Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Philipo Mulugo (katikati) akitoa tamko kuhusu hatma ya wanafunzi waliofutiwa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011 ambapo Serikali imeamua watahiniwa 9,629 waliofutiwa matokeo kutokana na kubainika majibu yao kufanana kurudia mtihani wa darasa la Saba mwezi Septemba mwaka huu 2012 . Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Elimu ya Msingi Zuberi Samataba(kulia) na Mkuu wa Idara ya Elimu ya Sekondari na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Charles Philemon(kushoto).Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam
Home
Unlabelled
wanafunzi waliofutiwa matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011 kurudia mtihani Septemba mwaka huu 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
nadhani serikali inawaadhibu watoto ambao hawasitahili kuadhibiwa. nadhani ingekuwa vyema kama watoto hawa hawatapotezewa mwaka kwa kupewa mtihani mwingine sasa. nadhani ni rahisi kuweka kituo kimoja cha mtihani kila mkoa uliokumbwa na matatizo hayo.
ReplyDeletejamani tunawaumiza watoto hawa bure
Tuambiwe basi kwa kipindi chote watakuwa wapi? watahudhuria madarasani? watajisomea majumbani? watafundishwa au wataandaliwa na nani? na kwanini muda mrefu hivyo? Food for thought
ReplyDelete