UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM UNIVERSITY STUDENTS
ORGANISATION (DARUSO)
P. O. BOX 35080-DAR ES SALAAM-TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA.
Kikao cha Baraza la Chuo kilifanyika tarehe 10/01/2012 na kujadili hali ya Chuo kwa ujumla na
Serikali ya DARUSO iliwakilishwa. Hivyo basi Serikali ya Wanafunzi inapenda kuutaarifu umma yafuatayo:
1. Serikali ya wanafunzi (DARUSO) haijafutwa, ipo na inaendelea kufanya kazi. Kuhusu taarifa zilizoenea katika vyombo vya habari kuwa DARUSO imefutwa ni uzushi na tunafanya taratibu za kuwachukulia hatua watu na vyombo vyote vya habari Vilivyoeneza uvumi huo.
2. Serikali ya wanafunzi inaendeleza juhudi za majadiliano kuhusu hatma ya wanafunzi ambao wamefukuzwa na kusimamishwa masomo.
3. Aidha, tunaomba wale wanafunzi wachache ambao wanaendeleza mgomo warudi madarasani na kuendelea na masomo kama kawaida. Pia serikali ya wanafunzi inasisitiza kuwa mgomo unaoendelea sio halali kwani taratibu zote za kisheria na kanuni hazikufuatwa. Kwahivyo tunawaomba wanafunzi wasitishe maandamano hayo ili kuruhusu jitihada zinazochukuliwa na viongozi wao kuzaa matunda ndani ya siku chache
kuanzia leo hii tarehe 11/01/2012.
Imetolewa na:
Hassan Mustapha
Waziri Mkuu



Hili ndilo la manufaa.
ReplyDeleteVijana someni wacheni migomo mutakuja kujutia muda muliopoteza baadae.
Aise poleni sana nyie vijana.Matatizo mengi ya hapo yalianza tu baada ya kile kinachoitwa COST SHARING(Kipindi cha Mutungirehi!-hivi yuko wapi huyu mtu??tulimbeba 'ju kwa ju' pale Nkrumah 1994 ilikuwa noma).Hao wanafunzi warudishwe mara moja bila Masharti..Ebu fanyeni utaratibu PUNCH irudi bwana...chuo hakichangamki bila MZEE PUNCH kurudi.
ReplyDeleteDavid V
hivi tuna mawaziri wakuu wangapi jamani ifikie mahali hivi vyeo viwe na maana. Mara rais mara waziri mkuu, na Mh. Pinda nae ni nani, vipi kama wakakutana katika hafla moja nani atakuwa nani hapo. Hii ni sawa na kuwavisha majoho chekechea
ReplyDeletewe unaesema masuala ya vyeo hujaenda shule nn?maana hapo wamesema ni serikali ya wanafunzi.sasa huyo pinda wako ni wa serikali ya jamuhuri.
ReplyDeletecomment vitu vevye akili kidogo.
David muni
man
Wewe waziri mkuu wa CKD una matatizo, watu wanatafuta haki yao halafu unasema eti mgomo siyo halali. Wewe umetumwa na baba yako Mkandala.
ReplyDeleteKwanza tazameni huyo anonymous wa pili kutoka juu, aliyejiita David V. Amesema kwamba yeye ni muhitimu wa UDSM.
ReplyDeleteAmesema kwamba matatizo yamesababishwa na COST SHARING. Lakini hawezi kueleza matatizo yapi na hiyo COST SHARING imesababishaje matatizo hayo.
Na jee, wakati wa utawala wa Nyerere ambapo hapakuwa na hiyo COST SHARING chuoni hapakuwa na matatizo haya?
Kisha anatoa amri kwamba hao wanafunzi warudishwe mara moja bila masharti.
Baadaye anasema fanyeni PUNCH irudi. Bila ya mzee PUNCH chuo hakichangamki. Wakati wote tunaelewa kwamba PUNCH ilikuwa ni "criminal organisation". Msomi huyu anasema kwamba pasipo crimes chuoni, basi chuo hakichangamki.
Msomi wetu huyo. Na tena kama alikuwa UDSM mwaka 1994, maana yake ni kwamba huyu sasa ni mtu mzima kabisa. Lakini akili zake ndiyo hivyo tena, zimeelekea kusini.
Tatizo kubwa katika hiyo COST SHARING ya sasa wanaopata kipaumbele kikubwa ni wale ambao wazazi wao wanazo ambao HAWASTAHILI KABISA!
ReplyDeleteWewe bwana titus said unakosoa bwana david. Mbona wewe hutoi msimamo wako? Wewe unataka nini.
ReplyDeleteMy take: Chuo kimebadilishwa kuwa uwanja wa siasa, maana huwezi kufukuza wanachuo halafu unasema wasiruhusiwe kujiunga na chuo chochote cha umma maana huu ni uhuni.
Wewe bwana titus said unakosoa bwana david. Mbona wewe hutoi msimamo wako? Wewe unataka nini.
ReplyDeleteMy take: Chuo kimebadilishwa kuwa uwanja wa siasa, maana huwezi kufukuza wanachuo halafu unasema wasiruhusiwe kujiunga na chuo chochote cha umma maana huu ni uhuni.
Wewe bwana titus said unakosoa bwana david. Mbona wewe hutoi msimamo wako? Wewe unataka nini.
ReplyDeleteMy take: Chuo kimebadilishwa kuwa uwanja wa siasa, maana huwezi kufukuza wanachuo halafu unasema wasiruhusiwe kujiunga na chuo chochote cha umma maana huu ni uhuni.
watanzania tumezaliwa na kulelewa katika mazingira yanayotufanya wajinga wa kudai na kutaka haki zetu. wengine hamjui wanafunzi wanachodai alafu unasema wanatumwa, mara siasa. we ndo mjinga. kama hujui kudai haki yako, waache waume zako wakutafutie haki zako. FREEDOM IS NOT FREE''
ReplyDelete