Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu amemteuwa Abdul-hakim Ameir Issa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumushi ya Mahakama Zanzibar

Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa habari Mrajisi wa Mahakama Yessaya Kayange amesema kuwa kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Sheria ya Utumishi wa umma namba 2 ya mwaka 2011 kifungu namba 34(2) ambapo kifungu hicho kimemtaka Jaji wa mahakama kuteuwa mwenyekiti ambaye anatakiwa kuwa na sifa za Jaji wa Mahakama kuu

Aidha Jaji Mkuu ameteuwa wajumbe watano wa Tume hiyo,akiwemo Kadhi mkuu wa Zanzibar Skh Khamis Haji Khamis,Safia Masuod Khamis Mwanasheria wa Serikali anayemwakilisha Mwanasheria Mkuu,Salum Taufig Ali Wakili wa kujitegemea anayewakilisha Chama cha Wanasheria Zanzibar,Othman Bakari Othman Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Serikalini pamoja na Hamidu A.S.Mbwezeleni ambaye ni Wakili wa kujitegemea pamoja na Yessaya Kayange ambaye anakuwa Katibu wa Tume hiyo.

Pamoja na hayo Mrajisi wa mahakama alisema kuwa kazi kubwa ya Tume hiyo ya Utumishi ni kuajiri watu kushika nafasi za utumishi ikiwemo kuthibitisha ajira zao za utuimishi.

Akielezea kazi za Tume hiyo Mrajis alisema kuwa ni pamoja na kushughulikia na kupendekeza Serikalini mishahara na marupurupu ya watumishi wao pamoja na kuidhinisha nyongeza ya utumishi mpaka miaka miwili.

Kazi nyengine ya Tume hiyo ni kuthibitisha upandaji vyeo kwa wajiri pamoja na kushughulikia suala lolote lililopelekwa kwake na Waziri, Katibu Mkuu Kiongozi au Mkuu wa Taasisi kwa maamuzi au maelekezo.

Mnamo tarehe 31.1.2012 Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makugu alizundua rasmi Tume ya Utumushi ya Mahakama ili kuanza kufanya kazi zake ambapo leo amewateua rasmi wajumbe wa Tume hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...