Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi nyenzo za kazi Dkt James Msekela baada ya kuapishwa leo kuwa balozi wa Tanzania Italy.
Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Dkt James Msekela kuwa balozi wa Tanzania Italy leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Gharib Mohamed Bilal na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mh John Haule (kulia) na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Penaeli Lyimo (kushoto) na Dkt James Msekela baada ya kuapishwa kuwa balozi wa Tanzania Italy leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Dr James Msekela na Familia yake baada ya kuapishwa na JK kuwa balozi wa Tanzania Italy leo Ikulu jijini Dar.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakiongea na Dr James Nsekela na Mkewe baada ya Dr Msekela kula kiapo cha kuwa balozi wa Tanzania nchini Italy leo Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Kikwete akiongea huku Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto), wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), na wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakishuhudia Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto), wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), na wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu wakitiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali washuhudia awaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto)na wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi wakibadilishana nyaraka huku wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu akitazama baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwa katika picha ya pamoja na na Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto), wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu na wa Tanzania Dkt Hussein Mwinyi baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiongea na Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto), wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), na wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. JK tumekuona,kuna sehemu umekula "ze konooooz".Michuzi keshakufundisha "ze konooz"

    David V

    ReplyDelete
  2. Jk umezd ktoa fadhila..hv haknaga kbsa new-figures? Kila cku mnazungushiana nyie tu? Au kwa vle wengne baba zao hawajawah kuwa kwenye Nec,taa,tanu? Jamani mimi hapa nina miaka 3 ni graduate hata kazi cna maskini..nimeomba kazi hadi hela za kuphotocopy vyeti zmeisha..mara nyngne ntatma orijino kabisa..MUNGU WANGU NALIA..michuzi ictpe comment yangu.

    ReplyDelete
  3. Namfagilia JZ (Jacob ZUMA) kwa kumteua mtu muafaka wa nafasi ya Waziri wa Ulinzi huko kwao.
    JK alijaribu kidogo lakini Ban Ki-Moon akamzidi maarifa.
    Teh Teh Teh!!!!!!!!!!!!!!!!

    Abiola Jr.
    Mafia kiduka cha juice

    ReplyDelete
  4. Mzee jitokeze pia kwenye issue ya madaktari, hizi hafla zipo tu mzee. Afya za watu wako ndo muhimu zaidi.

    ReplyDelete
  5. Graduate Anonymous wa Tue Feb 07, 06:26:00 PM 2012

    Pole sana ndugu yetu kwa masahibu yaliyokukuta ya kukosa kazi licha ya Elimu stahili uliyo nayo.

    SULUHISHO LA HARAKA NA DHARURA,JARIBU KUJIAJIRI MWENYEWE KWANZA: ingawa ni vigumu kwa uchache wa uwezeshaji na mazingira tata tuliyo nayo: Kwa vile Serikali nyingi za Dunia zinazidi kubana matumizi ili kupunguza gharama za Utawala na madeni ya Serikali.

    Nafasi za Kazi Dunia nzima nchi zote 'NI NYINGI KISIASA' na zinaongezwa au kuahidiwa kuongezwa na Wanasiasa kipindi hadi kipindi hasa wakati wa Kampeni za Uchaguzi, Isipokuwa kiuhalisia Dunia nzima nchi zote 'NI CHACHE KISAYANSI AU KIUHALISIA' na zinatakiwa kupunguzwa kadri iwezekanavyo ili kurekebisha mwenendo wa Kiuchumi nchini, ndio maana unaoa WANA ZUNGUSHIANA WENYEWE KWA WENYEWE!

    ReplyDelete
  6. Mdau wa Tue Feb 07:06:26:00 PM 2012

    Graduate, ndugu yangu katika jitihada za kujikwamua kimaisha kabla ya ajira kulingana na taaluma uliyosomea,

    Jaribu haya hapa:

    1.Kuwa Dakitari wa Upasuaji kwa muda kwa kuuza Mafenesi (Fenesi lipo kama Binaadamu na wewe Muuzaji inabidi ulipasue kukata vipande vipande ukiwa kama Dakitari wa Upasuaji) huku ukisubiri maombi ya kazi kujibiwa.

    2.Fungua genge la Bamia na Dagaa ikkwezekana ktk baraza la nyumba unayoishi na uwe mbunifu kibiashara unaweza fanikiwa zaidi ya kazi ya ajira.

    3.Angalia zaidi shughuli za Ujasiliamali zilozo endelevu (zingatia tija na uwezekano kwanza) bila kujali Taaluma yako au kazi ya U Bosi wa kuvaa makoti makoti na matai matai.

    Kwa vile upo katika kipindi kigumu huku ukizingatia hali halisi tuliyo nayo tumia akili kichwani!

    ReplyDelete
  7. Umewahi kufikiria kuuza juisi? Dar joto!

    ReplyDelete
  8. Graduate Mdau wa pili hapo juu:

    Pole sana na kizaa zaa cha wimbi gumu la maisha kinachokukabili wewe na wengineo.

    Madai yako ni sawa, inapendelewa ninyi mpewe zaidi ila Wakubwa wamesha fanya utafiti wakaona Vijana wakipewa Mamlaka wengi hugeuka kama hapa:

    1.Wanaota mapembe Maofisini kwa kuwa wahujumu na wezi, wanakuwa jeuri na kiburi.

    2.Wanakuwa 'Vijogoo' ,unamkuta Kijana Mtumishi anataka atembee na wanawake Ofisi nzima tena wengine wake za watu bila kujali.

    3.Wanazalisha Mifarakano ,uchochezi na vurugu Maofisini.

    Mara nyingi wazee hujitahidi ktk uadilifu na hukaa kwa utulivi Maofisini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...