Warembo walioshiriki Miss Tanzania mwaka 2011,wakiongozwa na Mrembo anaeshikilia taji hilo.Salha Israel (wa tatu kushoto) wakifungua pazia kuaziria uzinduzi wa nembo mpya ya Redd's Miss Tanzania 2012 wakati wa hafla iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.
Baada ya Uzinduzi sasa ni Burudani ya kijipongeza kwa warembo wa Miss Tanzania na Wakuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ndio wadhamini wakuu wa Redd's Miss Tanzania 2012.
Miss Tanzania anaeshilia ttaji hivi sasa,Salha Israel akiwa na kinywaji cha Redd's Original mbele ya Nembo mpya ya wadhamini hao.
Cheazzzzzzzz.....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. TUMECHOKA NA HIVI VICHUPI JAMANI LOOH

    ReplyDelete
  2. hayo magoti sasa! hao sio 'miss tanzania" halisi, bora nyerere alipiga marufuku haya mambo! kwa nini tusibaki na mashindano mengine na hao "reds" wakaweka hizi fedha kwenye mambo mengine? itabidi pia tufanya tathmini ni kwa kiasi gani "umiss" umeitangaza tanzania, kama kuna maeneo mengine yanaitangaza tanzania zaidi then tuweke kipaumbele huko. Leo nimeangalia tv citizen ya kenya nikaona tangazo la shirika la ndege la uganda, wanatangaza shirika na uganda pia, utaona group ya waganda wanacheza ngoma za kiganda na pia alama zao za nchi zinatoka vizuri kabisa. Jamani Tanzania!!!!

    ReplyDelete
  3. jamani haya mavazi sasa ni kupitiliza nadhani ipo haja ya kukemea.

    Sijui alaumiwe nani kwa kweli inaumiza mno kuona mavazi ya hawa wasuchana mweee Mungu utusaidie

    ReplyDelete
  4. Hivi hapo Miss ni nani, hao waliovaa vimini au Victoria Kimaro?

    ReplyDelete
  5. Ajabu kwenye hiyo picha ya Cheazzzzz kuna bwana amevaa vizuri na tai nzuri nyekundu na bidada amepiga gauni yake nyekundu ndefu kabisa (nadhani ni staff wa wadhamini) wakati hao tunaowaita warembo wamepiga vichupi. Ili ku-balance angalau 50% ya wanaoandaa nao wawe wanapiga vichupi badala ya wao kuwa na nguo ndefu alafu wenzao wamevaa vichupi.

    Nawasilisha

    Mdau

    Jodoki Kalimilo

    Mwanza

    ReplyDelete
  6. wewe mdau wa maoni namba 2 acha ushamba wako wewe fala, wewe magoti ndio umeona issue? wewe bado unamkumbuka nyerere mpaka leo walikwisha kufa wala hawajui ni nini kinachoendelea huku duniani . Nenda kamuamshe mwabie watu siku hizi wanatembea uchi uone atakwambia nini! Mama yake tu mzazi na Nyerere alikuwa anatembea matiti yako nje sasa hayo magoti wewe ndio umeona ni porno kupindukia?Au nikutumia picha za mama yake mzazi mzee nyerere uone jisi gani alivyokuwa akivaa?

    ReplyDelete
  7. Kwa namna hii vazi la taifa litavaliwa kweli???????? vivyo vinguo ni vifupi mno jamani, huo ni utamaduni wa wapi???????? wasichana jirekebisheni.

    ReplyDelete
  8. MUNGU WANGU HIV KWELI KUNA MTU HUA ANATAMANI Hawa wavaa vichupi wawae wake zao dunia hii kwishnei kama mama atavaa hv mbele ya kadamnasi sasa unategemea watoto wao itakuaje... mu
    mungu atuepushe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...