Imeandikwa Na Fabian P. Mghanga

Ni Jumatatu asubuhi. Hali ya hewa ya joto la kadiri ilikuwa ni kitu cha kawaida kwa maeneo haya ya Dar es Salaam kipindi cha miezi hii ya mwisho wa mwaka. 

Tupo darasani kwenye presentation ya somo linalohusu magonjwa ya figo. Mada ilihusu kushindwa kufanya kazi ghafla kwa figo au Acute Renal Failure kwa lugha ya wenzetu. Lilikuwa somo refu lililozungumzia kwa undani tatizo hilo. 

Baada ya mwenzetu mwasilishaji kumaliza kuwasilisha somo lake kikafuata kipindi cha maswali na majibu na masomo zaidi kutoka kwa Profesa aliyekuwa anasimamia ile mada.

Mada ilikuwa moto. Maswali yetu pamoja na uzoefu wa yule profesa ulitosha kuibua somo na majibu yaliyotosheleza kiu zetu za kujifunza zaidi. Kisha baada ya somo akauliza swali kwa hali ya utani kidogo, nani kati yenu anapenda kuwa Nephrologist (daktari bingwa wa magonjwa ya figo). 

Wote tulibaki kimya tukitazamana kisha mwanafunzi muwasilisha mada huku akitabasamu alininyoshea kidole akasema Fabby huyo. Profesa aliniangalia kisha akainamisha kichwa chini kwa masikitiko akasema “I feel sorry for you my friend (nakuonea huruma rafiki yangu)”. 

Sikuelewa kwanini alisema vile nikashtukia tu namuuliza “why Professor?” Huku bado akiendelea kunitazama akanijibu “because you will be seeing your patients dying everyday”. Jibu lake ghafla likanirudisha nyuma kama mwaka mmoja hivi nikiwa nafanya kazi hospitali moja ya Mission iliyopo mkoa fulani kusini mwa nchi.

Ilikuwa siku ya Jumatano asubuhi. Hali ya kaubaridi baridi iliyokuwepo siku hiyo iliashiria kuanza kwa siku njema. Ninaingia wodini na kusalimiana na wauguzi wa wodi yangu kabla ya kuingia ofisini kujiandaa na round. Nilikuwa na kawaida ya kuanza siku kwa kufanya round kwa wagonjwa waliolazwa kabla ya kuingia ofisini kuwaona wagonjwa wengine wapya na wale wanaokuja kwa ajili ya follow up.

Baada ya kuwaona wagonjwa kadhaa, nikakifikia kitanda cha mgonjwa mpya aliyekuwa amelazwa usiku wa kuamkia siku hiyo na kuonwa na Clinical officer aliyekuwa zamu. Ni binti wa miaka takribani 20 (kwa sababu za kimaadili sitataja jina, umri wake halisi, mahali anapoishi wala details zake nyingine).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. VIFAA NA MAZINGIRA BORA YA KAZI HUZAA HUDUMA BORA ZA AFYA:

    Somo la Habari hii linajieleza vizuri sana.

    Isipokuwa ni jambo la ajabu sana ukakuta Serikali ya Nchi fulani Duniani inaelekeza idadi ndefu ya Masifuri ya FEDHA (MABILIONI) katika Sekta ya SIASA badala ya HUDUMA YA AFYA!

    HIYO SERIKALI YA NCHI SINA HAJA YA KUITAJA MTAJAZA WENYEWE!

    ReplyDelete
  2. Huwezi kupanda Bangi ukavuna Mchicha!

    Huwezi kuwekeza katika Siasa halafu ukavuna huduma bora za Afya.

    Ukiwekeza zaidi katika Siasa utavuna Ubabaishaji na Ufisadi.

    Huduma bora za afya ni pamoja na kuwekeza sehemu kubwa ya Bajeti ya matumizi katika Sekta ya afya!

    ReplyDelete
  3. Duh!Afadhali mimi mwalimu.Kumtazama mgonjwa anayekata roho huku uwezo wa kumsaidia unao lakini nyenzo hamna INAUMA SANA tena inaharibu kisaikolojia kuliko mimi ninapomfundisha Physics mwanafunzi pasipo vifaa wala chumba maalumu cha maabara.

    ReplyDelete
  4. It is real frustrating to work on this situation. After reading your sad story I feel sorry for Tanzanian doctors. I am not sure what the quick fix here is. Money is there but so many leaders are corrupted and the governing system is bad. My opinion the government should use 50% of the gold, songo songo gas, diamond, coal, gold income to fund for health and education. Where does that money go????

    ReplyDelete
  5. Maskini doctor, pole sana aisee... Nimeisoma hii article yote mpaka nikajikuta nabubujikwa na machozi bila kujua! Frankly speaking, the government needs to DO something now!!

    Dennis

    ReplyDelete
  6. Hii imeelezwa vizuri kabisa, lugha nzuri , hongera
    By far GOOD point nimekuwa so touched , mungu nipe utajiri niisaidie nchi yangu. Ni vigumu kuona wagonjwa wako wanakufa mikononi mwako, na huwezi kuwasaidia, tena tu kwa sababu huna vitendea kazi loh! mungu tusaidie

    ReplyDelete
  7. Nafikiri wanasiasa wanaosoma mtandao huu wanahitaji kusoma hii habari kabla ya kuamua kubwabwaja mbele ya wananchi kuwa madaktari wanasababisha vifo vya wagonjwa mahospitalini.
    Pia wao kuona kuwa mgomo huu una lengo la uzalendo na kujenga Tanzania imara na yenye huduma bora za afya.

    ReplyDelete
  8. Wakati mwingine watu wanalaumu serikali bila kuangalia nyuma. je unajua ni vifaa kiasi gani vinaibiwa/kupotea mikononi mwa wauguzi na madaktari. hebu fuatilia vifaa vilivyoletwa na wakorea katitka vituo vya afya vya Sinza,Ilala, M/MMoja, Nk uone vilivyobaki.

    ReplyDelete
  9. NI MUHIMU KUBADILI MUELEKEO NA SASA INGEFAA TUANGALIE UWEZEKANO WA KUIWEKA SEKTA NA HUDUMA YA AFYA KATIKA MIKONO YA SEKTA BINAFSI:

    KWA NJIA HII:

    1.MADAKITARI NA WADAU WA AFYA INGEFAA WAPEWE MAMLAKA NA UWEZESHAJI HATA KWA KUPEWA MIKOPO ILI WAFUNGUE HUDUMA ZA AFYA ZA BEI NAFUU NA KUZIMILIKI BINAFSI KWA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI.

    2.SERA YA HUDUMA YA AFYA IBADILIKE BADALA YA SERIKALI KUIENDESHA SASA JUKUMU LAO LIBAKI KUSIMAMIA NA KUKAGUA.

    ReplyDelete
  10. Anonymous wa mwisho, kweli umeshidwa jua sababu ya vifaa hivyo kuibiwa? Kwa kifupi ni njaa,...

    ReplyDelete
  11. Mimi inanisikitisha saaana kuona madaktari wetu mahili tuliowasomesha kwa kodi zetu sasa wanakimbilia Botswana, Burundi na Rwanda kwa sababu tu ya siasa za baadhi ya wanasiasa na viongozi wa serikali. Hivi hawa viongozi wanafuatilia wenzetu hao wa nje wanaendeshaje huduma za afya mpaka madaktari wetu wakimbilie huko? Lazima sisi tutakuwa wrong somewhere, jukumu la viongozi wa sekta ya afya ni hili sasa kuangalia na kufanya tathmini. Haiingii akilini kuona viongozi wanatumia vitisho badala ya kuzama kwa undani kuangalia matatizo yaliyopo, hivi kazi zao za kiuongozi za kila siku ni nini?. kufukuza madaktari so what? uongozi si kukomoa unaowaongoza, hivi haikuwa rahisi kusema madaktari mnataka tukutane jumatatu sawa tupange jumatatu tuzungumze, ilikuwa ni suala la siku moja tu jumapili na jumatatu.Kweli tunatofautiana jinsi ya kufikiri, kuona, kuamua na kuwa na busara.

    ReplyDelete
  12. Jamaniii!uuuuuwwiii!!nalia lakini najua yapo mengi zaidi ya haya.mimi binafsi niliwahi kupata tatizo la moyo ndio nilipobahatika kuzijua hospital karibu zote.jamani mahospitalini kuna hali mbaya.hivi hakuna kabisa asasi za kiraia kuhusu afya,kama ilivyo haki elimu na haki ardhi?kama hamna jamani naomba tuianzishe itusaidie.tatizo la afya lisiachiwe wanasiasa watatumaliza.DAKTARI KUFANYA KAZI KWENYE MAZINGIRA YASIYOKUWA NA VIFAA NI SAWA NA DEREVA WA BASI LA ABIRIA KUENDESHA BILA BREKI.MWISHO WA SAFARI NI VIFO.NA UWEZO WA KUEPUSHA UPO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...