Ankal akiwa na Wazee wa Kazi wa Serengeti Freight Forwarders Waarabu Chris na Muhisin Uwanja wa Nyumbani barabara ya Ripple Road, Barking, London, IG11 OSN ambako sio pa kukosa uwapo katika jiji hilo kwani pana machopochopo yote ya nyumbani na muziki wa home.
Ankal akitoa zawadi kwa mshindi wa pili wa Pool wa wiki hii Uwanja wa Nyumbani. Kila Jumatno kuna mtanange wa Pool ambapo mshindi wa kwanza na wa Pili huondoka na mkwanja swaaafi
Ankal akitoa zawadi kwa mshindi wa kwanza wa Pool wiki hii Uwanja wa Nyumbani
Menyu ya Uwanja wa Nyumbani. Ugali, nyama choma na Kisamvu.... Acha!
Ankal akiwa na anko Abuu, mwenyeji wako wa Uwanja wa Nyumbani
Hapo gemu la pool linataka kuanza na tayari wafadhili wameshapandisha chata yao..
safi sana vijana wa london, hii ndio inatakiwa sio watu kupiga domo tu mnatakiwa mnafanya mavitu kama haya, Hongera sana wazee wa kazi na abuu . BIG UP!
ReplyDeleteankal angalia wasikulishe kiti moto!
ReplyDeleteAnkal ugali wote na nyama zote hizo utamaliza peke yako!! Lakini sawa maana huko baridi nyingi ina bidi uweke mavituz tumboni. kIla la heri mzee.
ReplyDeleteAnkal hebu acha ubahili. kwenye picha mpo watatu lakini sahani za ugali zipo mbili, nyama sahani mbili, chupa mbili,vichupa vya chumvi viwili na glasi mbili. Hivi kweli mmeshindwa kumlipia mwenzenu chakula chake mpaka ajibane kwenye sahani zenu kiasi hicho? Kwani maisha yamekuwa magumu kihivyo?
ReplyDeleteUgali ni chakula ambacho haunilishi hata kwa dawa.
ReplyDeletehongera kaka wa uwanja wa nyumbani, maisha ni popote alimradi huvunji sheria za nchi husika mambo mswano... ujasiriamali oyeee!
ReplyDeleteAnkal naona picha ya juu kabisa unafakamia ugali na cholesterol. Kumbe tuko wengi. Anyway, hiyo sehemu inaonekana imetulia sana. Nikija London itabidi nipatafute. Hapo panaonekana ni home away from home.
ReplyDeleteAnkal walahi mimi nipasie nyama finyango moja tu!
ReplyDeleteKiti moto kwa UK tena si ndio kwao,,,hujui Msafiri Kafiri?
ReplyDelete