Ankal, salaam. Vita dhidi ya rushwa ni yetu sote. Picha hii ni ya trafiki waliopo eneo Bwawani katika barabara kuu ya Chalinze-Morogoro. Nilikaa hapo jana kwa muda na kushuhudia wakipokea rushwa kwa namna ya kusikitisha kweli kweli. Vijana wanaoonekana hapo hujifanya wakisafisha gari wakati rushwa ikipelekwa kwa askari ambao hawashuki kwenye gari hilo. Baada ya kubaini nimewapiga picha, trafiki mmoja akaniufuata ndani ya basi na kuanza kupambana na mimi. Lakini nilimshinda baada ya kubaini kuwa hana uchuzi wowote na Digital Camera. Iweke picha hii ili pengine trafiki wapunguze kula rushwa jamani.
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Nadhani mdau aliyeandika habarti hii alikuwa na haraka, kwani kuna spelling error kadhaa. Hata hivyo hii ni habari ya kusikitisha sana. Trafiki wanakula rushwa kama hawana akili nzuri. Nakumbuka jana abiria fulani alipiga picha hii akiwa ndani ya basi la Upendo. Sikujua kama aliipata maana trafiki walianza kumbana, lakini akafaulu. Amenikumbusha ya Jerry Mullo.
    Safi sana

    ReplyDelete
  2. Ni aibu tupu. Rushwa ya trafiki wala si kubwa. Wanapokea hadi Sh 500 (mia tano). NI aibu tupu.

    ReplyDelete
  3. ndoto ya kuisha kwa rushwa itabakia kuwa ndoto na kamwe haitoisha

    wakuu wanaogopana sasa unafikiria kuna atakae mkemea mwenzake kwa kupokea rushwa?

    ReplyDelete
  4. JESHI LA POLISI LINANUKA KWA RUSHWA.

    ReplyDelete
  5. kwanini nani atakayemzuia polisi kula ruswa?na sasa itapaa zaidi.Kwani hao PCCB wao mbona sasa ndiyo wala rushwa wakubwa?
    Baada ya serikali kuona polisi imekithiri kwa rushwa ,walibuni PCCb na sasa PCCB nao wamekuwa balaa,sasa sijui watabuni nini tena?Rushwa imeanzia viongozi wakubwa wa serikali na ndiyo maana hakuna anayejari na mwisho wa siku tutapogana tu.MUNGU INARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  6. unasumbuka na vidagaa wakati mapapa yametulia tu.

    ReplyDelete
  7. mmhhh?mhhhh!Gerry Murro yuko wapi?

    ReplyDelete
  8. JAMANI NDIO BONGO KIYO KILA MTYU ANA KULA RUSHWA YAKE KWA NAFASI YAKE BILA MSONGO. SASA KAMA WEWE HUTAKI KUTOA RUSHWA BASI MAMBO YAKO HAYAFANIKIWI WEE ACHA TU TUTAFIKA LAKINI , KWA SABABUI SIMLAUMU ASKARI HUYO KULA RUSHWA KWANI KUANZIA HUKO MPAKA KUSHUKA NI RUSHWA TUPU , LAKINI TANZANIA SASA SIO RUSHWA NI BAAH SSHISH!. KWANI HAKUNA MTU ANAEFUNGWA HAPA TANZANIA UKIWASHITAKI NDIO HAO HAO WANAKUGEUZIA UBAO WEWE NDIO UNAKWENDA JELA NA MASHITAKA YA KUSEMA UONGO NA VIDHIBITI KIBAO JUU YAKO KAMA YALIVYOMTOKEA NDUGU YETU AMBAYE KANUSURIKA KATIKA TUNDU LA SINDANO KUFUNGWA MIAKA 25 JELA KWA KUSEMA UKWELI KUHUSU POLISI(JERRY mURRO).KISA KATOA SIRI YA ASKARI ANAEKULA RUSHWA BABABARANI HATA HUYO RAIS ANAJUA KITU HICHO LAKINI KAFUMBIA MACHO KANA KWAMBA NOTHING IS GOING ON ,RAIA NI WAONGO!

    TANZANIA HOYEEEEEEEEEEEEEE!!!!!
    mdau dar es salaam

    ReplyDelete
  9. Waacheni wale mnataka wao waishi vipi...wabunge wanajiongezea posho, mafisadi wanazidi kuitafuna nchi, hata mimi nikipata mwanya naila vizuri.

    ReplyDelete
  10. Safi sana mdau! mapambano ni makali na inapendeza kuona sasa jamii inashiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa. Juzi kule kwa MJ yametolewa madudu ya TBS, nae akavamiwa kwa mtindo wa ciber! Aluta Continue, kila mtu ana wajibu wake katika kutokomeza rushwa!

    ReplyDelete
  11. Ankal, Umeshasahau ya Jery Muro. Utaingia kwenye mawindo na wewe sasa hivi. Jery na yeye alijifanya kimbelembele kwa hawa majamaa mimi simo!!!!!

    ReplyDelete
  12. i think to expose this askari takin rushwa is wrong hawa wanatafuta kula i think u should expose bigger picture of corruption not this petty rushwa

    ReplyDelete
  13. Hapo umechemsha mbona hii picha haina maana yoyote? kiboko yao alikuwa jerry muro.

    ReplyDelete
  14. MDAU ASANTE SANA KWA PICHA NA MAELEZO. CHA KUSHANGAZA HII POST INAPITA HAKUNA HATA MDAU ALIYECHANGIA MADA....AU WOTE NDIO TUMEKAZOEA KAMCHEZO HAKA KACHAFU!!!
    HUYO MWELA SI ATAJIONA KASHINDA VITA AU BWANA ANKAL UNABANIA MAONI YA WATU KUHUSU HILI!!!MJOMBA NINI HUYO UNAMLINDIA KITUMBUA CHAKE!!!!

    ReplyDelete
  15. Unaporipoti hivi iambie pia serikali iboreshe mishahara yao,nayo yote iache kula rushwa kubwa kwenye ikataba inayolihusu taifa letu!!

    ReplyDelete
  16. Hongera kijana wa kitanzania na mwenye uchungu wa nchi yako, lakini chonde chonde baba ukipata nafasi mpate kijana mwenzio Jerry Muro muulize yaliyompata wakati alipofuatilia nyendo za watu wa namna hii. Alitupa full newz za rushwa zinavyokwenda kutoka kwa wenye magari makubwa kupitia kipindi chake through TBC1, eeeeeeh siku mbili tatu watu wametega mtego ambao kidogo kachangamka kauruka kiunzi. Cha kusikitisha sana hata hao TBC wenyewe wenye kipindi wamembwagia virago wakati tulijua watahangaika nae. MCHI HII HAIJENGEKI NYERERE KAONDOKA NAYO MWENYEWE

    ReplyDelete
  17. samahani lakini hao polisi wanataka hela ya kula sio kama wengine serekalini walio iba mabillion na hakuna anayewakamata au kuwapiga picha

    ReplyDelete
  18. acha ukuda

    ReplyDelete
  19. wakale wapi????...utajiju

    ReplyDelete
  20. Tunaelewa kinachoendelea mabarabarani, na hii picha ni ushahidi. Ila sidhani kama ni ushahidi wa kutosha, hasa mahakamani. Hapa trafiki akibisha kuwa haikuwa rushwa bali alikuwa anamuandikia mtu faini utamruka vipi? Kisha anakugeuzia kibao kwa kumchafulia jina na kumhatarishia 'ujira' wake?

    ReplyDelete
  21. Lakini ndugu yangu uliyeandika habari hii ukumbuke kuwa hata sisi wananchi tunachangia hali hiyo kwani sisi ndo tunawashawishi wapokee hizo rushwa ili tusilipe faini.

    rushwa haitaisha kamwe mpaka wananchi waache kutoa rushwa.

    ReplyDelete
  22. Mdudu huyu hawezi kuondoka kirahisi.mim naamini ingelikuwa wanapata mishahara minono katu wasingetaka vijisenti.hawa wanapoteza maisha wakati mwingine. Wale waliokuwa wanataka posho nyngeza "wawakilishi wetu" watufanyia nini zaidi ya kuengezeka vitangu kila kukicha.

    ReplyDelete
  23. Ni ngumu kuipiga kwani ni utaratibu wa utawala wa serikali ya Tanzania,institutional.Hawa hizo pesa wanapeleka kwa wakubwa kuna kiwango ambacho lazima wapeleke kila siku.Ni kwamba kuna fungu OCD hupelerka kwa RPC,na yeye kwa IGP, na yeye juu zaidi.Ni mfumo wa utendaji wa nchi sio siri kwa hiyo picha haisaidii ila kubadilki mfumo kwa amni au nguvu ndio utasaidia

    ReplyDelete
  24. Hawa jamaa ni kweli wankula rushwa kweli,mimi mnamo tarehe 04/januari/2012 nilipita hapo wakanibambika kosa la spidi nikawaeleza wanipatie print out inayoonyesha muda,namba ya gari na spidi niliyokuwa nayo wakaanza kunitukana ati tunakupatia nitification utalipa tsh 30,000= nikabishana nao sana huku hao vijana wakiosha gari nikaona napoteza muda wangu kwa watu wasio wastarabu nikasema nitalipa hiyo faini wakanijiu juu ati kama unataka kulipa basi unamakosa mawili na moja ni la kubishana na sisi,nikawweleza sikilizeni ninyi ni kwasababu nna haraka na sihitaji kupoteza muda naweza kuwapeleka mahakamani na nikawashinda!ndo mmoja akaja akasema ohooo sikiliza mzee badala ya kulipa tsh 30,000=fanya tshs 15,000= uishie!niligoma katakata nikawaeleza nipeni notification mimi ntalipa hy 30,000= nikalipa,wakaanza kunishambulia ohooo unajifanya una hela sana tunakuhakikishia utashikwa njia nzima nkasema sawa!nikaondoka zangu ukweli hawa jamaa si
    askari bali ni vibaka wanalipakazia jeshi la polisi matope naomba salamu hizi zimfikie Kamanda Said Mwema.

    ReplyDelete
  25. tuchukue namba na kuripoti hili tukio takuru.

    ReplyDelete
  26. Nilipita hapo tarehe jan 22 jumapili mchana, jamaa walinisimamisha kuwa nimekwenda mwendo mkali 65kmh badala ya 50kmh. Waliniomba nilipe sh 10,000 on the spot fine. Nikasema sina, ila nikawambi waniandikie bill niende morogoro polisi nilipe. Walikata katakata na sikulipa baada ya kubishana nao sana. Cha ajabu, kila gari iliyo simamishwa,dereva aliambiwa kua ameendesha 65kmh badala ya 50kmh. Madereva wengi walikua wanadondosha hela kupitia dirisha la driver la hiyo gari ya police na kuondoka. Nilikua hapo kwa muda wa dakika 45 nilishuhudia zaidi ya magari kama 15 hivi yakisimamishwa na kutoa kitu kidogo. Ni aibu.

    ReplyDelete
  27. Msiwalaumu wanaotafuta pesa ya kulisha familia zao,kwa kuwa hawana njia nyengine,wakati mabosi wao,mawaziri,mameneja,majenerali hawali bali wanabugia rushwa.mimi napiga vita rushwa vibaya vibaya,lakini sio rushwa hiyo ya ngazi ya chini ya mlalahoi anaefanya kazi mwezi mzima na akapata mshahara wa siku tatu.Siwatetei hao wakuda lakini kama vita ya rushwa tuianze juu.
    Mungu atubariki.

    ReplyDelete
  28. Babu hao jamaa ni NOUMA,na huu mradi wa TOCHI ndo ushakua balaa,manake kuna trafik mmoja huku mbele ya UYOLE ukishashuka mlima nyoka mbeya huku,mjamaa analala nayo TOCHI nyumbani kwake,anaweza akakurupuka hata usiku wa saa 10,na kutega mbele ya kibao cha 50 KMP,ni anaramba vichwa mbaya sana.

    ReplyDelete
  29. mishahara yao miduchu sana wataishije? bora hao kuliko mafisadi wanakwapua, au na wao wagome kama mdr? rushwa nchi hii wote tu naona, siibariki ila kunatakiwa measure kubwa zaidi na sio nguvu au kuumbuana! itafutwe model mbadala kudeal nayo, na hiyo ni " Fair Payment kulingana na Hali halisi ya Maisha, wewe ulietoa 30,000/ fasta seems unazo nyingi, kwa wengine hiyo ni kodi ya six months! askari longa nae buku 2 tano unasepa! ni km kuwasaidia, they are paid 150,000/ per month imagine! kuna manesi, walimu, but tujue nchi hii ingekuwa na mfumo mzuri, hela inayopotea kiholela ingetumika vyema wote tungekuwa fairly paid!

    ReplyDelete
  30. Si kweli hii picha ya kutengeneza,hivi hamjui siku hizi computa inaweza kufanya maajabu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...