Balozi Maajar akimsikiliza mwalimu wa Chuo cha Milwaukee Area Technical College (MATC) akionyesha mitambo ya kujifunzia na kuelezea jinsi wanafunzi wa chuo hicho wanavyotumia teknolojia kujifunza kwa vitendo mitaala ya ufundi wa nishati ya umeme
Balozi Maajar akiwa kwenye studio ya radio ya WUWM (Milwaukee Public Radio) akizungumzia madhumuni ya ziara yake Jimboni Wisconsin kwenye kipindi mashuhuri cha Lake Effect kinachorushwa na mtangazaji Mitch Teich jijini Milwaukee. Listen to full Lake Effect Radio Interview at
Balozi wa Tanzania nchini marekani Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akipewa zawadi na Makamu wa Rais wa kampuni ya A. O. Smith Corporation Bw. Steve Rettler mara baada ya kuzungumza na wawakilishi wa makampuni takriban thelathini kutoka miji mbalimbali ya Wisconsin wenye nia ya kufanya biashara na Tanzania
Balozi Maajar akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watazania waishio kwenye mji wa Milwaukee, Jimbo la Wisconsin waliofika hotelini kwake kumpokea mara baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya kikazi .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...