Rais Jakaya Kikwete akimsindikiza mjumbe maalumu wa Rais wa Urusi Bw. Mikhail V. Margelov mara baada mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo
Rais Jakaya Kikwete akiagana na mjumbe maalumu wa Rais wa Urusi Bw. Mikhail V. Margelov Ikulu jijini Dar es salaam leo.PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Mikhail V. Margelov, Mjumbe Maalum wa Rais wa Urusi, Mheshimiwa Dmitry Medvedev.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo, Jumatatu, Februari 13, 2012 Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amemtaka Mjumbe Maalum huyo kusaidia kushawishi makampuni zaidi ya Urusi kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.

Aidha, Rais Kikwete ametaka Tanzania na Urusi kuongeza ushirikiano wa kiuchumi katika nyanja mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua ambazo zitaongeza idadi ya watalii wa Urusi wanaotembelea Tanzania. Mwaka jana ni watalii 4,500 wa Urusi waliotembelea Tanzania.

Rais Kikwete na Mheshimiwa Margelov pia wamezungumzia masuala mbali mbali ya kimataifa, ya kanda ya Afrika na ya uhusiano kati ya Tanzania na Urusi.

Mjumbe Maalum huyo wa Mheshimiwa Medvedev anatembelea Tanzania ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika nchi za Afrika Mashariki za Kenya na Uganda. Alianza ziara yake kwa kutembelea Zanzibar jana na atakuwa Kenya kesho.

Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.
Dar es Salaam.
13 Februari, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. muheshimiwa hizo tiles za kuingilia lango kuu hapo mbona zimekaa kihasarahasara sana. hebu badilisheni mpango kidogo.

    ReplyDelete
  2. Dobi kanyosha trouser kisawasawa!

    ReplyDelete
  3. URUSI:

    Hawa ndio Washirika wenye Sera za wazi na tija katika mipango.

    Kiongozi wetu, ni wakati muafaka tukikaa nao kikazi zaidi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...