzania hata jezi zetu za taifa za kushangilia na kushabikia shida?, mnaona wageni wetu hapo full jezi ingawasi sio nchi yao hii....jezi za manu unaweza nunua na kizivaa wakati mpira unaonyeshwa kwenye TV, acheni ubahili na ulimbukeni jamanii:-) alex bura, dar
ReplyDeletekikosi kazi cha ukweli jembe
ReplyDeletetuachane na taifa stars sasa tutujiunge kusapoti twiga stars timu ya kweli.
Watanzania 2naweza sema huu unyonge wa kuhusudu vya nje ndio unatudumazaga.
ReplyDeleteWallahi mumenipa raha nyinyi mabinti, hongereni sana.
ReplyDeleteWay to go Twiga stars onyesha wanaume kwamba you are much better than Kilimanjaro. Tunaomba Mungu pamoja na juhudi zenu mutuletee kombe hapa Tz.
TWIGA OYYEEEEEEEEEEEE! MBELE KWA MBELE MUSILEWE SIFA BALI MULETE KOMBE NA SISI TUNAWAPA FULL SUPPORT.
Hongera sana Twiga stars, wanawake tunaweza hata bila kuwezeshwaaaa.
ReplyDeletesafi sana!
Hongera kaza buti forwards ever backwards never!
ReplyDeleteBora Mtoto wa Kike(TWIGA STARS) ambaye ni Mama ntilie ana Faida kwetu ktk Familia kuliko Mtoto wa Kiume(TAIFA STARS) ambaye hana mafanikio kimaisha na kazi yake ni PUSHA WA BANGI!
ReplyDeleteGo Twiga Go, wafute machozi watanzania ambao siku zote wamekuwa kichwa cha mwendawazimu
ReplyDeleteMichu ingependeza ungetueleza pia kutoka kulia kwenda kushoto tunawaangalia kina nani.
ReplyDeleteWatanzania tunakatisha tamaa sana tunaposhindwa kwenda uwanjani kuwaunga mkono Twiga Stars. Tuujaze uwanja huo jamani.
Nimeipenda sana hiyo picha ya Mwanahamisi Omari akiruka daluga la beki wa Namibia, Esther Amukwaya.