Kampeni iliyoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kuchangisha fedha kupitia Red Alert na M-pesa imewezesha kupatikana kwa shilingi 11,607,470/=

Kampeni hiyo iliyodumu kwa wiki tatu kuanzia Disemba 22 mwaka jana hadi Januari 10, 2011 imewezesha kupatikana fedha hizo zilizochanganywa na wateja kuunga mkono juhudi za Vodacom za kusaidia waathirika wa maafa.

Kampuni ya Vodacom ilitangaza kuwashwa kwa nambari ya Red Alert na kuweka nambari maalum ya kuchangia kwa M-pesa saa chache baada ya kutolewa taarifa rasmi za kuwepo kwa athari kubwa za mvua zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo Dar es salaam.

“Kila mtu alikuwa na nafasi ya kusaidia kuokoa na kusitiri maisha ya wenzetu waliothiriwa na ndio maana tukawasha nambari ya Red Alert na kuruhusu uchangiaji kupitia M-pesa” Amesema Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Mwamvita Makamba.

Nambari ya Red Alert hutumika na Vodacom wakati wa maafa kuwezesha wateja kuchangia fedha kusaidia waathirika na hakuna makato yanayofanywa katika ujumbe mfupi unaotumwa katika nambari hii ili kiwango kinachopatikana kiwanufaishe waathirika moja kwa moja.

Maafa yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Dar es salaam Disemba mwaka jana yaligharimu maisha ya watu huku maelfu ya familia yakiachwa bila makazi.

“Ni jambo la faraja kwamba tumeweza kusimama kama familia moja ya Vodacom wafanyakazi, wateja wetu na wadau na kuonesha upendo wetu dhidi ya wenzetu walioguswa na maafa hayo”. Aliongeza Mwamvita.

Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusiadia jamii – Vodacom Foundation inaandaa utaratibu wa michango hiyo kuwanufaisha walengwa kama ilivyokusudiwa.

Awali Vodacom Tanzania ilichangia vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni thelathini ikiwemo vyakula, magodoro na mablanketi kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam waliokuwa wakiishi katika kambi maalum kwa wakati huo.

Ujumbe mmoja wa maneno kwenda nambari ya Red Alert 15599 uligharimu Tzs 500/-, na kwenda M-pesa nambari 155990 uligharamiu Tzs. 1,000/- na kwamba hakukuwepo na ukomo wa kutuma ujumbe na kuchangia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nimefurahishwa na habari hii pia kwa kuona watanzania wameanza kuongeza moyo wa kujaliana hata kama msaidiwa si wa kutoka katika familia moja au ukoo moja. Eeeh! Mungu tuongezee moyo huu kuanzia sasa na hata milele

    ReplyDelete
  2. WATEJA WA VODA WAKO JUU KAMA KAMPUNI YAO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...