Rais Jakaya Kikwete akibeba tofali wakati alipotembelea kambi hiyo leo, katika hatua mbalimbali za kusaidia kufyatua matofali ya kisasa kwenye kambi ya mafunzo ya ujasiriamali na ujenzi kwa vijana 380 toka wilaya zote za Mkoa wa Pwani za Kibaha mjini Kibaha vijijini, Mafia, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji. (PICHA NA IKULU)
Rais Jakaya Kikwete akimwaga kokoto kwenye chekeche kwa ajili ya kufyatulia matofali.
Rais Jakaya Kikwete akifyatua tofali kwa mashine wakati alipotembelea kambi hiyo na kushiriki katika shughul;i mbalimbali za vinaja hao.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hatua mbalimbali za kusaidia kufyatua matofali ya kisasa kwenye kambi ya mafunzo ya ujasiriamali na ujenzi kwa vijana 380 toka wilaya zote za Mkoa wa Pwani za Kibaha mjini Kibaha vijijini, Mafia, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji.

Kambi hiyo ya mwezi mmoja iliyo katika kijiji cha Msoga, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ni moja kati ya kambi kadhaa zinazoandaliwa mkoani humo, ambapo ikimalizika hii ya ujenzi mnamo february 29, itafuatia ya upandaji miti na mazingira itakayokuwa katika Chuo cha Elimu Kibaha. Baada ya Hapo itafuatiwa kambi ya ukulima wa mazao ya mbogamboga wilayani Rufiji.

Rais Kikwete ameusifu mkoa wa Pwani kwa kubuni kambi hizo na kutaka mikoa mingine iige mfano huo ili kuwapa vijana ujuzi wa kuweza kujiajiri wenyewe.

Ameahidi kuendelea kusaidi vikundi vya vijana vya aina hiyo ambavyo amevitaja kama hazina nzuri ya maendeleo na utatuzi wa vitendo wa tatizo la ajira.

Rais Kikwete ametoa mashine za kufyatulia matofali ya kisasa 76 ambapo kila moja kati ya vikundi 38 vilivyopo vitapewa mashine mbili mpya na waliyofanyia kazi wataondoka nayo na kuwa ya tatu. 

Pia Amewapa vijana hao mifuko 3800 ya saruji (kila kundi mifuko 100), viatu vigumu (gum boots) pamoja na mananasi toka shambani kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hongra sana mkuu!..lkn. nadhani wana JF hawajaiona hii, ukasikia 'upupu' wao!..yaani wale jamaa? Mm nachoka hasa!

    Hawajulikani wanacho taka wala wasichotaka!

    ReplyDelete
  2. Hongera mh.raisi wetu kwa moyo wako mwema kwa watanzania, hiyo ndio njia nyepesi ya kuwapatia ajira kundi kubwa la vijana.

    ReplyDelete
  3. Good. Lakini inapaswa iwe endelevu. Na ili iwe endelevu, wizara ya kazi inapaswa iingize kwenye programu zake. Hongere kwa walioanza na hili wazo

    ReplyDelete
  4. safi sana president

    ReplyDelete
  5. JK umenikumusha mbali sana.Wakati nasoma shule ya msingi somo la siasa au sijui historia kulikuwa na kitabu kina picha ya Malimu Nyerere akitembea kutoka Butihama kuja Mwanza na kofia kama hiyo...

    David V

    ReplyDelete
  6. Mimi hii nimeipenda Rais JK KIKWETE ni mtu wawatu yaani kwenye mshikamano wawa tanzania yupo karibu nao

    ReplyDelete
  7. Safi sana Mr President, huko ndiko tulikojisahau na kuendekeza mambo ya nje. Hebu turudi huko na tuzalishe ajira zetu kwa pia kuzidisha mkazo katika kilimo. Sasa wale watu wa RITA waliokataa mavazi ya mapama mbona mheshimiwa raisi amevaa tena katika majukumu ya nchi? Kweli ofisi za Tanzania na viongozi wake kichwa panzi badala ya kuboresha utendaji wanaendekeza ujinga, Watanzania kibao hawana birth certificate halafu wanaendeleza urasimu. Shame!

    ReplyDelete
  8. Mdau UjerumaniFebruary 16, 2012

    Na we mchangiaji wa 1 huko Jamii Forum unatafuta nn?
    mi nikiwa na stress ndo hujaribu kuingia kule kusoma utumbo nipunguze stress. Ni kama kijiwe cha mateja kutwa kuongea utumbo tu. Ukitaka kujua hawana jema fuatilia mada zao, za kujenga hawana, wanajua umbea,uzushi na uchochezi wa kidini tu. Tena wana watu wao, mtu akitenda jema hata liwe vipi mradi c wa kwao watatukana tu. Waache waliwazane watuachie JK wetu

    ReplyDelete
  9. Kofia, sawa: Shati, sawa japo liko kichadema kidogo,: Suruiali, Mhhhh, kiatu, mhhhhh. Next tuime Presidaa apigwe had hat na jeanz kabisa apige mzigo for about two hours kama nyerere vile.

    Ila hii imetulia siyo kila siku yuko Davos

    ReplyDelete
  10. good job mr president,asante sana.
    kweli naamini mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe."ask not what your country do for you,ask what you can do for your country"
    huo mfano mzuri,kujiwezesha.
    mwalimu jk alisema....(it can be done play your roll)sasa mhe rais anatoa changamoto,shukrani kiongozi.
    mdau washington

    ReplyDelete
  11. NASEMA UKWELI.
    HII NI PICHA BORA YA RAIS WANGU YENYE KUVUTIA NA KUHAMASISHA KULIKO ZOOOOOTE.

    MAINA A. OWINO
    CCM UK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...