MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WA MKOA WA RUVUMA AMBVAYE PIA NI MKUU WA HUO SAID MWAMBUNGU AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI HIYO,WATENDAJI WA MITAA NA WENYEVITI KUFUATIA MAUAJI YA WANANCHI YANAYOFANYWA NA WATU WASIOJULIKA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA. KULIA NI MKUU WA WILAYA YA SONGEA  MH. THOMAS SABAYA.
MKUU WA WILAYA WA WILAYA YA SONGEA AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA HIYO THOMAS SABAYA AKIZUNGUMZA AKIZUNGUMZA WAKATIKA WA KIKAO CHA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA RUVUMA KUSHOTO NI MKUU WA MKOA HUO SAID MWAMBUNGU. 
WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA RUVUMA WAKIMSIKILIZA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO AMBAYE PIA NI MKUU WA MKOA HUO SAID MWAMBUNGU HAYUP[O PICHANI WAKATI WA KIKAO CHA KAHIYO KILICHOKAA BAADA YA KUTOKEA MAUAJ YA VIJANA 3 NA MAANDAMANO KATI YA POLISI WA KUTULIZA GHASIA NA VIJANA HAO,
WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA RUVUMA WAKIMSIKILIZA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO AMBAYE PIA NI MKUU WA MKOA HUO SAID MWAMBUNGU HAYUP[O PICHANI WAKATI WA KIKAO CHA KAHIYO KILICHOKAA BAADA YA KUTOKEA MAUAJ YA VIJANA 3 NA MAANDAMANO KATI YA POLISI WA KUTULIZA GHASIA NA VIJANA HAO,
POLISI WAKIWA NA VIJANA WALIOSHIRIKI MAANDAMANO HARAMU KATIKA MANISPAA YA SONGEA KUPINGA MAUAJI YA WENZAO HASA MADEREVA WA PIKPIKI YANAYOENDELEA MJINI HUMO,
POLISI WAKIWA NA  MMOJA KATI YA VIJANA ALIYESHIRIKI MAANDAMANO HARAMU MJINI SONGEA KUPINGA MAUAJI YA RAIA YANAYOENDELEA MJINI HUMO AMBAPO HADI SASA WATU 10 WAMESHAUAWA NA WATU WASIOJULIKANA,
POLISI WAKIONDOA MAGAGOGO YALIOWEKWA BARABARA NA VIJANA WA LIZABONI KUPINGA WENZAO KUUAWA NA WATU WASIOJUKLIKANA KATIKA MAENEO MBALIMBALI MJINI SONGEA,
POLISI WAKIONDOA MKOKOTENI ULIWEKWA BARABARANI NA VIJANA WALIOANDAMANA KATIKA ENEO LA LIZABONI MANISPAA YA SONGEA,
ASKARI WA KUTULIZA GHASIA FFU WAKIMSHIKILIA MMMOJA WA VIJANA WALIOKUWA WAKIWARUSHIA MAWE KATIKA MAPAMBANO KATI YA POLISI NA BAADHI YA WAKAZI WA SONGE.PICHA NA MUHIDIN AMRI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Suala la kuua wananchi kwa risasi sasa limkuwa normal kwa Police. There is no justification ya kumpiga risasi mtu anayekurushia mawe.

    Wakipigiwa simu kuna majambazi yana silaha yanavunja sehemu wanajivutavuta kwenda ila wananchi wasio na silaha ndiyo wanona soft target ya kuona kama risasi zao bado zinaua.

    Vyovyote watakavyoandika hakuna justification ya kutoa uhai wa mtu alikaa tumboni kwa mama yake miezi Tisa akahudumiwa kwa miaka 20 au 30 na wazazi wake halafu wewe unakuja kuyakatisha kwa sekunde moja tu ya ku-pull trigger. Kuua mtu ni uamuzi mzito sana ambao unatakiwa kupata baraka za mahakama tu.

    Kosa la kumtupia mawe polisi si kifo, hiyo ieleweke. Polisi wanakuwa wavivu katika kutekeleza majukumu yao, wanatumia short kati. Kama watu hao wangekuwa na silaha za moto kweli ningekuwa upande wa polisi 100%. Maana mwenye silaha ya moto akienda Rogue njia pekee ya kulinda wengine ni kumuangusha yeye.

    ReplyDelete
  2. POlisi wa Tz bado mmelala, mtawapigaje watu wenye njaa? Je hiyo ni human rights au ile MP D.C wa Uk aliyokuja kuwaletea ya kuoana kwa jinsia moja? Mbona sisi bado giza lipo? Na je mlkuwa wapi wakiweka hayo magongo?

    ReplyDelete
  3. Si haki kabisa kwa Polisi kuwapiga risasi za moto wananchi waliokuwa wanarusha mawe. Jamani mabomu ya machozi na maji ya kuwasha si yangetumika!

    ReplyDelete
  4. Maisha ya Binaadamu ni GHALI na HAYARUDISHIKI kuliko gharama ya Mabomu ya Machozi na Risasi!

    ReplyDelete
  5. Uwekwe ulinzi shirikishi na pia si busara kumpiga mawe askari. Wanaoua waendesha yeboyebo lazima ni ktk jamii hiyo na si askari hivyo tuwe makini zaidi

    ReplyDelete
  6. Hivi maisha ya binadamu walikufa kwa kugoma madaktari yalikuwa sawasawa. Myonge mnyogeni na haki yake mpeni. Mmeona ugirika wanavyoshughulikiwa waandamanaji.

    ReplyDelete
  7. Hakukuwa na sababu ya kuua watu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...