Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu ameitaka timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) kuhakikisha inabuka na ushindi kwenye mechi yake dhidi ya Namibia.

Mechi hiyo ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) itachezwa Januari 14 mwaka huu jijini Windhoek, Nambia na timu hizo zitarudiana Januari 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Waziri ametoa mwito huo leo mchana (Januari 11 mwaka huu) katika hafla fupi ya kuiaga timu hiyo na kuikabidhi Bendera ya Taifa iliyofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Timu hiyo yenye msafara wa watu 25 inaondoka leo saa 2 usiku (Januari 11 mwaka huu) kwa ndege ya PrecisionAir kupitia Johannesburg, Afrika Kusini ambapo kesho alfajiri (Januari 12 mwaka huu) itaunganisha safari hiyo kwa ndege ya Air Namibia hadi Windhoek.

Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho ni Asha Rashid, Aziza Mwadini, Ettoe Mlenzi, Fadhila Hamad, Fatuma Bushiri, Fatuma Khatib, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Hamisi, Mwapewa Mtumwa, Pulkaria Charaji, Rukia Hamisi, Siajabu Hassan, Semeni Abeid, Sophia Mwasikili za Zena Khamisi.

Benchi la Ufundi lina Kocha Mkuu Charles Boniface, Kocha Msaidizi Nasra Mohamed, daktari wa timu Dk. Christina Luambano na Meneja wa timu Furaha Francis.

Kiongozi wa msafara ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Lina Mhando na Naibu kiongozi wa msafara ni mjumbe wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Layla Abdallah.

Timu hiyo itarejea alfajiri ya Januari 16 mwaka huu kwa ndege ya PrecisionAir.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Maskini wee..warembo wanateswa bureee...hahaha! Hawa ilikua sio watu wakufanyishwa kazi ngumu namna hii jamani,huku kukubali kila tunaloletewa na jamaa wasio na melanin a.k.a wazungu kutatuharibia kabisa dunia..sasa hebu angalia vipenzi vyetu vinavyokomazwa..hahaha.

    ReplyDelete
  2. Vipenzi vyenu vinavyozunguka na machungwa na maembe siku nzima kwenye mabeseni vikiuza barabarani na jua kali au vinavyolima vijijini havikomazwi? Acha mfumo dume wewe, waache wenzio watafute ugali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...